Uchaguzi 2020 Ingekuwa katika Nchi za wenzetu, Nyalandu na wenzake wangejitoa na kumuachia Lissu

Sina imani na wajumbe wa mkoani wa CHADEMA, nina wasiwasi wanaweza pindua meza na kumpiga chini Tundu lissu.
 
Anaweza kupata kura za aibu hiyo Jumanne.

Nikuambie Waziri wa Vitalu vya maliasili alishaumaliza huu Mchezo zamani?Fedha fedha mikoani?
ingawa hana uwezo kwa Lisssu lakini ndo hivyo kuna Mjumbe hapendi nyumba au piki piki?
 
Lissu angekubalika angekuwa Mwenyekiti
 
Acha demokrasia ifanye kazi yake.

Mbona CCM alipochukua fomu mmoja tu tumepiga kelele sana?

What if waliona anafaa wakamwachia?

Tuache double standard
Hapa ndipo utaona mapungufu yao.

Sasa nyalandu ajitoaje wakati ni haki yake?
Mimi naangalia hili picha linavyoenda na usikute Nyalandu atashinda kura za maoni ila watamkata jina lake.

Wanajua kutoa kibanzi kwa CCM tu ila maboroti yao hawayaoni .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kwanini ajitoe?
Hana Haki ya kugombea?
Wakimtoa watakuwa watu wa hovyo Sana kuwahi kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I can see the logic ni kama unatuambia Magufuli alihonga ili achukue fomu peke yake.
 
Hivi unaelewa maana ya kujitoa?Kujitoa unajitoa law hiari yako na ni kawaida kabisa na.sio kwa kushinikizwa.

Watu wagumu kue!ewa!
 
Ingelikuwa ni nchi za Wenzetu
Mwenyekiti wa Kudumu Chadema Asingeweza Kuzuia wengine Kugombea kiti hicho na kuwa yeye miaka nenda Rudi
And so is Magu.. asingezuia Membe kugombea na wasingemfuta uanachama
 
Kwenye msafara wa mamba,hata kenge wamo!
Hivi nyie Nyalandu mnadhani ni mwenzenu? Nyalandu atarudi CCM muda muafaka ukifika. Mimi naweza nina uwezo mkubwa wa kujua watu wenye dhamira ya nia ya kuwa upinzani na watu walioko huko kimkakakati. Wapinzani kama wanajua kusoma alama za nyakati, mtu sahihi wa kusimamisha kwa sasa ni Membe. Lissu ni mzuri sana, na namkubali sana ila tu kwa kipindi hiki Membe ndiye aliye kwenye nafasi nzuri zaidi ya kukubalika na watu wa aina mbalimbali. Lissu anaweza kupata support kubwa lakini watu potential wa kumpigia kura ni vijana na wapinzani wakereketwa. Membe akiungwa mkono na Lissu atavutia wale mashabiki wa Lissu na wengine kutoka CCM na watu wasio na hisia kali za upinzani.
 

'Mimi naweza nina uwezo mkubwa wa kujua watu wenye dhamira ya nia ya kuwa upinzani na watu walioko huko kimkakakati.'

Na hapo hapo unasema tena:

'Wapinzani kama wanajua kusoma alama za nyakati, mtu sahihi wa kusimamisha kwa sasa ni Membe.'

Hakika dunia ina maajabu yake.
 
Of Course wewe utaona ni maajabu kwa sababu unadhani Membe amekuja upinzani kimkakati. Ni kweli asingekuja upinzani kama CCM mambo yangekuwa mazuri lakini hii haimaanishi kaenda huko kufanya hujuma. Najua watanzania ni wagumu sana na wengi hawana uwezo wa kutafakari na kupima mambo kwa kina bali kukariri na ndiyo maana baada ya Lowassa kurudi CCM wameshakaririshwa kuwa alienda huko kuhujumu. Ukweli ni kwamba Lowassa alikwenda upinzani akidhamiria na alikuwa tishio kubwa kwa walifanikiwa ku-kushinda na asingerudi huko kama siyo afya yake kuwa mbaya.
 
Sielewi unayaonaje ni mawazo ya hovyo kama wanachama, wapenzi na washabiki wengi wa Chadema wanataka Lissu ndiyo abebe bendera ya Chadema kugombea nafasi ya Urais.
Ni mawazo ya hovyo kutaka Nyalandu ajitoe.
Kwani Hana Haki ya kugombea??
Mbona mnataka atoke hata kabla ya kura ya maoni...hii ndiyo demokrasia mnayoipiga kelele kila siku??

Kwa staili hii upinzani hamji kushika dola .

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BAK njoo ujionee miujiza mzee baba.
 
'Ni kweli asingekuja upinzani kama CCM mambo yangekuwa mazuri'.

Roger that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…