Inspekta Mkuu wa Polisi Kenya athibitisha, mwanablogu Albert Ojwang alizuiliwa rasmi katika kituo kikuu cha polisi Nairobi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya, Douglas Kanja amethibitisha kuwa mwanablogu, Albert Ojwang alizuiliwa rasmi katika Kituo Kikuu cha Polisi chini ya OB nambari 136/7/6/2025.

Kanja alisema kuwa Ojwang alikamatwa kufuatia malalamishi yaliyowasilishwa na Naibu Inspekta Jenerali Eliud Lagat, ambaye alimshtumu kwa kumharibia jina.

Baada ya kukamatwa, Ojwang alihojiwa Jumamosi kabla ya kuhamishwa hadi kitengo cha kuzuilia ndani ya kituo hicho.

Hata hivyo, kulingana na ripoti, polisi baadaye walimpata akiwa amepoteza fahamu katika seli yake na kumkimbiza katika Hospitali ya Mbagathi, ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) imeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo, huku mwenyekiti wake Anne Makori akizuru kituo hicho kutathmini hali ilivyo.

 
Hata Tanzania kulipaswa kua na chombo huru cha kuichunguza polisi na vyombo vingine vya usalama pake wanapo fanya uhalifu hata ikiwa ni kutoka nje ili kuwabana vizuri, kenya wabakosea kwenye mengi lakini kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…