Ingekuwaje tungepata uhuru mwaka 1919 baada ya Mjerumani kushindwa vita?

Ingekuwaje tungepata uhuru mwaka 1919 baada ya Mjerumani kushindwa vita?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Huwa najiuliza ingekuwaje tungepata uhuru mwaka 1919 baada ya Mjerumani kushindwa vita vya kwanza vya duni 1914 hadi 1918.

Kumbuka tungekuwa nchi moja na Rwanda na Burundi.

Je, tungetumia lugha gani shuleni. Kumbuka kingereza bado hakijaingia wakati huo ila Germany kwa maeneo machache.

Kabila kubwa kabisa ni hutu, sukuma na tusi. Je tungekuwa na amani hii? Kimaendeleo tungekuwa wapi?

Je, Zanzibar nayo ingeungana na taifa kubwa la zamani la mjerumani 1964?

Je, vita vya watusi na wahutu miaka ya 1950, 1970 na 1994 vingetokea?
 
Muingereza katurudisha nyuma sana,mjerumani angekaa mpaka 1961 tungekuwa mbali sana kama nchi za ulaya
Ila tusingepata uhuru kwa ukatili ule. Pona yetu ni 1919 baada ya yeye kufuzwa
 
tungekuwa kama ma black American Tu!
 
Muingereza katurudisha nyuma sana,mjerumani angekaa mpaka 1961 tungekuwa mbali sana kama nchi za ulaya
kwanin tusimuombe arudi au tusubiri tuone kama hawa wazee dubai labda watatupeleka mahala
 
aliezingua ni nyerere na sera zake hakuna kingine huwezi peleka unamaa kwenye jamii zilizolala wapelekee moto wa kibepari lazima wataamka na kujitafuta
 
aliezingua ni nyerere na sera zake hakuna kingine huwezi peleka unamaa kwenye jamii zilizolala wapelekee moto wa kibepari lazima wataamka na kujitafuta
Wengine wanadai kaleta usawa kwa kuondoa matabaka nchini.
 
Wengine wanadai kaleta usawa kwa kuondoa matabaka nchini.
angeweza kuweka usawa ila sera yake haikustahili ila tusilaumu sana tupambane kujitoa kwenye umaskini mmoja mmoja ukiwa na mali zako haya mambo hayaonekani kabisa
 
Back
Top Bottom