Nijuavyo mimi hakuna sheria ya moja kwa moja inayokutaka uende TCRA ili upewe kibali cha kufungua Internet TV au Internet Radio kwani hizo utaziendesha kwa kutumia website ambayo mipaka yake ni zaidi ya Tanzania. Unapofungua website auhitaji kibali toka TCRA, au hata unapostream kitu kwenye internet auhitaji hicho kibali. Ila kwa kuwa kuna sheria ya makosa ya mtandao ambayo nayo sidhani kama imezungumzia chochote SPECIFICALLY kuhusu internet Radio na internet TV, nakushauri si vibaya ukapata ushauri kutoka TCRA, ila sidhani kama kwa utaratibu wa sasa kuna kibali maalum kutoka kwao. Unaweza kuanzisha bila kibali chao ila kama iivyo kwa blogs na website zote zingatia sheria iiyopo kwa vile utakavyokuwa unavirusha. I stand to be corrected!