Ingekuwa ni jambo la kimataifa, serikali ingeshindwa mahakamani na pengine kutakiwa kuwalipa fidia Wanufaika wa Bodi ya Mikopo

Ingekuwa ni jambo la kimataifa, serikali ingeshindwa mahakamani na pengine kutakiwa kuwalipa fidia Wanufaika wa Bodi ya Mikopo

Kuna mambo mengi mnayo sifia Serikali ya Rais SSH kuyafanya, miongoni ya hayo ni "Kufunguliwa kwa nchi", Diplomasia ya Uchumi and so on, yaani kana kwamba Nchi ilifungiwa,na palikuwa hakuna "Diplomasia" which is bogus, kwani mpaka sasa hakuna anyejua maana halisi ya "Diplomasia ya Uchumi" hakuna anyejua inafanya nini na wala anayejua wanafikiaje hiyo "Diplomasia ya Uchumi" Kwa kifupi ni kelele tupu. Kelele za Chura. Ni propaganda tu.

Kudai kwamba Serikali ya Hayat Rais Magufuli iliongeza percentage bila ya kuzingatia sheria ni Bogus! Kama ni kweli aliyayafanya yalikuwa na makosa kama mnavyodai alifungia nchi na sasa imefunguliwa, nibkitu gani hasa kinachomshinda au kinachowashinda Serikali hii kutengua au kufanyia marekebisho Sheria unayodai ilibadilishwa?

Ni Sheria gani hiyo Iliyobadilishwa?

Nini haswa kilichobadilika, Sheria au Mkataba?

Kuongezeka kwa percentage ni badiliko la Sheria?

Tuwekee huo mkataba hapa na hiyo Sheria unayodai ilibadilishwa, zaidi ya hapo mada hii itabakia kuwa kati ya mada nyingi zinazojengwa kuchafua Serikali ya Hayat Magufuli kwasababu ya vinyongo na visasi binafsi vya Mafisadi, Mamluki, Mawakala na Vibaraka wa Majambazi na Mabeberu.

Bogus!

"Serikali ya awamu ya tano chini ya Magafuli, wakabadilli sheria na kuongeza kiwango cha makato kutoka asilimia 8 mpaka asilimia 15 ya sasa na sheria imekuwea ikitekelezwa bila kujali mkataba baina ya mkopeshaji na mkopeshwaji."
Inshort umejidhalilisha🤣🤣
 
Mkuu punguza makasiriko,
Kuita mada ni Bogus ni Makasiriko? Ha ha
kwanini makato yalipanda kuanzia 2016 na pia wakaweka rentation kila mwaka deni likawa linapanda huwe umeajiriwa au hujaajiriwa, mfano mimi deni lilipanda mpaka milion 32 mwaka 2020, lakini baada yakuondolewa hizo rentation fees deni lilifika 17 milion kwanini nisishukuru.
Ina maana hukusoma Mkataba uliopewa. Ina maana ulikurupuka kupiga sahihi bila ya kusoma na kuelewa wajibu wako kama mkopeshaji. Ulisoma hiyo sheria hiyo inayodaiwa ilibadilishwa? Weka hiyo Sheria au Huo mkataba hapa turidhie, zaidi ya hapo, narudia, Madai yenu ni Bogus!

Hatahivyo, kama kulikuwa na makosa na hitilafu kisheria au kwa mahesabu, hayo makosa au hitilafu haya dondokei moja kwa moja kwa Raisi.
 
Mbali na hayo ya HESLB Umeshaona wapi hayo?? Kuwa wanufaika wa mikopo wanajadiliana na Mkopeshaji, umeona wapi?
Mfano wewe ni mwajiriwa wa serikali unataka kukopa pesa labda milioni kadhaa je utakopeshwa tu bila kuangalia mkataba kipengele na riba na utarudisha kwa muda gani? Kama hakuna majadiliano basi hakuna ukopeshaji hapo.
 
Kuita mada ni Bogus ni Makasiriko? Ha ha

Ina maana hukusoma Mkataba uliopewa. Ina maana ulikurupuka kupiga sahihi bila ya kusoma na kuelewa wajibu wako kama mkopeshaji. Ulisoma hiyo sheria hiyo inayodaiwa ilibadilishwa? Weka hiyo Sheria au Huo mkataba hapa turidhie, zaidi ya hapo, narudia, Madai yenu ni Bogus!

Hatahivyo, kama kulikuwa na makosa na hitilafu kisheria au kwa mahesabu, hayo makosa au hitilafu haya dondokei moja kwa moja kwa Raisi.
Kwanini kipindi cha kikwete kurudi nyuma mabro walikuwa wanakatwa 8% kulingana na mkataba lakini hawamu ya tano mambo yakabadirika ghafla.
 
Kwanini kipindi cha kikwete kurudi nyuma mabro walikuwa wanakatwa 9% kulingana na mkataba lakini hawamu ya tano mambo yakabadirika ghafla.
Lipi ni Lipi? 8% 9% Mkataba? Sheria? Kikwete? Magufuli? Samia?
 
Awamu ya tano chini ya Rais wa wakati huo, Marehemu Magufulli, ilikuwa kinara wa kukiuka sheria na kuvunja mikataba na matokeo yake leo hii serikali inashitakiwa huko katika mahakama za kimataifa na nchi kushindwa kesi na kulazimika kulipa mabilioni ya shilingi kama fidia.

Walichokifanya katika kuvunja mikataba ya kimataifa, ndicho walichokifanya katika kubadili sheria/taratibu inayotumika kuamua kiwango cha kukata mshahara kwa ajili ya kulipia deni la Bodi ya Mikopo.

Kwa wasiolewa, miaka ya 2016 kurudi nyuma, mkataba kati ya Bodi ya Mikopo na Wanafunzi ambao ni Wanufaika wa mikopo hii, ulielekeza Mnufaika kukatwa asilimia 8 ya mshashara wake ghafi(basic salary) ili kulipia mkopo wake kila mwezi na siku zote mambo yalienda hivyo kama mkataba unavyosema.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Magafuli, wakabadilli sheria/taratibu na kuongeza kiwango cha makato kutoka asilimia 8 mpaka asilimia 15 ya sasa na makato yamekuwa yakifanyika bila kujali mkataba baina ya mkopeshaji na mkopeshwaji.

Hivyo, jambo hili lingekuwa ni jambo la kimataifa, serikali ingeshitakiwa na wangeshindwa kesi na wangelazimika kuwalipa fidia wanufasika wote wa Bodi wanaokatwa/waliokatwa viwango tofauti na jinsi mkataba unavyoeleza unless mkataba ulikuwa unaruhusu mkopeshaji kubadili asilimia ya makato wakati wowote bila ridhaa ya mkopeshewaji jambo ambalo sidhani kama lipo kwenye mkataba.

Humu ndani hata mkiishitaki serikali na ikashindwa kesi, bado wanaweza tu wasitekeleza hukumu ya mahakama na watu mkaishia kulalamika tu.

Hii ni sababu nyingine kwanini watanzania tunahitaji katiba mpya.
Umeandika vizuri sana ila ulipofika mwisho ukaingiza utumbo eti katiba mpya. Maendeleo yanafanyika hata bila hiyo katiba mpya yako unayoitaja, ambayo si ajabu hujui hata iliyopo inasemaje.
 
Back
Top Bottom