Intaneti imezidi kupanda Bei

Intaneti imezidi kupanda Bei

Jana, nimenunua 640 MB kwa sh. 1000 lakini kuamka asubuhi 350 MB Ni kwa hiyo 1000. Kwa hiyo gharama imepanda mara mbili ndani masaa machache. Yote haya Ni kwa sababu upinzani wa Rais upo mtandaoni.

Hili balaa lilianza Baada ya huyu Rais kuingia madaraki. Kutokana na kusemwa sana akaanza kupandisha virushi.

Enzi za Magufuli kwa sh. 500 unapata 1GB - 500 mb , na alisisitiza sana taasi za serikali kuhamia mtandaoni.
Hii ilichangia ongezeko la internet users.

Madhara ya kupunguza watumiaji wa intaneti Ni makubwa :-

Kuwa na lundo la wasomi wasioendana na kasi ya duniani (wasomi wa vitabu).
Uhaba wa ma-programmer
Mifumo itakuwa ni analog
Hivi Leo Kuna watu ni matajiri kutokana tu na kucheza game online, (Ninja).
Umesahau vifurushi vilianza kupanda baada ya waziri mteule wa Magufuli kuagiza TCRA waweke bei elekezi za bundle?
Hivi watanzania tuna kumbukumbu fupi hivi?
 
Mwenye ttcl aje na elfu kumi ya kitanzania atoke kwenye malalamiko..😂
 
Nimegundua kuongopewa ni rahisi sana.
Jaribu kufanya alichosema huyo alafu leta mrejesho. Vifurushi vimepanda sana wala halihitaji kuzungukazunguka
Wewe hujielewi aliyesema vifurushi havijapanda ni nani?

Matumizi ya 3G na 4G yanaweza kuwa sawa? Utakuwa una tatizo kichwani.
 
Umesahau vifurushi vilianza kupanda baada ya waziri mteule wa Magufuli kuagiza TCRA waweke bei elekezi za bundle?
Hivi watanzania tuna kumbukumbu fupi hivi?
Vifurushi vilipanda mwaka Jana mwezi wa 4, baada ya malalamiko mengi mama Samia akaingilia Kati na vikarudi Kama ilivyokuwa.
Mwaka huu ndio vimepanda tena japo sio kama ilivyokua mwaka Jana mwezi wa 4. Huenda Sasa hivi kelele sio nyingi.
Jibu la nape kule twitter ilikua ni haya makampuni yanajiendesha kwa gharama kubwa.
 
Wewe hujielewi aliyesema vifurushi havijapanda ni nani?

Matumizi ya 3G na 4G yanaweza kuwa sawa? Utakuwa una tatizo kichwani.
Soma hiyo reply ya huyo jamaa alafu uone na nilichojibu na ww ulichokujanacho.
Kweye hiyo reply haikuwa inahusu 3G Wala 4G, hiyo reply umesema kuna vifurushi huwa chini kabisa unabonyeza namba zaidi ya unazoona kwenye menu
 
Mimi 1000 nimeuziwa 225MB Jana! Na mtandao huu nilikuwa nauunga Mkono sana!
 
Hapa umekwepa tu ukweli
Halotel miezi michache iliyopita 4G halotel kwa sh 10000 ilikua GB 10. Sasa hivi GB 6.6
Hiyo sijui namba au sijui nenda kwa chini ni uongo.
Kweli Halotel walikuwa wanatuokoa.
Nilikuwa najiunga kifurushi cha 10000 chenye dakika na mbs za kutosha natumia mwezi mzima.
Muda mwingine inabidi niongeze matumizi ili nimalize kifurushi kabla mwezi haujaisha.
Sasa hivi 10000 eti GB 6 mbaya zaidi unweza shangaa umezimaliza hata wiki haijaisha.
 
Kwa vile umedanganya
Lini GB 1ilikuwa 500??
Mie sina shida na mwendazake
Voda - kwenye ya kwako tu. Baadae ikawa 1000 kwa GB 1, baadae ikawa 1000 kwa MB 750, baadae ikawa 1000 kwa mb 550, sasa hivi ni mb 500.
Ila hizo mb 500 zenyewe watahakikisha unazimaliza ndani ya masaa matatu
 
Soma hiyo reply ya huyo jamaa alafu uone na nilichojibu na ww ulichokujanacho.
Kweye hiyo reply haikuwa inahusu 3G Wala 4G, hiyo reply umesema kuna vifurushi huwa chini kabisa unabonyeza namba zaidi ya unazoona kwenye menu
Kwa mfano tigo kwenye size yako tsh 2000 unapata GB 1 na dakika 90 siku 7, ipo namba 9, usidhani naandika hapa kujifurahisha naijuwa vizuri michezo ya kampuni za simu.

Kabla ya kuleta ligi za kijinga jipe muda wa kuzikaguwa menu zote za mtandao unaotumia.

Watu wengi wapo kimazoea akishanunuwa vocha anajiunga alivyozoea wakati hawa wahuni wa kampuni za simu vile vifurushi wanavihamisha hamisha kuwachanganya wateja.
 
Voda - kwenye ya kwako tu. Baadae ikawa 1000 kwa GB 1, baadae ikawa 1000 kwa MB 750, baadae ikawa 1000 kwa mb 550, sasa hivi ni mb 500.
Ila hizo mb 500 zenyewe watahakikisha unazimaliza ndani ya masaa matatu
Kwenye muda wa matumizi mkiambiwa mtumie 3G bado mnashupaza shingo, na bado kuna siku hizo mb zitakwisha ndani ya nusu saa tu.
 
Back
Top Bottom