Ndugu zangu
Natumai nyote muwazima wa afya
Tunapoelekea katika Chaguzi za Jumuiya na Chama kama Vijana na wanachama tunao wajibu wa kukisaidia Chama na Jumuiya zake kupata Viongozi wenye sifa za ziada,
Kutokana na Maelekezo, Ushabiki na makundi huenda tukaangukia pabaya tukachagua Viongozi ambao ndani ya muda mfupi tutajutia maamuzi yetu na kusema ni kwanini tuliwachagua,
Kwasababu Maelekezo na ushabiki vinaweza kutusababishia kuwaacha Viongozi wazuri mno ambao wangeweza kutusaidia,
Maelekezo yatafanya tusiwe na Viongozi wetu ambao watatuheshimu na kutusikiliza na tutakuwa nguvu ya kuwawajibisha.
Maelekezo yanabagua watoto wa Masikini, wasio Koneksheni, wasio na wakubwa wanaofahamiana nao.
Maelekezo yataigawa Jumuiya na Chama kwasababu wengine wataona wanabaguliwa na hawana thamani,
Mh. Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu mama yetu Samia Suluhu alisema ya kuwa tuchague Viongozi bora zaidi watakaokibeba Chama.
Lakini kama hiyo haitoshi
Mh. Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati kuu Dr. Hussein Mwinyi naye ametuhusia tunapokwenda kuchagua Viongozi tusiangalie Urafiki, Undugu na kufahamiana bali tuangalie watu wanaofaa zaidi.
Najua mnanifahamu vema
Tumekuwa wote, nyakati zote katika kupambania na kusimamia Kweli na Haki kwenye masuala mbalimbali,
Hivyo nawaomba sana
Katika Uchaguzi huu tushirikiane kupambania na kusimamia Kweli na Haki kwasababu Kweli na Haki vinaposhinda kunakuwa na mafanikio.
Kwa Upande wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwenye nafasi ya Mwenyekiti Chama kimetuletea majina ya Vijana wetu wanne.
Vijana wetu wote ni wazuri,
Lakini kwenye kumpata Kiongozi bora tunatakiwa kumchagua mwenye sifa za ziada.
Kijana atakayeweza kuwa sauti ya Vijana wa Chama na Sauti ya Vijana wa Kitanzania.
Atakayeweza kusimama kwa Ujasiri kutetea maslahi ya Vijana.
Atakayeweza kusimama kwa Ujasiri kuipigania Jumuiya na kukipigania Chama.
Atakayeweza kuisaidia Serikali kwa kushirikiana na wenzake.
Atakayeweza kuaminika na Vijana wa CCM na Vijana wa Kitanzania.
Atakayeweza kuimarisha na kuiboresha Jumuiya yetu adhimu.
Atakayeweza kuwanadi wagombea wa Chama kwenye Chaguzi na akaaminika kwa wananchi.
Atakayeweza kuheshimu Vijana wa kila hali, kila jinsia, kila Imani na kila kabila pasipo kuwabagua wala kupendelea.
Kati ya Vijana hawa wa CCM tulioletewa Sifa hizi zinamwangukia
Injinia KASSIM Haji Kassu
KASSIM ni mcha Mungu,
Mwenye hekima, busara na mtu wa watu,
Mwenye kujali wengine kuliko kuitanguliza nafsi yake,
Mpambanaji mahiri asiyechoka,
Mwenye uwezo wa kuwasemea Vijana na kukisemea Chama,
Mwenye fikra za kimaendeleo kwenye Jumuiya, Chama na Taifa kwa Ujumla,
Mwenye sera na ajenda za kuibeba Jumuiya ya Umoja wa Vijana,
Anaaminika na kukubalika na Vijana
Kugombea kwake ni hamasa kwa Vijana wanaotokea Vijijini na Mikoani kuamini kuwa inawezekana kabisa kwa Vijana wa Vijijini kugombea na kupata dhamana ya kuongoza katika nafasi kubwa nchini
Injinia KASSIM Kassu tumeletewa kwa wakati na majira sahihi hivyo ni ombi langu kwenu Vijana wenzangu tumuunge mkono kwa kumchagua kwa kura nyingi awe Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM)
Aliyewaokoa watu kwenye ndege Bukoba anaitwa Majaliwa
Anayekwenda kuivusha Jumuiya yetu anaitwa KASSIM
Kwa heshima na taadhima nawaomba ndugu wajumbe wa Mkutano mkuu UVCCM Taifa tumchague Injinia KASSIM Kassu kuwa Mwenyekiti wetu UVCCM Taifa!
Ndugu yenu
Ibrahim Jeremiah
Mshamba wa Songea