JamiiForums imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kusambaza kwa habari hapa nchini na Afrika Mashariki, acha maeneo mbalimbali ya Dunia. Tukitolea mfano wa habari ambazo zimekuwa zikitambuliwa zimetoka katika chombo hiki cha JF kama vile ilivowahi tangazwa na BBC kutumia JF kama chanzo. Na pia kutajwa mara kadhaa na viongozi wa ngazi za juu hadi kwenye Bunge letu tukufu la Tanzania; kwa msimu huu imetajwa sio chini ya mara 3.
Naam,
A]. U/mmejipanga vipi kuhimili kukua kwa kasi kwa JF ili kuweza enda sambamba na mabadiliko hayo?
Kama nilivyofafanua awali; mipango mkakati ya muda mfupi na ya muda mrefu itaweza kutatua hili.
B]. U/mmejipanga vipi kuhimili matakwa ya baadhi ya viongozi kutaka JamiiForums ifungwe kwa madai kuwa haifai na inaleta uchochezi?
Wana haki ya kupendekeza vyovyote, ndiyo demokrasia.
Sidhani kuna uchochezi uliofanywa ndani ya JF, hapana. Ni wengine kuguswa na watumiaji wa JF na huenda wahariri wetu wakawa hawajaona kilichoandikwa na kikawakera wahusika. Kuongeza idadi ya wahariri, wahusika kuwasiliana nasi haraka pindi wanapoona kitu kisicho sahihi au kisicho cha kawaida kunaweza kupungua kwa malalamiko haya. Hatufurahishwi na watu kuchafuana ama kuchochea vurugu za namna yoyote.
Hata hivyo; kufungia tovuti si suluhisho la matatizo! Bahati ni kuwa waendeshaji wa JF wapo Tanzania, wakipewa ushirikiano mambo mengi yanaweza kukaa sawa. Kwanini wanaolalamika na kutaka ifungwe wasilalamike kuwa iwezeshwe iweze kuboresha utoaji wa huduma? Mara zote, hata kama una mazuri kiasi gani, baya moja humfumba macho mwanadamu.
JamiiForums si siasa tu. Kuna majukwaa kama
JF Doctor ambapo watumiaji wengi wamenufaika na kupata msaada kwa matatizo yao ya kiafya; kuna forum ya
Great Thinkers (hawa ndio naweza kuwaita nguli wa JF) ambapo watumiaji wa forum hii hawajadili propaganda bali kujadili 'issues'. Kuna
Forum ya Sheria ambapo wadau wengi hupata kujadili mambo mengi yanayohusiana na sheria, na nyingine nyingi!
C]. Nini kinachokuongoza kuweza kusimamia chombo hiki kwa haki bila upendeleo na unafikiri una misingi inayoweza kufanya team yako yote isimame pale unapoamini bila kuyumbisha lengo na msimamo wa JF?
Tuna mwongozo wa utendaji kwa wahariri, mwongozo huu unasomwa na wahariri wetu wote. Hata hivyo, kuna namna ambayo mhariri yeyote anaangaliwa kila kitendo anachofanya. Iwe ni kumfungia mtu, kuhamisha hoja au kuifuta hoja. Tunafanya hivyo ili kuweza kuhakikisha kila kitu kinaenda tunavyotarajia.
D]. Kuna mpango gani wa kuvihusisha vyombo vingine vya habari hasa Radio na TV kwa vipindi vya mahojiano mahususi kama vile anavyofanya ndugu yangu Yahya Mohamed pale Star TV Mwanza?
Kwanza niwapongeze vyombo vya Habari kama Star TV na Magic FM walioamua kuwapa ushirikiano wana JF kuhakikisha hoja zao zinaenda nje ya mtandao. Huu ni mwanzo mzuri, ndugu Yahya Mohamed wa Star Tv ni mwandishi wa kwanza Tanzania kuitumia JF kuweza kukusanya maoni na kuyafikisha nje ya mtandao akifuatiwa na dada Fina Mango (kupitia Magic FM kila Jumamosi); kwa hili kwa niaba ya JF, niwapongeze na kuwatia moyo kuwa tutahakikisha tunaboresha kadiri siku zinavyokwenda.
Hata hivyo, kama nilivyoeleza hapo awali; tayari tuna mkakati wa kuongeza vyombo vya nyumbani tutakavyokuwa na ushirikiano nao; tumekwisha kuongea na ITV na huenda tukafanikisha karibuni.
Zaidi, tumeongea na vyombo vya nje kama Aljazeera, BBC, Redio Ujerumani na CRI kuhakikisha tunawafikia wasikilizaji/wasomaji wao pia. Mikakati ya ushirikiano inaendelea.
E]. Last time jf ilikuwa offline sababu ya service ilichukua muda kurudi na baadhi ya data kupotea kama vile threads na matendo (actions) nyingine kupotea. je mnajiandaaje na changamoto hiyo siku za mbele kwa kuweza fanya marekebisho ya haraka nay a kutopoteza chochote kilichokuwa tayari kipo?
Kwanza:
- Kabla ya kufanya maboresho (miundombinu) tulitoa taarifa; tuliahidi ingechukua siku 2 na kwamba tungejitahidi kufanikisha hili.
- Nini kilifanyika? JF ilikuwa inahama kutoka server moja kwenda nyingine na huku ikiongezwa server ya ziada kwa ajili ya kutunza data endapo kutatokea tatizo lolote. Tulijitahidi lakini kosa lililotokea likawa ni kuruhusu watu kuendelea kuitumia JF wakati tunahamisha data, hapa ikatokea kukuta kuwa kilichokuwa kinawekwa kwenye server ya zamani hakikuhamia kwenye server mpya, tukarudia zoezi, ikafikia siku 3 lakini pia bado tulikuwa hatujashtukia kuwa bado watu walikuwa wanaandika na havichukuliwi; tukaamua kuzima kabisa server ili tufanye kazi ikiwa offline.
Pili:
Tuliomba radhi, tulitambua makosa yetu ambayo kimsingi lengo la kazi lilikuwa ni kuboresha lakini katikati tukakumbana na changamoto; kwetu lilikuwa ni funzo kubwa na tunalitilia maanani ili lisitokee wakati mwingine. Miundombinu tuliyo nayo kwa sasa inaweza kuihudumia jamii yetu kwa miaka mingine walau 4 bila kuathirika; hivyo kwa sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha tunaitunza vema kwa manufaa ya watumiaji wa JF.
*ADDED* LALAMIKENI kuhusu JF kutoweka hewani kwa muda mrefu na posts nyingi na watu waliojisajili kati ya May 13 - May 15 kupotea!
Tunastahili lawama katika hili lakini tunaomba sana radhi kwakuwa kilichotokea hakikutarajiwa. Kimsingi lengo la kufungua ili watu waweze kuendelea na mijadala ni kutaka kutowaudhi wateja wetu. Tumejifunza kutokana na kosa hili na tunawahakikishia halitajirudia.
NINI KILITOKEA?
Tuliona JF kuendelea kuwa katika server moja japo ilikuwa kubwa ilikuwa ni risk kubwa kwetu, tukaamua kupanua wigo wa JF kuweza kupatikana kwa urahisi na kuhakikisha inakuwa salama zaidi; katika mchakato huo, kitendo cha kuhamisha data toka kwenye server moja kwenda nyingine kilishaanza tangu tarehe 12 (kama tulivyowatangazia) na tukajikuta kumbe vyote vilivyoongezeka siku hiyo havikuweza kuingia kwenye database vikawa vimeachwa!
Tumejitahidi sana kuvi-recover lakini ikaonyesha kuwa inaweza kutuchukua muda mrefu sana na kuathiri kuweza kuirejesha JF hewani, tukatambua kuwa kwakuwa wanachama wetu ni waungwana watatuelewa kuwa lengo japo lilikuwa jema lakini athari iliyojitokeza imekuwa nje ya uwezo wetu na hivyo tunawaomba radhi NYOTE.
Niwaombe wadau wachangie JF iweze kujiendesha bila utegemezi, kutuchangia kwa kuwa Premium Members ni kutusaidia kuweza kuwahudumia kirahisi bila vikinza kama hivi. Kuwa tunafanya kila kitu wenyewe ndiko kunapelekea kukumbana na vigingi kama hivi, tungekuwa tuko safi kifedha ni wazi tungewapa kazi hii wataalamu wengine wakasaidia kuhakikisha inafanyika ndani ya muda mfupi sana.
Wenye dhamira ya kuchangia wanaweza kusoma hii thread:
JamiiForums Premium Member Subscription