Institute of finance management

Institute of finance management

Kichwa ndio mtu ama kweli yeye ana kichwa tu hana tumbo wala miguu. Kama IFM inatoa elimu mbovu mbona CRDB all most kila mwaka ajira zao wanapitisha IFM kwanza? Pia mbona still wahitimu kutoka IFM wanaajiriwa sehem mbalimbali. Be a grown up man maswala ya kucredit vyuo waachie TCU wewe haya kuhusu. Afu inaelekea ww ni mwanafunzi sisi tuliosoma pale mbona tupo makazini sasa.?
Hili jukwaa kwa style hii halifiki popote..
 
Ndg yangu Kichwa, ni bora ukafika IFM ukapata utaalam wa kufanya tafiti. Kwa kifupi tu ni kwamba, moja ya taasisi bora zinazojihusisha na utoaji wa elimu ni IFM. Ushahidi, jaribu kufuatilia wahitimu wa kada ya Uhasibu. Mbali na kuhitimi Shahada, Stashahada ya Juu ama Shahada ya Uzamili, mhitimu anahitajika kufanya mitihani ya bodi ya uhasibu, NBAA ili aweze kutambulika kama 'Professional Accountant'. Angalia 'trend' ya ufaulu wa mitihani ya bodi utajua nn namaanisha. Hiyo haitoshi, zunguka maeneo yote yanayotoa ajira iwe ni selikalini au katika mashirika, kampuni ama taasisi binafsi angalia wahitimu wa IFM walivyojazana huko. Hiyo haitoshi fika IFM uone waajiri mbalimbali walivyosambaza 'offer' za ajira kwa wanaohitimu IFM katika fani mbali mbali. Issue ya 'Past papers' katika taasisi za elimu ni jambo la kawaida sana kwani linamfanya mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujibu maswali ya aina mbali mbali. Mtu kushindwa kufanya vizuri katika 'interviews' sio kwamba hajui, huo ni udhaifu wa asilimia kubwa ya watanganyika, aah samahani, watanzania katika mambo yanayohusu 'interviews'. Kuhusu walimu wenye elimu kiwango cha shahada ya kwanza kufundisha IFM, sioni kama kuna tatizo. Kila mwalimu ana majukumu yake kulingana na kiwango cha elimu aliyonayo. Kwa kifupi IFM inatoa elimu kuanzia kiwango cha astashahada mpaka shahada ya uzamili. Usifikiri kila kitu kinafundishwa na Professors, ingekua umepitia elimu ya huko juu hasa vyuoni, nadhani hili lisingekuwa kwenye mada yako. Aidha unaweza ukafika IFM ukapata elimu iliyobora kwa maendeleo ya taifa letu. Karibu....
 
IFM haipo kama mnavyoifikiria mnaongea tu kwasababu hampo mle ndan,ila waliopo mle wanajua stress za pale..naamin mtu anaeingia pale hawezi akatoka mtupu lazima awe amejifunza mengi..
 
Kichwa ndio mtu ama kweli yeye ana kichwa tu hana tumbo wala miguu. Kama IFM inatoa elimu mbovu mbona CRDB all most kila mwaka ajira zao wanapitisha IFM kwanza? Pia mbona still wahitimu kutoka IFM wanaajiriwa sehem mbalimbali. Be a grown up man maswala ya kucredit vyuo waachie TCU wewe haya kuhusu. Afu inaelekea ww ni mwanafunzi sisi tuliosoma pale mbona tupo makazini sasa.?
Hili jukwaa kwa style hii halifiki popote..

Kaka naona umepanic
 
Back
Top Bottom