Ingekuwaje kama Kiingereza kingefanywa lugha ya JF?

Ingekuwaje kama Kiingereza kingefanywa lugha ya JF?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nafikiri, ingeweza kuwa na manufaa kwa JF kama taasisi, lakini isingekuwa na faida kwa Watanzania wengi.

1. Wana Afrika Mashariki wengi: Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, n.k., wangeweza kujiunga na JF. Na Watanzania wangekuwapo pia ila idadi ingekuwa ndogo sana.

2. Ingekuwa na watumiaji wengi toka sehemu mbalimbali duniani zaidi ya ilivyo sasa.

3. Ingekuwa na members wengi zaidi ya ilivyo sasa.

Ingawa ingeweza kuwa na faida nyingi kwa JF kama taasisi, lakini sipendekezi wabadilishe uwe mtandao wa English. Kama walivyoinesha uzalendo tokea mwanzo, waendelee nao hata sasa.

Pongezi kwao kwa kuweka mbele maslahi ya Watanzania wengi badala ya fedha.
 
Nafikiri, ingeweza kuwa na manufaa kwa JF kama taasisi, lakini isingekuwa na faida kwa Watanzania wengi.

1. Wana Afrika Mashariki wengi: Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, n.k., wangeweza kujiunga na JF. Na Watanzania wangekuwapo pia ila idadi ingekuwa sana.

2. Ingekuwa na watumiaji wengi toka sehemu mbalimbali duniani zaidi ya ilivyo sasa.

3. Lingekuwa na members wengi zaidi ya ilivyo sasa.

Ingawa ingeweza kuwa na faida nyingi kwa JF kama taasisi, lakini sipendekezi wabadilishe uwe mtandao wa English. Kama walivyoinesha uzalendo tokea mwanzo, waendelee nao hata sasa.

Pongezi kwao kwa kuweka mbele maslahi ya Watanzania wengi badala ya fedha.
Kwa hiyo unataka kusema nini?
 
......wazee wa kuongea pumba fasta tungerudi fb, mijadala ingekuwa serious, memba wengi kutoka nje ya nchi wangejiunga, waswahili tungepungua, siasa za kimataifa zingetawala, wajanja wangepata connection za nje....so kungekuwa na faida na hasara........
 
Back
Top Bottom