International airport ndani ya Serengeti ni makosa makubwa kiuhifadhi

Serikali unajua dhahiri kuwa na kiwanja cha kimataifa ndani ya hifadhi ya Serengeti ni makosa makubwa na madhara yake ni makubwa kuliko faida ila kwa wachache wanangalia faida za kifedha na kupuuza madhara makubwa ya kimazingira na hapa ndo tunapofeli.
Wakati mwingine hao watawala hufanya mambo yanayoonekana kama hujuma.
Sidhani kama hawajui hayo madhara.

Ukute kuna wageni fulani wanapata shida kusafirisha wanyama hai kupitia KiA, nk, maana inashindika kuwa siri, wamekuja na huu mchongo hatari na serikali "sikivu" imeridhia..
 
Eneo kutakakojengwa uwanja wa ndege si ndani ya mbuga ya wanyama ya Serengeti. Niko jirani na eneo husika(uwanja wa ndege) na liko mbali na mbuga ya wanyama
 
Serikali unajua dhahiri kuwa na kiwanja cha kimataifa ndani ya hifadhi ya Serengeti ni makosa makubwa na madhara yake ni makubwa kuliko faida ila kwa wachache wanangalia faida za kifedha na kupuuza madhara makubwa ya kimazingira na hapa ndo tunapofeli.

Kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kunaweza kuleta madhara makubwa kwa mazingira na wanyamapori. Baadhi ya madhara hayo ni:

Kuharibu Mazingira Asilia – Ujenzi wa kiwanja cha ndege utahitaji ukataji wa miti, ujenzi wa barabara, na miundombinu mingine, jambo ambalo linaweza kuharibu makazi ya wanyama na kusababisha mmomonyoko wa udongo.

Kuvuruga Mfumo wa Ikolojia – Serengeti ni mojawapo ya maeneo yenye mifumo ya kipekee ya ikolojia duniani. Shughuli za ujenzi na uendeshaji wa kiwanja cha ndege zinaweza kuvuruga uhamaji wa wanyama (kama nyumbu na pundamilia) na mzunguko wa maisha yao.

Kelele na Uchafuzi wa Hewa – Ndege zinazotua na kupaa zitazalisha kelele kubwa, ambazo zinaweza kuwasumbua wanyama na kuwafanya waondoke kwenye maeneo yao ya asili. Pia, moshi na hewa chafu zitakazotoka kwa ndege na magari zinaweza kuharibu ubora wa hewa na mimea.

Kuongezeka kwa Watalii Kupita Kiasi – Wakati utalii ni chanzo muhimu cha mapato kwa Tanzania, idadi kubwa ya watalii inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira na ongezeko la taka, magari, na ujenzi holela wa hoteli na miundombinu mingine.

Hatari kwa Ndege za Abiria – Hifadhi ya Serengeti ina idadi kubwa ya ndege wa porini, ambao wanaweza kugongana na ndege za abiria (bird strikes), jambo ambalo linaweza kusababisha ajali mbaya.

Kuharibu Utalii wa Ikolojia – Serengeti ni kivutio cha kimataifa kutokana na mandhari yake ya asili na wanyama wake wa porini. Ujenzi wa kiwanja cha ndege unaweza kuharibu uhalisia wa hifadhi na kuifanya ionekane kama jiji badala ya eneo la porini.

Kwa ujumla, madhara ya kujenga kiwanja cha ndege ndani ya Serengeti yanaweza kuwa makubwa zaidi kuliko faida zake. Njia mbadala inaweza kuwa kuboresha viwanja vya ndege vilivyopo nje ya hifadhi, kama vile Kiwanja cha Ndege cha Arusha au Mwanza, na kuimarisha usafiri wa ndani kwa kutumia viwanja vidogo vilivyo karibu na Serengeti.

mambo yanayofanyika sasa ni sawa na mlevi kuficha kiwiliwili kichakani na kuacha makalio wazi yakiwa kando ya barabara, alaf eneo lenyewe ni mombasa!!
 
Aisee sijui wamewaza nini ila kwa yanayoendelea wacha tuwe wasikilizaji tu ni Nchi gani wameona kiwanja cha ndege kikubwa kimejengwa Mbugani wao badala ya kupunguza gharama za kutua hapo KIA wanataka kuififisha KIA na Daslm ili wafanye mambo zao huko...
Pana vitu vinatokea Tanzania na hauwezi kuamini kama ni watu wenye fikra zao wameanua kufanya hivyo...
" Pana vitu vinatokea Tanzania na hauwezi kuamini kama ni watu wenye fikra zao wameanua kufanya hivyo " mkuu hii inasikitisha sana
 
Wakati mwingine hao watawala hufanya mambo yanayoonekana kama hujuma.
Sidhani kama hawajui hayo madhara.

Ukute kuna wageni fulani wanapata shida kusafirisha wanyama hai kupitia KiA, nk, maana inashindika kuwa siri, wamekuja na huu mchongo hatari na serikali "sikivu" imeridhia..
umeongea ukweli kabisa!!!
 
KIA iko mbali sana na Serengeti na tunakoelekea kama Serengeti itapata International Airport na hapo jirani tu Mwanza kunapanuliwa kuwa International Airport tegemea Watalii wa kuja Serengeti kushukia Serengeti au Mwanza! KIA itabaki kuhudumia watu wa Northern circuit hasa wa kutembelea Kilimanjaro na Ngorongoro!
MADHARA YA KWENYE MBUGA HUJASEMA...
Unaweza kuwa na kiwanja baada ya muda madhara yatakuwaje..
 
" Pana vitu vinatokea Tanzania na hauwezi kuamini kama ni watu wenye fikra zao wameanua kufanya hivyo " mkuu hii inasikitisha sana
Wanatangaza kuwa Utalii unaipatia Nchi pesa nyingi hapo hapo wanavuruga utalii hawalindi kitu baadae utasikia wanatoa vibali vya kuchimba madini mbugani hawa jamaa sio watu kabisaa.
 
Lengo hapa mambo yao yaishie humo humo mbungani, hatari sana basi tu
 
kiwanja kitajengwa mjini mgumu kilomita zaidi ya 50 toka kwenye hifadhi ya serengeti huo uharibifu wa uoto wa asili hautakuwepo.
Hao wana chuki na mkoa wa Mara,, mkoa wa Mara pia unahitaji kufunguliwa kumbuka ndo muasisi wa Taifa hili alipozaliwa
 
Sasa ccm inaweza kumpa makamu na mkuu wa vijana ccm huyu.we unazani akili zinafanya kazi
IMG_0612.jpeg
 
Serikali unajua dhahiri kuwa na kiwanja cha kimataifa ndani ya hifadhi ya Serengeti ni makosa makubwa na madhara yake ni makubwa kuliko faida ila kwa wachache wanangalia faida za kifedha na kupuuza madhara makubwa ya kimazingira na hapa ndo tunapofeli.

Kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kunaweza kuleta madhara makubwa kwa mazingira na wanyamapori. Baadhi ya madhara hayo ni:

Kuharibu Mazingira Asilia – Ujenzi wa kiwanja cha ndege utahitaji ukataji wa miti, ujenzi wa barabara, na miundombinu mingine, jambo ambalo linaweza kuharibu makazi ya wanyama na kusababisha mmomonyoko wa udongo.

Kuvuruga Mfumo wa Ikolojia – Serengeti ni mojawapo ya maeneo yenye mifumo ya kipekee ya ikolojia duniani. Shughuli za ujenzi na uendeshaji wa kiwanja cha ndege zinaweza kuvuruga uhamaji wa wanyama (kama nyumbu na pundamilia) na mzunguko wa maisha yao.

Kelele na Uchafuzi wa Hewa – Ndege zinazotua na kupaa zitazalisha kelele kubwa, ambazo zinaweza kuwasumbua wanyama na kuwafanya waondoke kwenye maeneo yao ya asili. Pia, moshi na hewa chafu zitakazotoka kwa ndege na magari zinaweza kuharibu ubora wa hewa na mimea.

Kuongezeka kwa Watalii Kupita Kiasi – Wakati utalii ni chanzo muhimu cha mapato kwa Tanzania, idadi kubwa ya watalii inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira na ongezeko la taka, magari, na ujenzi holela wa hoteli na miundombinu mingine.

Hatari kwa Ndege za Abiria – Hifadhi ya Serengeti ina idadi kubwa ya ndege wa porini, ambao wanaweza kugongana na ndege za abiria (bird strikes), jambo ambalo linaweza kusababisha ajali mbaya.

Kuharibu Utalii wa Ikolojia – Serengeti ni kivutio cha kimataifa kutokana na mandhari yake ya asili na wanyama wake wa porini. Ujenzi wa kiwanja cha ndege unaweza kuharibu uhalisia wa hifadhi na kuifanya ionekane kama jiji badala ya eneo la porini.

Kwa ujumla, madhara ya kujenga kiwanja cha ndege ndani ya Serengeti yanaweza kuwa makubwa zaidi kuliko faida zake. Njia mbadala inaweza kuwa kuboresha viwanja vya ndege vilivyopo nje ya hifadhi, kama vile Kiwanja cha Ndege cha Arusha au Mwanza, na kuimarisha usafiri wa ndani kwa kutumia viwanja vidogo vilivyo karibu na Serengeti.

Actualy according to taratibu za uhifadhi huiruhusiw kujengwa international airport. International airport unaongelea akina KIA na JKIA airports, zinafuatia regional airports.

Zinazokuwamo ndani ya mbuga ni airstrips ambazo kimsingi si internationa wala hazijafikia hadhi ya regional airports
 
Wanawaza kuvuna pesa tu hawawazi wanaharibu chanzo cha kuvunia pesa
Akili zao ni kama yule bwana alikuwa na bata anayetaga yai la dhahabu kila siku, akaona ili asichelewe avune dhahabu yote akamchinja yule bata apekue tumboni na kutoa dhahabu yote.

Alipompasua yule bata hakupata dhahabu yoyote tumboni, bata akafa na hata ile dhahabu kidogo kupitia mayai nayo ikaota mbawa.

Ecology ya Serengeti ikiharibika kwa huo upuuzi wanaotaka kufanya, na hizo senti za utalii nazo zitayeyuka na airport itakosa kazi ya kufanya.
 
kiwanja kitajengwa mjini mgumu kilomita zaidi ya 50 toka kwenye hifadhi ya serengeti huo uharibifu wa uoto wa asili hautakuwepo.
Kwaninpale Mgumu ndio paharibiwe? Duh!
 
Kwakweli kuna mambo yanatakiwa yajadiliwe kitaalamu na kuweka wazi ili maoni yachukuliwe kwa uzito, lakini tukiacha maamuzi yafanyike mahala flani na watu flani tu basi tutabakia na historia tu kama ya majengo ya pale Salamander
 
Back
Top Bottom