Ingekuwa wewe ungefanya nini?

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,715
Reaction score
8,058
Mjumbe wa nyumba 10 mtaa fulani katusimulia kuwa kaletewa kesi kuwa jamaa kaoa, ila kaenda gesti na mchepuko siku ya krismas. Baada kumaliza yao akaondoka lakini kasahau simu ?. Muhudumu akahifadhi ile simu, sasa mkewe akawa anapiga muhudumu akapokea tu akasema simu mmesahau hapa gesti fulani (kaitaja jina) mlipolala, mke akachua bodaboda akaenda kuichukua akarudi nayo nyumbani katulia akatulia nayo. Jamaa karudi gesti kaambiwa simu uliacha lakini mkeo alipiga hatukujua tukamweleza, kaichukua kaondoka nayo, Sasa unaambiwa jamaa leo toka krismas hajarudi nyumbani anaogopa kurudi atafanyaje!. Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Toa maoni yako...
 
Mambo yote yanazungumzika labda kama mke wake ni bondia,,,,,sipati picha mke nae atakuwa anamsubiri jamaa kwa style ya "RUDI NYUMBANI KUMENOGA"
 
Naenda polisi napiga mchongo na afande Chacha Mwita Marwa anifungulie kesi ya wizi,then nachukua na rb kabisa.
 
Na Mimi Namtengezea Mchongo Wa Kumfumania! Namwandaa Kijana Namuweka Sawa Kuanzia Meseji Mpaka Fumanizi, Halafu Ngoma Inakuwa Droo
 
Na Mimi Namtengezea Mchongo Wa Kumfumania! Namwandaa Kijana Namuweka Sawa Kuanzia Meseji Mpaka Fumanizi, Halafu Ngoma Inakuwa Droo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…