MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni imeshindwa kusikiliza kesi ya madai inayomkabili ,Mtangazi wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC1) Bw. Jerry Muro kwakuwa mdaiwa huyo ameshindwa kuwasilisha vielelezo vya maombi ya kurudia kesi hiyo.
Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa, hapo awali mdaiwa huyo aliiomba Mahakama kurudia upya kesi hiyo kwa kuwa yeye hajawahi kuudhuria katika shauri hilo.
Hakimu Sundi Fimbo aliyesoma shauri hilo alimwambia mdaiwa kuwa kama anaitaji kesi irudiwe upya inabidi alete vielelezo vya maombi ili shauri hilo lilidiwe upya.
Hapo awali ilidaiwa kuwa Desemba 26 mwaka 2008 mdaiwa alikwenda katika Kampuni ya Boneste General Enterprise Ltd kwa ajili ya kukopa pesa talimu sh milioni 1.5 kwa ajili ya kwenda kugomboa gari lake bandarini.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa kampuni hiyo ilimpa sharti la kurudisha pesa hizo kwa siku 60, lakini mshitakiwa alilipa sh. milioni moja badala ya milioni 1.5 .
Hata hivyo Mahakama hiyo ilisema kuwa mshitakiwa anadaiwa sh. milioni 15 ambayo ni pamoja na fidia ya kukaa na pesa kwa muda mrefu.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka Julai 9 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa upya.