Naona hapo mnapewa bundle za juu lakini lakini ziko capped at maximum bandwidth unaweza kutumia kwa mwezi, hata iwe speed gani, ukimaliza hio 50GB na siku moja huwezi tumia internet hadi unune tena... Tofauti na hio safaricom home fiber ukipewa bandwidth ya 20Mbps unapewa unlimited bundle Yani Una download vitu vya 1TB baada ya wiki moja na bado unaruhusiwa kuendelea kutumia....
Mi nishajiandikisha nataka Fiber Kwa nyumba, Friday walikua kwa nyumba kupima na wamesema Monday saa nne niwe Kwa nyumba niwekewe kitu! nitakuonyesha speed yangu hapo Kesho Mungu akipenda, lakini mbali na hilo nitakua na download unlimited! Yani hata nitakua si zimi computer, nitakua naiwacha iki download siku nzima, naona baada ya wiki moja ntakua sina cha kudownload tena , nitabaki ni ki stream Netflix na YouTube nikingojea new content.