International Friendly Match, Taifa Stars Vs Malawi The Flames | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Leo Jumapili Juni 13, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa kutakuwa na mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wakiumana vilivyo na Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames).

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:0 Jioni. Usikose Ukasimuliwa.​



========

10' mchezo umeanza kwa kasi huku mashambulizi yakiendelea kusaka bao kwa pande zote mbili.

Yusuf Mhilu anapiga shutiiiiii loooooo, anakosa nafasi nzuri ya kufunga ambapo shutiiiiii lake linapaa nje ya lango.

22' Mchezaji namba 10 wa Malawi anapiga shutiiiiii linatoka nje.. Ilikuwa nafasi kuandika bao | Taifa Stars 0-0 The Flames.

30' Hakuna timu imeona lango la mwenzake huku mashambulizi yakiendelea.

Almanusura The Flames wajipatie bao, kama si umahiri wa golikipa Manula kuokoa mchomo mkali kutoka kwa mshambuliaji wa The Flames.

Taifa Stars wakimiliki sasa kwake Mhiluuu, wanaokoa mabeki wa The Flames

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Mkapa. Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Timu zinatoka bila kufungana | Taifa Stars 0-0 The Flames.

Kipindi cha pili kimeanza huku Taifa Stars wakifanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwa mkupuo.

65' Shuti kali la Ayoub Lyanga linapanguliwa na golikipa wa Malawi na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda | Taifa Stars 0-0 The Flames

68' Goooooooooaaal Goooooooaaal
John Bocco anahesabu bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Kibu | Taifa Stars 1-0 The Flames

Mpira ni Free Kick kuelekea Malawi The Flames.

Goooooooooaaal Goooooooaaal Israel Patrick anahesabu bao la pili kwa mpira wa Free Kick | Taifa Stars 2-0 The Flames.

85' The Flames wapo nyuma kwa mabao mawili huku wakifanya kila mbinu kuweza kusawazisha au kujipatia bao la kufutia machozi.

90+3' kuelekea kumalizika kwa mchezo, huku matumaini ya kusawazisha yakitoweka upande wa The Flames.

Naaaam umekwishaaa ambapo Taifa Stars wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya The Flames| FT: Taifa Stars 2-0 Malawi.

Ghazwat..!
 
10' Mchezo ni mkali Wanaume hawa wanapambana huku Taifa Stars wakimiliki zaidi kuliko The Flames

Taifa Stars wamepoteza nafasi nzuri ya kufunga, ambapo shutiiiiii kali la Mhilu likipaa juu ya lango

Taifa Stars 0-0 Malawi
 
Nyoni ukija kwa mbwembwe anakutukiza...!
 
45+2' Mpira ni mapumziko ambapo hakuna timu imeweza kusalimia lango la mwenzake | Taifa Stars 0-0 The Flames.
 
68' Bocco Goooooooooooooaaal Goooooooooaaal

John Bocco anahesabu bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Kibu

Taifa Stars 1-0 The Flames
 
Patrick Mwenda anaipatia Tanzania goli la pili.

Kumbe hakuna haja ya kina Samata. Maingizo mapya yanaweza kufanya kitu
 
75' Goooooooooaaal Goooooooaaal
Patrick anahesabu bao la pili kwa mpira wa Free Kick

Taifa Stars 2-0 The Flames
 
Hivi mpaka sasa john boko ana jumla ya magoli mangapi- michezo yote?
 
Huyu bwana mdogo Peter Banda imebidi nim google aisee..dogo anacheza Moldova huko europe katika timu ya sheriff tiraspol..no wonder anaujua sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…