Ubavu
JF-Expert Member
- Jun 19, 2012
- 2,790
- 3,263
Shemeji umeamua kunianika hapa?!Nadhani Mashoto karibu wote wako hivyo, aidha wasiri sana ama hawasomeki kabisa yani shagalabagala. Ally Kiba hana tofauti na shemeji yangu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shemeji umeamua kunianika hapa?!Nadhani Mashoto karibu wote wako hivyo, aidha wasiri sana ama hawasomeki kabisa yani shagalabagala. Ally Kiba hana tofauti na shemeji yangu.
Mi ni shabiki wake lakini. Sasa nimchoka kwa interviews zile alizofanya.
Utafikiri ni underground.
Sijui ji kuringa??
In Lowassa's voiceElimu elimu elimu
WellExposure...Uswahili....Shule
Sasa hata watu aliofanya nao collabo nayo ni issue binafsi?mnatetea upuuziTatizo unataka kusikia unachokitaka wewe. Ukijiweka kusikiliza anachokisema muhusika hutaboreka.
Wakati nyumba za akina Kanye,Diddy nk zimeonekana duniani kupitia tour wanazowapa waandishi!Mwanamuziki unatakiwa ukipata nafasi ya publicity ujiachie sio hata swali sio personal unasema najianika;hivi ukijibu nilikutana na wife kwa mara ya kwanza sokoni linakuharibia nini?Seven anam manage msanii wa ajabu najua kwa exposure yake hata yeye hafurahiiSijaiona enterview yake,,ila kutokana na comments za humu,,naona jamaa aache tu kufanya enterviews ,kwa sababu haziwezi,,,sasa mtu unajenga nyumba,ukiulizwa kuhusu hiyo nyumba hutaki kuongea,,ni wazi jamaa hajui maana ya kuwa public figure
kibakuli ni mshamba.....kuna siku dozen alikuw anamhoji kuhus richone kusajili line kwa jina la kibakuli na kutapeli watu,akasema ishu hiyo hawezi zungumzia ....dozen akampiga bit watu wanataka kujua jamaa kakomaa,dozen akamwambia poa basi tufanye interview yetu imeishia hapa na ndo mwisho wako kufanya interview na dozen/xxl.kibakuli baada ya kuona mungu mdogo wa show ya mchana toka mawimgu kamind' mwemyewe ikabid afunguke..Tofauti na masuper wengine ambao ukiangalia interviews zao mtazamaji utajifunza kitu kutoka kwake, na ataku-inspire kwa namna moja au nyingine.
Huyu mheshimiwa, kati ya maswali 10 atakayoulizwa atajibu 2 tu!
Yeye kwake kila kitu nni PERSONAL... Aaagrh, wewe ni msanii mkubwa bwana, watu wanapenda kujua na kujifunza kutoka kwako including some of your personal life stories (Sio kila kitu off course cha kuweka hadharani) lkn kwako ni too much!
Sasa umejipeleka mwenyewe kwenye vipindi kama LEO TENA na SHILAWADU, na unajua kabisa aina za interview ambazo huwa zinafanyika kule, matokeo yake kila saa unatishia kuondoka...
THIS IS TOO LOW BROTHER!
Ukwel mtupuNi muda umepita sijachangia chochote JF ila kwa hili nimeshindwa kabisa kujizuia kwa kumtakia mema Ali Kiba na mustakabali wa bongo flavour kwa ujumla. Interview za huyu bwana nimeziona nyingi ila hizi za mwisho zinasikitisha sana. Ni vizuri na meneja wake akipata ujumbe amshauri akubali kujifunza.
Shida yake si elimu ni kutokuwa na kipaji cha kujieleza na kutokuwa na nia ya kujifunza (rigid). Si kwamba anaficha siri au nini. Ni kwamba hawezi kujieleza. Na hii si kwa interview za hapa TZ ni hata interview za nje. Kuna wakati alikuwa kwenye Red Carpet South Africa akaulizwa swali simple tu "mavazi yako yamekuwa inspired na nini/nani?" majibu yake dah...yaani wenye uzalendo kama sisi inabidi ushike mdomo. Shida hii vile vile iko kwenye interview zake za kenya.
Nasema hoja si elimu sababu rafiki yake Ommy Dimpos ambaye viwango vyao vya elimu ni kama sawa ana uwezo mzuri sana wa kujieleza. Interview zake Ommy Dimpos utazipenda tu hata kama asipozungumzia chochote "personal".
Na hakika Ali Kiba kwenye mazingira ya kawaida ni mtani na mcheshi ila akiwa kwenye mazingira rasmi ( formal setting) ya interview anajikanyaga. Tujiulize ni kwa nini?
Jibu lake nadhani liko kwenye saikolojia (psychology). Huyu bwana amelemewa (burdened) na umaarufu na ushindani wake (au beef) na msanii/wasanii fulani. Hii inamkwaza kwenye kujieleza (kuji express) sababu kila wakati anahisi analinganishwa na msanii/wasaii fulani. Akitaka kutengeneza sentensi mawazo ya ya beef yanamuingia kichwani anajikuta anakosa mtiririko mzuri (consistency) kwenye kujieleza kwa hiyo anajichanganya.
Hata kwenye kutoa nyimbo ana stress nyingi ndio maana anachukua muda mwingi sana kutoa nyimbo moja. Na anashindwa ku-explore collabo na kufanya na producers tofauti etc. Ni kwamba hayuko free ku-enjoy fani yake. Yuko "rigid" kila angle.
Yaani huu ujumbe naomba meneja wake auone sababu inasikitisha. Kushidwa kujieleza, pamoja na mambo mengine, kunamfanya achukulie mambo "for granted". Kwa mfano, kwenye kipindi cha "Clouds 360" pamoja na presenter Baby Kabae kumbeba ili interiew ipendeze Ali Kiba alimaliza interview bila kutoa shukrani (ku-appreciate). Yaani anabebwa bado haoneshi hisani na cooperation. Kwa promo ya ngoma yake mpya na kinywaji chake kimpya clouds media alitakiwa kushukuru sana. Ali Kiba anahitaji coaching na practice za interviewing (kwa kiswahili).
La mwisho ni hukusu social media. Biashara ya enterntainment kwa kizazi kipya cha sasa huwezi kujitenga na socia media. Yeye Ali Kiba amesema wazi hayuko kwenye social media, instagram etc. Huyu ata survive vipi?. Ni wazi kwa "burden" ya competition aliyo nayo hawezi kujikusisha (ku handle) social media. Hili jukumu inabidi lichukuliwe na management yake. Msifikiri ma celeb wakubwa wanafuatilia social media yenye mamilioni ya followers wenyewe si kweli. Ni wasaidizi wao wanafuatilia social media kwa niaba ya hao celebrities.
Huyo mkewe aliyempeleka anafanya muziki?
Mkewe ni kitu chake binafsi sasa alikibeba cha nini kwenda nacho studio?Au mbunye ya mkewe ni ya jamii watu tuanze inyatia?Umeshasema **binafsi** alafu unataka uyajue [emoji23][emoji23]
Kwa vile yeye hapafahamu CMG?Mkewe alimsindikiza