Ingekuwa ni hotuba ya mwendazake ungesikia...

Ingekuwa ni hotuba ya mwendazake ungesikia...

Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
1,541
Reaction score
3,521
INGEKUWA HOTUBA YAKE TUNGESIKIA

Ndugu zangu! Nataka niwaambie ukweli. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Tusibaguane kwa vyama, dini na makabila yetu maana Maendeleo hayana Chama!

Kuhusu KODI; Wizara ya Fedha, Kitengo cha TRA nimeona hapa Bajeti yenu ya mwaka huu. Mmesema mnahitaji Billioni 27 ili muweze kutimiza vizuri majukumu yenu ya kukusanya fedha.

Hizo Billioni 27 nitaziweka kwenye Akaunti yenu wiki hii, ninataka kuona mnachapa Kazi kweli kweli tupate mapato mengi zaidi. Waziri ametoa ripoti ya makusanyo ya karibu Trillioni moja kwa mwezi uliopita, nataka kuona hata Trillioni mbili mwezi huu.

Nchi yetu hivi sasa tumefika uchumi wa kati, nataka tuwafukuze China na hata Amerika. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu; nataka Watanzania wanyonge wafurahie matunda yao.

Hapa kwenye TV; wanyonge wanaotazama LIVE wanakenua meno yote mpaka unaona magego ya mwisho. Unasikia maneno; huyu ni Yesu aliyechelewa kuja.

Mzee anaendelea; kuna watu wameficha hela. Nendeni mkazifukue. IGP uko hapa na wakuu wengine wa Usalama mko hapa. Kuweni wazalendo!

Makofi; Kwa! Kwa! Kwa! Waziri anainuka kwa tabasamu anashukuru halafu anakaa tena! Mkurugenzi wa TRA naye anainuka huku anatabasamu, anatoa heshima halafu anaketi tena!

Kuhusu UHURU WA HABARI: Kuna waandishi wa habari sio Wazalendo, wanaandika habari za kuichafua nchi. Kwa nini Waziri usichukue leseni zao ili wajifunze? Nchi hii ni yetu sote; tusibaguane kwa vyama maana Maendeleo hayana Chama!

Hii mitandao! Natamani malaika wangeshuka waizime ili tuchape kazi. Mimi nimejitoa kwa ajili ya wanyonge!

Kuhusu UHUSIANO WA KIMATAIFA: Uhusiano wetu wa Kimataifa uko imara sana. Inaonekana Waziri Kabudi unafanya Kazi nzuri sana huko! Nataka wewe uwe Mfano wa kuigwa.

Kabudi anainuka, kisha anainama kidogo kutoa heshima kwa Mkuu halafu anaketi tena!

Mkuu anaendelea tena; hata juzi Kiongozi wa China ametutembelea hapa kwetu na wiki ijayo, Kiongozi wa Madagascar anakuja tena hapa!

Mahusiano ni mazuri sana! Hata makinikia siku hizi hayaibiwi kama zamani. Sasa hivi wazungu wanalipa vizuri sana! Watanzania tuchape kazi.

Kuhusu COVID 19: Waziri na timu yako nawapongeza kwa kukamilisha mashine ya kujifukiza pale Muhimbili. Pelekeni huduma katika Hospital zote kubwa wapate hizo mashine.

Namuona Mama anatikisa kichwa kufurahia sifa za Mzee kwake!

Ningependa kuona, hata huko vijijini watu wanajifukiza na kupiga nyungu kweli kweli. Nataka kuwaelezeeni ukweli; hizo chanjo hapana. Hata sisi tutengeneze chanjo ili tuwauzie.

Francis M. Garatwa,
Vingunguti, Dar Es Salaam.
06 April, 2021.
 
IGP kamateni wahujumu uchumi wote kwasababu hao ndio wanatuchelewesha, nchi hii ni tajiri sana, nasema kwa dhati kabisa ya moyo wangu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Vita vya kiuchumi ni mbaya sana nimejitoa uhai wangu kwa ajili ya wanyonge, watanzania mniombee sana.

By Mwendazake.

RIP Mwendazake.
 
IMG-20210406-WA0059.jpg
 
Dah! weee jamaa bhana, upo vizuri kwenye kuwasilisha hotuba za mwendazake, yaani unagonga mule mule....
Mwendazake: Nimejisakirifaisi maisha yangu kwa ajili ya watanzania maskini...
Machinga: Kweli baba wewe ni jembe..
 
Watanzania wamezoea utapeli hata kaz ya magu inaonekana ulikuwa utapeli
 
nimecheka sana leo aisee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mbavu zangu..... " Maendereo hayana chama! ... sitowabagua kwa vywama, dini.... ila huwezi kumpa mtoto wa jirani chakura kabula wako hajala...."

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom