Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa wewe mdogo kuna kitu kinaitwa MVNO, mobile virtual network operator,Nikitaka niweze Ku provide fiber niwe internet provider Kwa kijiji kidogo mfano nyumba 200..
Natakiwa nifanyeje..?
Nianzie wapi?
Kwa wewe mdogo kuna kitu kinaitwa MVNO, mobile virtual network operator,
Hapa unakua unanunua data kwa bulk toka kwa Isp na kuuza kwa vifurushi vyako. Mfano wa MVNO ni uhuru one, walikuwepo sana Kkoo hawa walikuwa wakinunua Toka Tigo, Hivyo Angalia eneo lako kama kuna Supplier yoyote wa maana kama TTCL anaweza kukuuzia kwa Jumla.
Tatizo hio keyword kijiji,Ni lazima ninunue kutoka makampuni ya simu?
Siwezi kuwa internet provider bila kushirikiana na kampuni za simu
Pale UCC udsm wanatoa wapi internet yao?
Tatizo hio keyword kijiji,
Waya asili zake ni baharini tena kwenye majiji makubwa, mtu kutandaza nyaya mpaka kijijini ni gharama sana, kampuni nyingi za fiber tupu hata mwananyamala hapo huzikuti, hivyo kijijini ngumu kufika unless ni haya makampuni makubwa ya simu.
Tusubiri starlink mkuu maananimeona internet yao tamu sana speed ya kutosha na huhitaji hata mtaalamu kuifunga satelite dish inajigeuza yenyewe ikishanasa satelite kwisha habariHakuna technology ya kupata internet Kwa satellite mfano halafu wewe ndo ukasambaza Kwa fiber?
Satelite zinakuwa na ping kubwa na ni ghali sana, hata ukitumia fiber haitasaidia. Ila inawezekana.Hakuna technology ya kupata internet Kwa satellite mfano halafu wewe ndo ukasambaza Kwa fiber?
Hii ni internet ya satelite inatolewa na kampuni ya Elon Musk ambapo imelenga zaidi watu walioko kwenye remote areas. Package ya vfaa nadhan dollar 700 na nadhani unakuwa unalipia 100$ kila mwezi ilivyo na speed nadhani ukinunua kadhaa unaweza kuwasambazia watuNipe elimu zaidi please
UCC si wapo mjini? Mjini zipo fiber za kutosha, zuku, raha, Home faiba, TTCL etc. Sijui wao wanatumia nini ila kwa mjini si tabu.Nilitoa mfano wa UCC
Unaweza nieleza internet Yao ikoje??