Bahati mbaya sana kuna watu immature wasio na hekima, wanataka kuaminishwa watu hivyo kwa kauli zao. Na kwa namna hiyo hiyo ni makosa kuanza kuwanyooshea vidole nchi jirani au watu fulani bila kuwa na ushahidi dhairi. Kinachochangia hizi speculation ni udhaifu wa vyombo vyetu vya usalama kwa kutofanya uchunguzi haraka na kutoa taarifa kwa umma.mwanzo nilikua nadhani mabomu yale ni siasa au dini. Kwa sasa nimeamini si chadema si ccm si wa kristo wala si waislamu wanaohusika na mabomu haya. Ni njama za jirani zetu. Jiulizeni kwa nini mabomu hayalipuki Sumbawanga au Songea? Ni Zanzbar na Arusha tu!
Sidhani kama ni sahihi kusema CCM wanajua. Kauli hii ina maana secretariat, Kamati kuu au halmashauri ya taifa wajumbe wake wote pamoja au kikundi chao wanahusika. Haiwezekani kuwepo kitu kama hicho. Halikadhalika si sahihi kwa wale wanaofikiria ni vyama vya upinzani. Bali ninafikiria ni kikundi au watu fulani ambao wana malengo mabaya wanafanya haya kwa kutumia udhaifu uliopo.Wakenya washindwe kwao waweze tz? Basi adui wa Tz na kenya ni mmoja. kwa sababu, kenya wanashambuliwa na alshababu ili wayatoe majeshi yao Somalia. Lakini nani alianza kumshambulia mwenzake? Ni alshababu ndipo kenya ikapeleka majeshi somalia kuwasaka alshababu.
Aidha, ni nchi nyingi zenye vikosi vyao huko somalia.mfano,Djibout, Ethiopia, Uganda na Burundi mbona huko kwao hakuna harakati za alshababu? Kama hoja itakuwa ni ufikivu, Ethiopia pia imeunga mpaka na Somalia.
Kama ni ushindani wa kibiashara, Kenya yawapasa washindane si kwenye utalii pekee bali na kwenye gesi, mafuta, ukubwa wa ardhi ya tz, jina la tz kujiuza lenyewe. Hulka ya watz kupenda na kuenzi amani.Jeshi la tz limetukuka duniani(syschelis,Comoro,Mozambique,Uganda,DRC,Darfur,Lebanon)
Milipuko ya tz CCM wanaijua vilivyo chanzo,sababu na mikakati yake. Viweje polisi watumie masaa 24 kuwanasa wauaji wa faru jacq; watumie masaa 24 kuwakamata wauaji wa mama wa kichina; watumie wiki kuwatia mbaroni wauaji na waporaji kituo cha polisi kimanzichana LAKINI polisi hao hao tena wakishirikisha FBI washindwe kuwakamata wauaji wa padri, walipua mabomu Soweto?...!!!
Upeo duni kabisa na fikra hafifu......hivi unaposema kenya wanahusika na mabomu unamaanisha kenya kama kenya nchi ndio imeleta watu kulipua mabomu. Au unamaanisha wakenya yaani wafanyabiashara binafsi wameamua kupiga mabomu? ............hebu jaribu kufikiria zaidi hivi serikali ya kenya inaweza kutuma mtu au kutuma usalama wao kurusha vibomu na bodaboda......wa tz tuache kujitia aibu na mawazo duni
Vyombo husika watalisimamia hili kwa nguvu zote.
mwanzo nilikua nadhani mabomu
yale ni siasa au dini. Kwa sasa nimeamini si chadema si ccm si wa
kristo wala si waislamu wanaohusika na mabomu haya. Ni njama za jirani
zetu. Jiulizeni kwa nini mabomu hayalipuki Sumbawanga au Songea? Ni
Zanzbar na Arusha tu!
Mkuu wangu nimekuuliza kama wanao choma makanisa,biashara za Watanganyika na kuua Mapadri huko Zanzibar ni Wakenya bado hujajibu!! Bado nakuuliza nakuuliza hao ni Wakenya?Wakenya wanaumia kuwa Tanzania inainuka kwa kasi. Mabomu haya yote ni yao, Arusha vs Nairobi, and Zanzibar vs Malindi in tourism.
Kenya is our TOP ENEMY!
Tatizo la mabomu halihusiani na udhaifu wa serikali, kwani mabomu yanalipuliwa hata Marekani, Uingereza na kwingineko ambako usalama ni imara, usipotoshe hoja ya mtoa madaHivi ni kwanini tu wepesi wa kupeleka vidole kwa nchi nyingine? Je, usalama si suaka la serikali kulifanyia kazi? Serikali dhaifu imefanya hata utendaji wa taasisi nyeti kuwa dhaifu na kutowajibika. Muda mwingi vyomba vyetu vya usalama vipo busy na wapinzani, sijui lini hawa viongozi wetu wataamka toka usingizi huu wa uzembe na ujinga.
Unashindwa kuelewe kitu gani kujua mahusiano ya Arusha na Vivutio vya Utalii kama Serengeti,Ngorongoro,Kilimanjaro,nk? Hii elimu duni inasababisha watu wavivu kufikiri.