Inonga Baka ataendelea kuumia endapo hatobadilisha style ya uchezaji, acheze kama Che Malone

Inonga Baka ataendelea kuumia endapo hatobadilisha style ya uchezaji, acheze kama Che Malone

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Natoa pole kwa beki wangu Inonga Baka, kitendo kilichofanywa na Hijja Ugando mchezaji wa zamani wa Simba hakikuwa cha makusudi wala dhamira ovu, Ugando alikuwa katika pilika za kumtoka Inonga ili akamuona Ayoub, Inonga wakati anataka kuondosha ball akakumbana na ajali kazini.

Binafsi nimekuwa nikimshuhudia sana Inonga akicheza kwa madoido na madaha, akicheza na jukwaa wamshangilie, mara kupiga chenga mahali pasipotakiwa kupiga chenga basi ali mradi tu akae nao mpira.

Uchezaji wake unamsababishia sana ajeruhiwe tofauti na Kennedy Juma au Che Fondoh Malone, uchezaji wa wawili hao ni nadra sana kuumia, hawana mbwembwe wala nn, wao ni kazi kama Joash Onyango.

Bro punguza mbwembwe utaumia sana msimu huu

1695339039277.jpeg

Natoa pole kwa beki wangu Inonga Baka, kitendo kilichofanywa na Hijja Ugando mchezaji wa zamani wa Simba hakikuwa cha makusudi wala dhamira ovu...
Sababu ulizozitaja hakuna hata moja onayohalalisha au kusababisha mchezaji kuumizwa. Unataka kusema Che Malone na Kennedy huwa hawaondoshi hatari?

Mbona ile rafu sioni uhusiano na chenga? Halafu kama ni chenga, mbona Che Malone anahadaa washambuliaji kuliko Inonga? Binafsi naona kama umekurupuka kuanzisha Uzi, maybe una dhamira nyingine
 
Kweli [emoji817]
 
Kuumia au kuumizwa kwenye mihangaiko ya maokoto kawaida Kwa Mwanaume,,,Sisi ni mateso tuu kwenda mbele na ndio asili tangu na tangu
 
KIUFUNDI labda nijaribu kufanua kitu kinachoigharimu sana Simba.

Simba Hawana Kiungo No 6
Hivyo Basi safu ya Ulinzi ya Simba Inakuwa inafikiwa Kila Mara.

Mabeki WA kati na wapembeni wataonekana kama hawaelewani, wamechoka, na kucheza ama kuchezewa rafu nyingi sana. KUUMIA ama Kuumiza wachezaji wenzao.

SHIDA YA SIMBA NI KUKOSA CDM KIUNGO MKABAJI WA ULINZI
 
Ni ajali kazini tu.
Kapombe aliandamwa na majeraha na hakuwa na mbwembwe,Humud,Mo Banka,Nampoka Nyumba walikua na mbwembwe lukuki lakini awakua wakiumizwa sana.

Victor Costa alikua anapunguza mtu ndani ya boksi la kipa.
 
KIUFUNDI labda nijaribu kufanua kitu kinachoigharimu sana Simba.

Simba Hawana Kiungo No 6
Hivyo Basi safu ya Ulinzi ya Simba Inakuwa inafikiwa Kila Mara.

Mabeki WA kati na wapembeni wataonekana kama hawaelewani, wamechoka, na kucheza ama kuchezewa rafu nyingi sana. KUUMIA ama Kuumiza wachezaji wenzao.

SHIDA YA SIMBA NI KUKOSA CDM KIUNGO MKABAJI WA ULINZI
Si yupo Kanoute
 
Back
Top Bottom