Innocent Killer (The Revenge)

Innocent Killer (The Revenge)

STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA

SONGA NAYO................

Asp Bakari Zalimo alionyesha shauku kubwa sana ya kuhitaji kujua kama mheshimiwa hapo kwake alikuwa amefuata kitu gani mpaka akaja mida hiyo japo alikuwa anaelewa kwamba jambo hilo lilikuwa na muunganiko mkubwa sana na lile la kupatikana kwa Yasinta Kobe. Lakini akiwa kwenye hiyo shauku wakati huo mheshimiwa anapata kahawa taratibu walisikia ujio wa gari karibu na nyumba ya afisa huyo wa polisi, mheshimiwa raisi alitabasamu kwani alionekana kama alikuwa anajua kila ambacho kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.

Jason aliingia ndani ya nyumba hiyo kama alivyokuwa ameahidi kwenye barua ambayo aliipata Asp Bakari sasa hapo akawa ana uhakika kwamba mtu ambaye alikuwa amempigia simu alikuwa ni yeye moja kwa moja, hakuwa peke yake bali alikuwa ameongozana na moja ya hao vijana wake

“Shikamoo mzee wangu” Jason alimpa salamu zake mheshimiwa raisi huku akiwa anakaa, hata hakuwa na mshtuko mkubwa kumuona mzee huyo mahali hapo.

“Marhaba kijana wangu, kwema huko utokako?”

“MUNGU amekuwa mwema sana kwa upande wangu, naona umeamua leo uje unisubirie hapa hapa moja kwa moja”

“Yes lile tukio nilikuwa na uhakika kwamba lazima ni wewe umelifanya hivyo nilivyo ona taarifa ya kwamba ungekuja kumuona huyu kijana, nikaona ndiyo nafasi yangu kuweza kuongea na wewe machache ambayo nilikuwa nayo maana kwenye simu siwezi kabisa kukupata”mheshimiwa aliagiza kahawa nyingne ili aongee na kijana wake huku wote wakiwa wanapata kahawa ambayo iliandaliwa na mke wa afisa wa polisi huyo ambaye leo kwake ilikuwa ni kama maajabu kutembelewa na vigogo hao wa serikali.

“Yes nimefanya hivyo kwa sababu wakati huo nilikuwa kwenye hali mbaya sana jambo hili lilipo tokea na niliwaahidi wananchi kwamba jumatano ningewaletea mtu wao hivyo kulikuwa na ulazima kwamba wamuone akiwa amerudi kisha nimchukue tena na kumuweka eneo ambalo ni salama kwanza kisha mazungumzo na huyu askari nije niyafanye naye akiwa amameliza kazi na namshukuru sana hajaenda kinyume na maagizo yangu, nadhani ni moja ya maaskari wanao hitajika sana kwenye nchi hii na inabidi aangaliwe kwa jicho la pili ikiwemo kupewa ulinzi na maslahi ” Leo mkurugenzi wa usalama wa taifa alikuwa anampigia pande afisa wa polisi mbele ya mheshimiwa raisi, Bakari Zalimo alipata moyo sana kuweza kuzipata hizo sifa.

“Kumbe mawazo yangu hayakuwa mbali sana na nilichokuwa nakiwaza, nilijua tu utakuwa ni wewe ndiye ambaye umelifanya hili jambo. Ila naomba kwa leo kama utaniamini niujue uhalisia wako, maana kuna stori nazisikia sikia siziamini bado kama ni kweli, kwa umri nakuona kama kijana mdogo” Bakari Zalimo aliwahi kugusiwa na IGP kwamba kijana huyo ndiye mkurugenzi wa usalama wa taifa ila hakuziamini sana hizo taarifa ndiyo maana leo alikuwa anahitaji mhusika mwenyewe athibitishe mbele yake.

“Kama IGP amefikia hatua ya kuweza kukuaamini kuhusu hili basi haina haja ya kukuficha tena, mimi ndiye mkurugenzi wa usalama wa taifa hili, huenda hata mimi huwa nashangaa kama wewe kwa umri wangu kuwa hapa ila kuna mengi ambayo huwezi kuyajua huenda mpaka unakufa. Kwa hili ambalo linatokea inaonekana kiongozi wako anakuamini sana hivyo kwa kipindi hiki wakati yupo ndani wewe utaikaimu nafasi yake ili kusiwe na pengo kubwa kwenye upande wa majukumu maana siyo muda sana kazi inaanza rasmi” Jason aliongea kitu ambacho ni kama kilikuwa ni utani kwa Asp Bakari Zalimo, alikuwa amepata shavu la kupandishwa cheo cha nafasi ya bosi wake ambaye alikuwa kwenye nondo za gereza mpaka muda huo.

“Huyu kijana unaona anafaa kwenye hiyo nafasi?” raisi aliuliza kisha Jason akaitikia kwa kichwa.

“Haya nambie kilitokea nini na ilikuwaje ukajua eneo ambalo alihifadhiwa yule mwanasheria?”

“Wale ambao walilifanya lile tukio walikuwa ni watu wa jeshi”

“Watu wa jeshi? Ulitambua vipi hilo?”

“Siku ile ambayo walimteka yule mwanasheria mimi nilikuwepo lile eneo, nilifika pale ila kwa kuchelewa sana hivyo nilikuta tayari wametoweka lile eneo ila nilibahatika kupata kitambulisho cha mmoja wao ambacho alikidondosha. Nilienda kukifuatilia kwa umakini kile kitambulisho, ndipo nilipo fanikiwa kuwajua hawa watu”

“Ni watu kutoka kwenye kikosi maalumu ndani ya jeshi la wananchi ambalo lipo chini ya CDF”

“Maana yake hadi kwenye hili ni CDF ndiye anahusika?”

“Hilo ni asilimia miamoja”

“Huyu mpumbavu anaanza kujigeuzia nchi kama ya kwake, nitamvua ile nafasi na kumfanya kitu kibaya sana” mheshimiwa raisi aliongea kwa hasira sana kiasi kwamba mpaka Bakari Zalimo alianza kuogopa na kuelewa namna watu wanavyokuwa wanatumbuliwa kiwepesi sana pale ambapo mambo yanaenda kinyume na vile yanavyokuwa yanatarajiwa.

“Hapana hatutakiwi kabisa kufanya hilo kosa. Mimi kumuacha mpaka muda huu haimaanishi kwamba nimeshindwa kumchukulia hatua au kumkamata hapana, bali nahitaji kujua kwamba mtu huyu yupo nyuma ya nani? Anafanya kazi na watu wangapi? Hapo ndipo nitakuwa na uwezo wa kuamua hatima ya Maisha yake” Jason aliongea huku akishushia kahawa kidogo.

“Kama ni kusema walipo hao watu si ni suala la kumkamata na kumhoji kwa nguvu?”

“Mhhhh mheshimiwa mambo hayaendi kienyeji sana namna hiyo, idara yangu ina majasusi wengi sana ambao wana uwezo wa kuifanya kazi hiyo hata usiku huu kama nikiwatuma ila huyu mtu kuwa mkuu wa majeshi siyo mjinga, siyo mwepesi kama unavyosema wewe hapo. Yule kakaa kwenye hiyo nafsi kwa muda mrefu sana, lazima huko ametengeneza watu wake ambao wanampa kiburi na wanajeshi wanamsikiliza yeye kuliko hata wewe hapo sasa vipi kama tukifanya hilo kosa halafu nchi ikaingia kwenye machafuko? Utakuwa tayari wananchi wako waanze kufa hovyo kila eneo?. Hilo jambo mimi siwezi kuliruhusu kabisa kwa sababu kazi yangu kubwa ni kuhakikisha usalama wa nchi na raia kwa ujumla”

“Ninacho kifanya mimi wale watu nimeamua kuwapa ushindi wa usoni ila nataka niwafanyie kitu kibaya mno ambacho kitawafanya kila siku waanze kuiogopa bendera ya nchi hii watakapo iona. Nimewaaminisha kwamba wapo huru sana kwa mambo wanayo yafanya ili nizidi kuwajua wote kwenye huu mzunguko kwamba kuna nani na nani kisha ndipo nianze kujionyesha hadharani, nadhani moja ya makosa makubwa sana ambayo mimi niliyafanya ni kuishi muda mrefu kule”

“Ule muda umenicheleweshea mambo mengi sana na hata vijana wenyewe sielewi walikuwa wanafanya kazi gani maana taarifa zilizopo hazina uzito wowote, uchunguzi unafanywa kienyeji mno nahitaji nianze kuunda huu umoja upya. Kuhusu mkuu wa majeshi, acha aruke ruke kwa huu muda kisha tutaanza naye baada ya kuwajua wale wote ambao wapo nyuma yake japo nimemchukua mwanae leo”

“Unamaanisha nini kusema umemchukua mwanae?”

“Oden nipo naye kwenye gari muda huu”

“Sasa huyo anahusika nini kwenye hili?”

“Alituma watu waweze kuniua, sasa nataka nifahamu kwa undani kwamba kuna sababu ipi mpaka ahitaji mimi nife? Na kama kuna kitu anakijua basi nina uhakika lazima ataongea tu maana huyu namhoji mimi mwenyewe hivyo hana uwezo wa kunificha”

“Mhhhhhh yule mtoto mbona kama namuona mstaarabu sana, halafu na yule pacha wake si alikuwa kusoma?”

“Kwenye Maisha wale watu ambao huwa wanauaminisha upande wao mmoja ndio watu ambao huwa wanakuwa hatari Zaidi ya kitu chochote kile na ndio hao ambao siku ukija kuwaelewa vyema unabaki umeachama mdomo. Hilo nitalithibitisha baada ya kuongea naye, na kuhusu huyo pacha ake mwanasheria nimemkuta akiwa mle ndani kwake wapo wote na kwa mazingira ambayo yalikuwepo pale ni kama dada mtu alikuwa anambana kwa maswali makali sana ila sikuwa na muda mrefu wa kukaa pale hivyo nitaongea na yule dada kwa siku zijazo” Jason alikuwa anaongea na mheshimiwa raisi kama rafiki yake wa karibu kwa sababu watu hao walikuwa wanajuana vyema sana.

“Na vijana wanarudi lini?”

“Mahesabu ilikuwa ni miezi sita ila naona kama itakuwa ni mbali sana, nawaza namna ya kuupunguza huu muda ili bosi anavyorudi asipishane sana na X ambaye ndiye namsubiri aniletee taarifa kamili ili nije kufunga mahesabu ya wadaiwa yangu” hao wadaiwa wake aliokuwa anawasema ni watu walio muulia ndugu yake pamoja na mheshimiwa raisi.

“Mimi kama raisi wa nchi nakupa baraka zangu zote, kwa sasa nakiacha kila kitu kwenye mikono yako kwa sababu hakuna mtu ambaye namuamini kwenye nchi hii Zaidi yako wewe hapo na ninapo kuona naona kabisa ushindi wa nchi ukija kwa kasi sana na kuamini kwamba haya mambo yataisha. Hili jambo naliacha kwako lakini muda wowote ukihitaji chochote kile Ikulu ipo wazi kwa sababu yako lakini mbali na hilo nina mambo mawili ya mhimu sana ya kuongea na wewe” kauli ya mheshimiwa raisi ilimpa uhakika Asp kwamba mwanaume huyo alikuwa anaheshimika isivyo kawaida kama tu mpaka mheshimiwa raisi anamkabidhi mtu jukumu la kuhakikisha usalama wan chi nzima huku yeye akiwa amekaa sehemu.

“Kwanza nadhani huyo binti Yasinta Kobe anatakiwa aje akae Ikulu kwa muda mfupi ili usijiingize kwenye jukumu la kupoteza muda wa kumlinda wakati inatakiwa uingie kwenye majukumu mengine ya kuilinda nchi, lakini jambo la pili nadhani unatakiwa ukaongee na IGP huko gerezani kisha mwambie anahitaji nini, kutoka au kuna mahesabu mengine anayo kwenye kichwa chake” mheshimiwa baada ya kuongea hivyo, maagizo yake yalikuwa yamekamilika hakuwa na la nyongeza.

“Kuhusu huyu binti kwa sasa anatakiwa kuwa kwenye mkono wangu atakuwa salama Zaidi, nina kazi naye sana ila kwa IGP ratiba yangu ni kwamba kesho mapema sana naenda kumuona kukiwa na mwanga tele”

“Kipi kinakufanya mpaka uhitaji kwenda kumuona ikiwa kila mtu anakuona?”
“Najua hawa wamefanya hivi kumkamata IGP ni kunipima mimi, nadhani wana habari zangu ila hawana uhakika kabisa hivyo wanahitaji kunijaribu ili waamini kama mimi ndiye, sasa hiyo kesho nataka nienda pale pale gerezani ambapo nina uhakika watakuwa wamewapenyeza watu wao wengi sana. Lengo la kwenda pale ni kuongea na IGP kisha niwaonyeshe ubinadamu wangu ambao nilishautoa mwilini unavyo fanya kazi, kesho kwa mara ya kwanza nina mpango wa kuwaonyesha namna mimi nilivyo na jinsi ninavyo fanya kazi”

“Mhhhh unataka ukaue hadharani?”

“Hapana, kwa sababu huyu tayari amekaimu ile nafasi ya IGP atazuia aina yoyote ya kamera mpaka nafika pale hivyo hilo jambo watalishuhudia tu ambao watakuwepo pale kisha nityaondoka na IGP”

“Una mahesabu gani baada ya hilo jambo?”
“Hapo najua wataanza kunitafuta kwa nguvu sana na nina uhakika hapo wataanza kutoka na wale ambao watakuwa wamejificha huko vichakani, sasa tutaanza na mmoja mmoja” mwanaume alikuwa anaongea akiwa siriasi sana mpaka hata Bakari Zalimo alianza kumuogopa japo alitamani sana kumuona huo uhalisia ambao alikuwa nao huwa unakuwaje.

Mheshimiwa raisi aliinua bendera na kumkabidhi Jason kisha akamkumbatia na kutoka humo ndani, hiyo ilikuwa ni ishara ya kumpa baraka zake kufanya yale ambayo aliyaona yanafaa kutoka kwa huyo kijana kwani alimjua vyema kwamba hakuwa mtu wa kukurupuka kabisa.

“Gari ambayo umeichukua muda ule utabaki nayo unaitumia, mimi nimekuja kukupa asante yangu kwa kazi uliyo ifanya. Kuanzia sasa wewe ni IGP mpaka pale zitakapo tolewa taarifa zingine, kesho najua nasubiriwa kwa hamu sana huko gerezani kwenda kumuona IGP hivyo nataka mapema sana uandae mazingira kule sitaki kuona mwandishi yeyote yule wala chombo chochote cha kupigia kamera”

“Mkuu sasa hayo mamlaka ambayo mmenipa ataniamini nani?” Asp aliuliza baada ya kuona Jason anaanza kuondoka.

“Kaa karibu na televisheni yako, mheshimiwa anaenda kutangaza muda huu hapa” mwanaume alimalizaia na kutoka humo ndani.

Kesho anasubiriwa kwa hamu sana na wanaume ambao walikuwa wanahitaji kujiaminisha kama kijana huyo alikuwa ana uwezo mkubwa sana kama walivyokuwa wanamsifia watu wachache, maana waliogopa kupoteza muda wao kwa mtu ambaye ni wa kawaida. Ni kweli kwake yaliyomo yamo?......86 inafika mwisho.

Wasalaam

Bux the storyteller.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Hii kitu ni [emoji91][emoji91] aisee
 
1500

Ukitaka kuisoma yote kwa pamoja mpaka mwisho, unalipia 1500 tu kwa sasa, nakutumia hapo hapo hata ukitaka kitabu kizima kwa pdf ukisha lipia nakupa.

Mwisho kabisa ni sehemu ya 135.

Unataka kujua huu mzigo ndani yake kuna mambo gani haswa?

Lipia ili uisome yote kwa pamoja.

Namba za malipo

0621567672 ....HALOPESA

0745982347 .....MPESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.

WhatsApp au kupiga 0621567672.

Muwe na asubuhi njema.
FB_IMG_1695616944502.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
1500

Ukitaka kuisoma yote kwa pamoja mpaka mwisho, unalipia 1500 tu kwa sasa, nakutumia hapo hapo hata ukitaka kitabu kizima kwa pdf ukisha lipia nakupa.

Mwisho kabisa ni sehemu ya 135.

Unataka kujua huu mzigo ndani yake kuna mambo gani haswa?

Lipia ili uisome yote kwa pamoja.

Namba za malipo

0621567672 ....HALOPESA

0745982347 .....MPESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.

WhatsApp au kupiga 0621567672.

Muwe na asubuhi njema.
FB_IMG_1695976883361.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom