Shirika la Uchunguzi la Mtandao la NetBlocks limethibitisha kuwa Data ya Mtandao ya moja kwa moja inaonyesha kuna usumbufu mkubwa wa muunganisho wa Intaneti Nchini Kenya, ikiwa ni siku moja pia tangu Mamlaka kudai hakutakuwa na kuzimwa kwa Mtandao.
Watumiaji mbalimbali wa Mitandao hasa wa X (zamani Twitter) wameandika kuwa wanalazimika kutumia VPN ili kuendelea kupata uwezo wa kutumia Intaneti
NetBlocks imeeleza changamoto hiyo ya Mtandao inayoendelea inadaiwa pia kuathiri Nchi Jirani zikiwemo Uganda na Burundi, hali hiyo inadaiwa inaweza kupunguza utangazaji wa matukio ya maandamano yanayoendelea