Ingekuwa ni Kenya, hivi ule muswada uliotokana na pendekezo la Mama Salma Kikwete kuwa "wapenzi" wa viongozi nao walipwe ingekuwaje?

Mama Salma alienda kuongea tu kwasababu anayo nafasi ya kusema.

Waliopanga mipango ni wajane wa hao viongozi, na walishaongea na SSH kuhusu shida zao. Mwenzao akaenda kuwaongelea tu, asipakwe matope tafadhali.
Hivi mjane kama Anna Mkapa anapata shida gani?
 
Ni uroho, unyang'anyi na uporaji uliorasimishwa, ila wahenga walishasema:
"Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha"
Haya mambo ni kama masihala hivi, sikutegemea yangeweza fikia hatua ya kwenda Bungeni hadi Ikulu.
Zilianza Nchi za West Africa Mapinduzi, Kenya, Iko siku Tanzania.
Kwa Tanzania Kuna haya:
1: Kikokotoo
2:Hilo la kujilimbikizia mali kama la wake za Wastaafu
3:Rushwa
4:Mambo yasiyo na uhalisia yanayopandisha gharama za Maisha bila sababu za kueleweka,mfano, Sukari kupanda Bei,Mafuta, Vifaa vya Ujenzi ambapo Nchi zinazotuzunguka mambo hayo hayatikei
5:Utekaji na upotevu wa watu bila Maelezo ya Msingi nk
Mambo haya yakiachwa yakue na kuayafumbia macho Kuna siku naona kabisa watu wanaweza kuleta shida
 
Nchi inaliwa na wenye visu vikali, kama huna unaweza kubahatika kurushiwa hata mfupa ukikubali kuws chawa.
Fupa la kongoro siyo. Hahaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…