Intelejensia ya polisi kwenye uunguaji wa masoko ni zero ila kwa vyama vya Upinzani ni 100%

Intelejensia ya polisi kwenye uunguaji wa masoko ni zero ila kwa vyama vya Upinzani ni 100%

Retina

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2015
Posts
1,039
Reaction score
1,163
Police wana uwezo wa kudetect uvunjifu wa amani iwapo vyama vya Upinzani wanataka kuitisha mikutano lakini mikusanyiko ya CCM na kwenye masoko hawawezi.

Miaka ya hivi karibuni masoko yamekuwa yakiungua mara kwa mara mfano Mwanjelwa Mbeya, Kariakoo, Karume n.k, lakini hutakuta wakitoa intejensia yao ya kuashiria hatari fulani inayoweza kutokea au kutoa elimu ya kiusalama maeneo hayo. Utakuta watu wajejazana masokoni, wakijiunganishia umeme wa majenereta bila hata elimu ya usalama.

Mitungi ya gesi inauzwa bila utaratibu maalum, wengine wanaitumia Mitungi kwenye majiko ya kukaangia Chips bila ya tahadhari yeyote n.k.

Polisi wamekariri siasa za Upinzani ndio zinavunja aman na usalama kumbe usalama wa raia ni zaidi ya kudhibiti vyama vya siasa.

Vyuo vya polisi inabidi wafundishwe namna ya kudhibiti na kudetect majanga kama ya Moto kwenye masoko na kutoa elimu kuliko kuelekeza mafunzo yao kudhibiti uhalifu na kudetect uvunjifuwa amani kwa wanasiasa hususan wa upinzani.
 
Police wana uwezo wa kudetect uvunjifu wa amani iwapo vyama vya Upinzani wanataka kuitisha mikutano lakini mikusanyiko ya ccm na kwenye masoko hawawezi...
Usitwgemee kumpata muhalifu kwenye moto wa asili

Pale karume na kariakoo ule moto ni hitilafu za umeme tu ndio mwan mpaka leo haijulikani mchawi nani kwa sababu hakuna mchawi.

Kama hitilafu imeanzia kwenye duka moja huko ndani sokoni,twna usiku na hakuna anayelala hapo,sasa unafanyaje uchunguzi kumjua mchawi ?

Sio kila moto wa mchongo,watanzania tuelewe hili
 
Tatizo Ni Siro ambaye Mungu aliona hafai kuwa Padre akalifukuza. Eti Leo wanadamu mnalipa madaraka makubwa. Laana ya Mungu hawezi kumuacha ndiyo maana ameshindwa kilitawala jeshi la polisi.
 
Police wana uwezo wa kudetect uvunjifu wa amani iwapo vyama vya Upinzani wanataka kuitisha mikutano lakini mikusanyiko ya CCM na kwenye masoko hawawezi...
Kwani tatizo ni elimu au tatizo ni umasikini wa watu? Ukiweka utaratibu wa umeme na gesi utawaongezea gharama za biashara zao hao watu wanaotafuta rizki masokoni. Umasikini huu tulionao tangu tupate uhuru ni chanzo cha matatizo mengi sana.
 
Kwani tatizo ni elimu au tatizo ni umasikini wa watu? Ukiweka utaratibu wa umeme na gesi utawaongezea gharama za biashara zao hao watu wanaotafuta rizki masokoni. Umasikini huu tulionao tangu tupate uhuru ni chanzo cha matatizo mengi sana.
Tatizo ni mfumo wa elimu yetu
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom