Interpol wanasa bilionea mwingine Arusha


Nadhani Kikwete na serikali yake wanatafuta pa kuanzia kwa Lowasa na Chenge kwa mtindo huo baada ya kuona PCCB na Polisi wa ndani ni watu wake na wanakosa weledi wa kadi
Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi fulani lakini kama lengo lao ndilo hilo nawapa angalizo, wakati unamulika nyoka kwenye nyumba ya nyasi kwa kutumia ukuni wa moto hakikisha mlango uko wazi.
 
Kufuatia kukamatwa kwa Wakili na Mfadhili maarufu wa chama kimoja cha siasa huko Arusha, ebu wana JF tujadili kama haya macho ya Intepol nayo hayataona ya EL, RA na AC? Je wao pia watakuwa kama PCCB juu ya Account na mienendo ya hawa tycoons wa Ufisadi Tanzania? au ndio Kikwete kafungua Mlango na kuwapigia kengere ya mwisho kabla ya kujipima wao wenyewe? Lakini kama hii itakuwa ndio kengere ya mwisho kuwa mwenye masikio na asikie vipi hawata weza kuona yanayosemwa juu ya Ridhiwani?

Tuchangie kwa umakini huku tukisubiri picha kuanza rasmi maana sidhani kama Intepol watakubali kushusha heshima yao kama PCCB na Polisi ya Tanzania walivyojishusha na kupoteza heshima yao machoni mwa Watanzania.
 
AM ni mmoja ya wafadhili wakubwa wa CCM, katika uchaguzi wa 2005 alipewa jukumu la kuwanunua wapinzani, moja wapo ya watu aliowanunua ni Thomas Ngawaiya. Huyu ni jeuri si mnakumbuka wakati wa kesi yake moja pale Kisutu alivyokuwa anajiachia kwa raha zake akiongea na simu mahakamani kama yuko sebuleni kwake.

Kama alivyosema mdau mmoja hapa hii inaweza ikaishia kujadiliwa tu hapa jamvini lakini hakuna kitakachoendelea ,hawa ndiyo watawala wenyewe.
 
ah..alijisemeaga namhala wa vijisenti..kila mtu na kiwango chake! yaani 20M kwa matumizi madogo madogo....wakati akina siye bukujelo ndiyo ya matumizi madogomadogo! bongo bila ujanja wa mujinimujini maumivu tupu!
 
wanataka kugawana naye tu hizo pesa, wamefikiria kwa nini awe nazo peke yake ! na ukifuatilia utakuta wala hajamwibia mtu, marehemu kaka yake alikwisha zitafuta hizo . . . . kabla hajafa.
 
inawezekana ni halali kwani hakumkaba mtu na yeye hayuko serikalini hivyo hakuna hela za walipa kodi, ukiwafatilia sana mawakili kweli wana hela za kutisha , mbona huyu tu Mkono mbona hammtaji kwa dhuluma na mikataba feki, je mkifatilia hela alizonazo zinalingana na kazi? acha uonevu.
 
Tuseme imefikia hatua hadi JK hawaamini polisi wake mwenyewe?
 
Ikiwa hivyo hata yeye JK hataweza kupona make ni lazima akina EL na EC watataka kurevenge
 
Ikiwa hivyo hata yeye JK hataweza kupona make ni lazima akina EL na EC watataka kurevenge

Hapo hapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliposema ikulu ni mzigo moja ya sababu ni kama unavyohisi wewe.
 
Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi fulani lakini kama lengo lao ndilo hilo nawapa angalizo, wakati unamulika nyoka kwenye nyumba ya nyasi kwa kutumia ukuni wa moto hakikisha mlango uko wazi.

nimeipenda hiyo!
 
Ina maana hapo kwetu hawa Usalama wa Taifa wanafanya kazi gani mpaka wameshindwa kumkamata huyu Wakili mwenye Mabilionea shilingi? Mpaka anakuja kukamatwa huyu Wakili na hao Polisi wa Kimataifa Interpol? Nchi yetu kweli haina Viongozi wanaopenda Nchi yao. wizi Mtupu Nchi yetu inaongozwa na Viongozi Mafisadi tu.
 
Tupeni jina kwani mtuhumiwa hatajwi jina amekuwa juvenile au under 18?
 
Mkubwa wa Interpol Tanzania ni IGP Mwema, na ndio ilikuwa kazi yake kabla ya kupewa uIGP.

Sidhani kama maelezo yako yana ukweli wo wote. Saidi Mwema alipokuwa Interpol alikuwa Nairobi na ndiyo akawacha hiyo nafasi na kuja kuchukuwa nafasi ya IGP.
 
Si munakumbuka tulipitisha ile sheria ya kuzuia money laundering? Tatizo la huyu kijana ni kwamba fedha hii US$ million 30 imeingia kwa mkupuo mmoja na bila ya maelezo ya kuridhisha ndiyo ikashtua jamaa wa Interpol. Akina Mkono wao huwa inaingia pole pole na kwa approval ya BoT.

Na hiyo jeuri ya kuwa na vijisenti vya Million 20 kama chenji ya wikiendi siyo mchezo. Arusha kumbe noma!
 
Dah, tumeshindwa kuwakamatwa cc wenyewe sana wageni ndo wanawakamata, haya huu ni mwanzo tu!
 
Kwani kaiba. Si za kwake mwenyewe, kwani hamjui kama kazi ya uwakili ina hela. Mbona hamumjadili Mh. Nimrod Mkono? Wacheni uchoyo wa nafsi.
 
bwana mashalla maneno yako yako hata nyuma ya kanga kwa kua hayana maana na ndio maana hua yanakaa nyuma ya kanga, usitumie peni yako kama silaha ya kueneza umbea, ni vyema ukafuata weledi na taaaluma yako inakutaka ufanye nini kabla ya kuandika habari, unajua tatizo letu sisi wabongo umbea mwingwi, kuna mtu aliyewahi kulalamika ya kua ameibiwa billion 30 ? Hao polisi wa interpoll wanaomchunguza jamaa wewe uliwahoji? Walikuambia wameajiriwa na interpoll? Unafiki bwana........
 
Woooooooooooteeeeeeeeeeee watahongwa halafu baadae kimyaaaa kitatawala..............................................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…