Chifunanga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 290
- 100
Utangulizi
Tokea 9/11 vyombo vya usalama wa taifa vimekua vikijihusisha zaidi na masuala ya ulinzi wa mipaka na kutafuta na kuzuia ugaidi. Vyombo
vya usalama vya nchi nyingi vimefanya marekebisho makubwa baada ya ushauri uliotokana na ripoti na utafiti uliofichua mapungufu yaliyo
enda kusababisha mabomu ya August 7 1998 Tanzania na 9/11, kutokana na kukosa intelijensia ya kutosha.
Kumekuwa na mabadiliko hapa kwetu pia, ingawa sio makubwa sana na sio ya wazi kutokana na uhalisi wa kazi. Hata hivyo mambo ya usalama wa taifa yamekuwa yakijitokeza bungeni na inalekea yataendelea kutokea katika siku zijazo.
Intelijensia sio jambo rahisi kulielewa. Ni jambo ambalo lina mambo mengi sana na limezungukwa na mitazamo potofu. Baadhi ya mambo yanaendeleawa chanzo cha mijadala kati wanausalama na wasomi, na mara nyingi ndani ya kila kundi. Ila pia, kama eneo la kujifunza, intelijensia linainua hisiaza kutaka kuifahamu zaidi. Ingawa hisia hizo hupelekea kusisitiza uchama na mambo yakiusalama ya kipindi hicho bila kuweka misingi kwenye mambo ya muhimu zaidiyanayohusu usalama wa taifa.
Kama walivyo watanzania wengi, pia wabunge wengi hawajihusishi na mambo ya intelijensia, au kuusikia uzito unaokuja na majukumu ya intelijensia. Baadhi hufatilia. Kwa wale wanaongilia fani hii kwa mara ya kwanza na kwa wale ambao wamekuwepo kwa muda, thread hii inajaribu kuwapa mwangaza wasomaji kwenye maeneo matatu ya intelijensia: asili ya intelijensia, maelezo kuhusu vipengele vyake, na picha kidogo kwenye jinsi serikali inavyofanya kazi za kiintelijensia. Mambo haya yataelezewa kwa juu juu tu, na mambo kadha wa kadha yanaweza kutajwa tu pale itakapokua muhimu kwenye kutaka uelezea kitu fulani.
Sehemu ya Kwanza: Intelijensia
Neno intelijensia/usalama wa taifa mara nyingi huwa linahusishwa na kuingiza uwoga au kufanya na kuficha uovu. Ukweli ni kwamba intelijensia ni kama kazi zingine kama uhasibu, au marketing. Kikundi au kampuni yoyote ambayo ina ajenda au mtazamo fulani kitatumia intelijensia kuelekeza matokeo, kuzuia vipingamizi na kuushinda upinzani.
Sehemu ya kwanza ya thread hii, tutaangalia intelijensia mtu halafu tutaangalia intelijensia idara. Nia ni kuonyesha kuwa kazi za kiusalama kwenye idara na kikundi fulani ni jnsi nyingine tu ya kujaribu kufanya intelijensia mtu kwenye skeli ya ukubwa zaidi. Halafu tutaelezea matokeo ya intelijensia na mzunguko wa intelijensia. Na mwishowe mtazamo, tathmini na haja ya intelijensia itafuata.
Intelijensia mtu
Kwanza neno intelijensia linatokana na neno intelligence ambalo linaelezwa kama ni uwezo wa kujifunza, kufikiri na kuelewa mambo, aliokuwa nao mtu, na ni mara chache huelezwa kama taarifa au jinsi ya kupata taarifa mara nyingi kwa kazi za kijeshi au kiserikali. Mitazamo hii inaelezea mambo mawili muhimu. Kwanza, intelijensia inahusiana na maamuzi yatakayochukuliwa, na pili kwamba maamuzi hayo yatatokana na utabiri utakaofanya kutoka kwenye taarifa zilizopatikana.
****ngoja nikale kwanza.....nitarudi muda si mrefu*****....HAYA NIMERUDI
Intelijensia idara
Kwamba intelijensia mtu kwa upana wake ndio unaunda intelijensia idara sio jambo la ajabu. Intelijensia ni jambo la kawaida kwa mtu, na idara zinaundwa na watu. Hii maana yake sehemu ya Intelijensia ndani ya serikali ni muendelezo tu wa kujaribu kutengeneza intelijensia mtu kwa upana zaidi.
[imebidi nifanye marekebisho kwenye paragraph hii kwa kushindwa kuweka mambo fulani fulani, mwenye macho na asome]. Idara nyingi za usalama barani afrika, hasa kwa nchi zilizotawaliwa na wazungu, ingawa idara hizo zilianzishwa au kubadilishwa chini ya uongozi uliokuwepo wakati nchi hizo zinapata uhuru, bado mpangilio wake kwa kiasi fulani unafuata mfumo wa Idara mbadala za uingereza. Hivi karibuni wamarekani pia wameweza kuingiza mambo yao kwenye ku'influence' utendaji kazi wa idara hizo. Kwa mfumo wa kiingereza, intelijensia na ukusanyaji wa taarifa ni kitu kimoja. Wataalamu wa intelijensia wa uingereza wanasema kuwa intelijensia inatafsiri na ni sehemu ya kawaida kabisa katika kufanya maamuzi fulani. Wamarekani wao, wanaona intelijensia ni zaidi ya taarifa, kwamba intelijensia ni sawa na taarifa pamoja na tafsiri ya taarifa hizo. Wamarekani wanasema kuwa intelijensia sio tu kupata taarifa na kuzitafsiri kwa nia ya kutolea maamuzi, bali pia ni njia nyingine ya kuelekeza matendo fulani fulani. Wamarekani wanadhani kuwa kazi ya intelijensia sio kutafuta ukweli, bali ni kusaidia kutafanya maamuzi ambayo yataleta mafanikio ya kuukandamiza au kuufuta upinzani.
Sehemu za intelijensia
Watu, Idara, Maamuzi, na Matokeo ndio sehemu ambazo intelijensia inafanya nazo kazi. Intelijensia inaanza na kupata taarifa au data, baada ya hapo taarifa hizo zinahakikiwa nakutafsiriwa, baada ya kutafsiriwa zinakuwa elimu. Elimu hiyo inatakiwa kueleweka na kutolewa maamuzi, elimu hiyo pia inabidi iweze kuotea jambo litakalotokea baadae.
Kama taarifa nyingi zitaletwa kuhusiana na jambo fulani, zikiwekwa pamoja zinaanza kuonyesha jambo ambalo linatokea au linataka kutokea. Na wingi wa taarifa unavyozidi kuongezeka kunapelekea kuwa na elimu kuhusu jambo hilo. Elimu ya kutosha ikishapatikana, jambo hilo litaanza kueleweka na kupelekea kulitolea maamuzi. Uwezo wa kulielewa jambo linalotokea huwa linahusu muda huu, na linaweza kubadilika kwenye muda mwingine mbeleni.
*********naenda kuangalia ze komedi......nitarudi badae au kesho mungu akipenda ***********