Interviews za Ali Kiba zinaboa; Yeye kwake kila kitu ni "Personal"

Nadhani Mashoto karibu wote wako hivyo, aidha wasiri sana ama hawasomeki kabisa yani shagalabagala. Ally Kiba hana tofauti na shemeji yangu.
Shemeji umeamua kunianika hapa?!
 
Kigoma sio watu wazuri hata zitto huwa haelezi Mali zake kiukweli
 
Jamaa ana majivuno ya kibwege nilisikia anasema sijafanya collabo na FM ni wacongo fulani hivi siwajui Manwater ndio anawajua!dah unafanya collabo na watu na haikusumbui kutojua majina yao au anawajua ila anahisi atawapromote?
 
Sijaiona enterview yake,,ila kutokana na comments za humu,,naona jamaa aache tu kufanya enterviews ,kwa sababu haziwezi,,,sasa mtu unajenga nyumba,ukiulizwa kuhusu hiyo nyumba hutaki kuongea,,ni wazi jamaa hajui maana ya kuwa public figure
Wakati nyumba za akina Kanye,Diddy nk zimeonekana duniani kupitia tour wanazowapa waandishi!Mwanamuziki unatakiwa ukipata nafasi ya publicity ujiachie sio hata swali sio personal unasema najianika;hivi ukijibu nilikutana na wife kwa mara ya kwanza sokoni linakuharibia nini?Seven anam manage msanii wa ajabu najua kwa exposure yake hata yeye hafurahii
 
kibakuli ni mshamba.....kuna siku dozen alikuw anamhoji kuhus richone kusajili line kwa jina la kibakuli na kutapeli watu,akasema ishu hiyo hawezi zungumzia ....dozen akampiga bit watu wanataka kujua jamaa kakomaa,dozen akamwambia poa basi tufanye interview yetu imeishia hapa na ndo mwisho wako kufanya interview na dozen/xxl.kibakuli baada ya kuona mungu mdogo wa show ya mchana toka mawimgu kamind' mwemyewe ikabid afunguke..

conc.majibu yake pia yanategemea 'ntu na ntu'akiona huyu nammudu anajichagulia maswali yanayompendeza.
 
Kiukweli ali kiba hajui kujieleza nimefatilia interviews zake nyingi yuko very low kwenye kujieleza
 
Ni muda umepita sijachangia chochote JF ila kwa hili nimeshindwa kabisa kujizuia kwa kumtakia mema Ali Kiba na mustakabali wa bongo flavour kwa ujumla. Interview za huyu bwana nimeziona nyingi ila hizi za mwisho zinasikitisha sana. Ni vizuri na meneja wake akipata ujumbe amshauri akubali kujifunza.

Shida yake si elimu ni kutokuwa na kipaji cha kujieleza na kutokuwa na nia ya kujifunza (rigid). Si kwamba anaficha siri au nini. Ni kwamba hawezi kujieleza. Na hii si kwa interview za hapa TZ ni hata interview za nje. Kuna wakati alikuwa kwenye Red Carpet South Africa akaulizwa swali simple tu "mavazi yako yamekuwa inspired na nini/nani?" majibu yake dah...yaani wenye uzalendo kama sisi inabidi ushike mdomo. Shida hii vile vile iko kwenye interview zake za kenya.

Nasema hoja si elimu sababu rafiki yake Ommy Dimpos ambaye viwango vyao vya elimu ni kama sawa ana uwezo mzuri sana wa kujieleza. Interview zake Ommy Dimpos utazipenda tu hata kama asipozungumzia chochote "personal".

Na hakika Ali Kiba kwenye mazingira ya kawaida ni mtani na mcheshi ila akiwa kwenye mazingira rasmi ( formal setting) ya interview anajikanyaga. Tujiulize ni kwa nini?

Jibu lake nadhani liko kwenye saikolojia (psychology). Huyu bwana amelemewa (burdened) na umaarufu na ushindani wake (au beef) na msanii/wasanii fulani. Hii inamkwaza kwenye kujieleza (kuji express) sababu kila wakati anahisi analinganishwa na msanii/wasaii fulani. Akitaka kutengeneza sentensi mawazo ya ya beef yanamuingia kichwani anajikuta anakosa mtiririko mzuri (consistency) kwenye kujieleza kwa hiyo anajichanganya.

Hata kwenye kutoa nyimbo ana stress nyingi ndio maana anachukua muda mwingi sana kutoa nyimbo moja. Na anashindwa ku-explore collabo na kufanya na producers tofauti etc. Ni kwamba hayuko free ku-enjoy fani yake. Yuko "rigid" kila angle.

Yaani huu ujumbe naomba meneja wake auone sababu inasikitisha. Kushidwa kujieleza, pamoja na mambo mengine, kunamfanya achukulie mambo "for granted". Kwa mfano, kwenye kipindi cha "Clouds 360" pamoja na presenter Baby Kabae kumbeba ili interiew ipendeze Ali Kiba alimaliza interview bila kutoa shukrani (ku-appreciate). Yaani anabebwa bado haoneshi hisani na cooperation. Kwa promo ya ngoma yake mpya na kinywaji chake kimpya clouds media alitakiwa kushukuru sana. Ali Kiba anahitaji coaching na practice za interviewing (kwa kiswahili).

La mwisho ni hukusu social media. Biashara ya enterntainment kwa kizazi kipya cha sasa huwezi kujitenga na socia media. Yeye Ali Kiba amesema wazi hayuko kwenye social media, instagram etc. Huyu ata survive vipi?. Ni wazi kwa "burden" ya competition aliyo nayo hawezi kujikusisha (ku handle) social media. Hili jukumu inabidi lichukuliwe na management yake. Msifikiri ma celeb wakubwa wanafuatilia social media yenye mamilioni ya followers wenyewe si kweli. Ni wasaidizi wao wanafuatilia social media kwa niaba ya hao celebrities.
 
nilikereka sana na interview yake ya shilawaduj, hamna cha maana hata alichokiongea, mashauzi mengi sana na kujiskia,
uchafu
 
Ukwel mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…