Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Hakukuwa na mamna tena,zaidi ya kujishusha na kuongea kwa upole ili aonewe huruma,maana ile kashfa ya ushoga siyo ya kitoto[emoji38]

Mbona hajasema kama Diamond alimkopa million 10 na mpaka leo hajamlipa?!Ommy huwezi kuwa msanii bora kwa kutafuta kiki kwa Dee.
Yan wewe naye bana mil 10 alimkopeshaje wakati hakutaka kumpa shavu hata moja? Yan wewe ni hewa

Huyu ndo anaemuongoza pia kumtafutia connections zote za ki international katika kazi yake ya muziki...huyu ndo aliemfanya Domo leo hii kuwa wa kimataifa...personal issues has nothing do with job related matters...huwezi jua pengine anaemuongoza vibaya katika personal issues anaweza ata akawa Zari,Harmonize,au hata mama ake aliemlea na kumkuza...Madudu binafsi ya Domo yasimfanye Sallam achafuke jamani.
Ila huyo sallam inabidi amfundishe domo kumpunguza mihemko inaonyesha kiba anamuumiza kila mtu na alichopangiwa na Mola, tena hata huyo sallam apunguze kiherehere Mara aonekane kila sehemu kiba alipo Mara kuzimiana mic tena sehemu nyingine na kutunga uongo, Mara ahangaike na timu kiba insta chah. Inaonyesha hapendi wasanii wengine wafanikiwe.

Utajiri una mambo yake si kila unachokiona kwa macho ndivyo kilivyo.Watu wanafanya vitu vya hatari maana hakuna anaependa umaskini. Unafikiri kwa nini dogo inakua vigumu kumsamehe baba yake?
Tena nashangaa kumwambia mwenzake anapumuliwa je yeye anayetumia sehemu iliyo mleta duniani je, anafikiri watu hawafahamu labda, hawa wasanii ni shida kweli kweli.

Kuna watu wakifanikiwa hata kama ni rafiki yako atapenda ubakie chini ili uwe unamuomba msaada kila wakati naye atumie mwanya huo kukunyanyasa kiaina

Nashangaa watu wanamsifia kaongea kistaarabu,lazima awe mpole kupumuliwa si mchezo,halafu mbona kamtukana mama wa Mwenzie, Hana tofauti na shish boy kumwingiza mama kwenye ma ugomvi Yao siku wakipatana atamwangaliaje huyo mama amekosa kitu cha kumuumiza nacho Dai,hata kama anajua huyo mama anapenda dogo dogo hakuwa na sababu ya kumwingiza huyo ni kama mamake.Mpaka hapo hii issue ya ushoga Ina walakini, Dai walikuwa karibu sana amekosa kitu chochote anachokijua juu yake mpaka amchanganye mamake?
Yani wewe unafurahia mond alivyomzushia mwenzie mambo ya ushoga at the same time unakasirika ommy alivyosema kuhusu mama yake mond in return.
Ulitaka akaye kimya?

Ukiishi kwenye nyumba ya vioo usianzishe ugomvi wa mawe.

Aisee leo Ommy amewaweza [emoji23] [emoji23]

mi sijaelewa kitu hapo. Ina maana kama Diamond kamuwahi Davido na Iyanya kupiga nae kolabo Ommy haruhusiwi? Au waliingia mkataba kwamba kwa tanzania watafanya kolabo na Diamond tu? msaada kwenye tuta.

Umeongea jambo la msingi ambalo binadamu wengi hawajiulizi. Ommy kafanikiwa kupata huruma ya raia Ila yeye ndio alianza maana alijua kabisa kauli Yake kuhusu kununua viewers itakuwa Na impact kwahiyo Kama ana basara Kama ambavyo wengi wanasema hakupaswa kuongea ile kauli kwenye media

Atashindwaje kua mstaarabu wakat mond kamwaga mboga angetokwa povu tu angeanikwa kweupeeee na bado ndio dawa ya waropokaji nani alimuanza mwenzie izo sympathy zako kwenye interview hazitabadilisha ukweli wa upunga mrs mwarabu ommy msambwanda leo ndo umeshika adabu eeh siulijifanya kujitoa akili kumdiss mond unabahat umejishusha tungeanika kila kitu ebooo moto umewasha mwenyewe na unakuunguza tungemwaga mpaka audio zako unabahati haya kampikie mwarabu huko
Yani leo Ommy amesababisha madale walale saa kumi na moja jioni. [emoji23] [emoji23]

Kaongea nn wengine hatujasikiliza
Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.

Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.

Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.

Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake ‘Number 1’ katika studio za MJ Records.

“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi, nikauchuna tu,” alisema Ommy.

Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa MJ Records na kwamba hakuna safari yoyote.

“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu si nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway labda ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.

Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe kualikwa.

Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection.

“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”

Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada ya kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa ‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema hapa kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”

Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo na Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja wa Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo ameshaiwahi.

Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu kwenye video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja ushkaji wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa macho yake.

Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.

“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu. Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.

Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye post yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka kukutana hakuchagulii tusi.’

“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba!”

Back
Top Bottom