Ingekuwaje laiti tungeishi katika ulimwengu ambao hatuogopi kujajiwa au kuhumiwa

Ingekuwaje laiti tungeishi katika ulimwengu ambao hatuogopi kujajiwa au kuhumiwa

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Ebu fikiria unaishi maisha ambayo hakuna anayekujaji kwa matendo yako,wala huofii watu watasemaje kuhusu mambo yako,bilashaka ungekuwa ulimwengu mmoja amazing sana.

Lakini bahati mbaya sana tunaishi kwa kujajiana sana kwa kila matendo tunayofanya,mfano ukiwa mtoa ushauri mzuri utaambiwa unajifanya unajua kila kitu,ukiwa mtu wa kusamehe na mpole wa nyoyo kwa watu utaambiwa wewe ni laini na dhaifu.

Nadhan mpaka hapo msomaji wangu utaona jinsi tulivyozoea kujajiana,haya maisha ambayo kwa wale wasio jitambua ni rahisi sana kukata tamaa na kushindwa kufanya mambo flani katika maisha yao kwa kuogopa hukumu za watu,inahitaji mtu ambaye anajielewa kuweza kuishinda hii tabia.

Mfano hivi ni nani alisema raba unavaa na jinsi au kadeti au kodrai tu,,kwanini huwa tunahukumiana pale mtu akivaa raba na suruali ya kitambaa,huo ujinga mimi siutaki kwasababu kwangu mimi,fasheni ni ile ambayo inanifanya niwe comfortable maadam tu sivunji tamaduni na desturi zetu

Ni kawaida sometime kunikuta nimetinga raba kali na suruali ya kitambaa,yaan wewe nijaji tu kwa kuniona labda nimekosea,,sikubali ujinga au maamuzi ya watu wengine wanipangie namna ya kuvaa.

Hao walioona labda raba inaendana na jinsi au kadeti ni maono yao na mapenzi yao lkn mapenzi yao yasinifanye mimi nishindwe kuvaa vile ninavyopenda maadam tu sivunji tamaduni na mila zetu

Huo ni mfano mmoja,kuonyesha ni kwa namna gani tumezoea kuendeshwa kwa maoni ya watu wengine na kukubali watujaji katika namna wanayo taka wao.

Lau tukianza leo kuishi katika namna ambayo hatuogopi sijui watu wengine watatuona vipi,naamini kabisa tutakuwa watu huru na kuepukana na huu utumwa,,hakika wengi wetu ni watumwa wa haya mambo ila tunatofautiana kiasi na aina ya mambo yenyewe

Lakini ukijiangalia wewe binafsi utajikuta kuna mambo huwa unahofia kuyafanya kwakuwa unaogopa huenda watu watakuonaje au watakujaji vipi.

Tukatae huu utumwa wa fikra na tuishi maisha yetu maadam hatuvunji desturi na tamaduni zetu,hatuvunji heshima ya mtu wala hatumkeri mtu.

Kumbuka maisha ndiyo haya haya

Ni hayo tu!
 
Unamzungumziaje Hassan Bomboko anayekamata dada poa??
 
Una hoja usikilizwe... Fikiria ungekua na dunia yako na copy zako kadhaa ingekuwaje?

Kwa mfano mkeo au mumeo angekuwa copyright ya akili yako na mawazo yako nini hatma ya maisha yenu hapa duniani?

natamani ingekua hivyo kwakweli... Cc Mahondaw
Nimeipenda hii
 
Una hoja usikilizwe... Fikiria ungekua na dunia yako na copy zako kadhaa ingekuwaje?

Kwa mfano mkeo au mumeo angekuwa copyright ya akili yako na mawazo yako nini hatma ya maisha yenu hapa duniani?

natamani ingekua hivyo kwakweli... Cc Mahondaw
Me hata mke wangu angekuwa copy yangu tungesumbuana tu....maana me mwenyewe najisumbua
 
Back
Top Bottom