Interviews za Ali Kiba zinaboa; Yeye kwake kila kitu ni "Personal"

Interviews za Ali Kiba zinaboa; Yeye kwake kila kitu ni "Personal"

Kumbe ndo mnamuona saizi tu uyu jamaa anamajivuno sana na kujiona watu awajui tu
 
kibakuli ni mshamba.....kuna siku dozen alikuw anamhoji kuhus richone kusajili line kwa jina la kibakuli na kutapeli watu,akasema ishu hiyo hawezi zungumzia ....dozen akampiga bit watu wanataka kujua jamaa kakomaa,dozen akamwambia poa basi tufanye interview yetu imeishia hapa na ndo mwisho wako kufanya interview na dozen/xxl.kibakuli baada ya kuona mungu mdogo wa show ya mchana toka mawimgu mwemyewe ikabid afunguke..

conc.majibu yake pia yanategemea 'ntu na ntu'akiona huyu nammudu anajichagulia maswali yanayompendeza.
hahahha dah natamani ningeisikiliza hiyo interview....umesimlia vizuri hadi raha
 
Wewe mtoto wa kiume ujue...unataka kufahamu siri zipi za alikiba...mmeuliza swali lolote kuhusu mziki wake akadhindwa kulijibu...or mnataka kujua kuwa huwa anamgegeda bao ngapi wife wake
Ndugu unatakiwa utambue kuwa wale watangazaji ni watu wenye elimu na kazi yao pamoja na maadili kwaiyo awawezi kumuuliza maswali nje ya utaratibu na misingi ya utangazaji kwaiyo yeye mwenyewe ndo anatakiwa atumie akili kujibu na sio kuacha nafasi wazi, je atajibu nani ayo maswali kama sio mhusika? Ajipange upya next time ali.
 
Unapohoji Ali kaenda kufanya nini kwenye interview, wote tunajua kaenda kuhojiwa. Lakini lazima wakati mwingine watu mjiongezee maarifa hata kama mnayo machache, mjifunze kuwa kila kitu kina mipaka yake. Kuna watu hatupendi muziki wa Ali Kiba, lakini tunapenda life style yake ni moja kati watu wanaojitambua sana! Eti kajamaa kana maringo, sikapendi! Ha ha ha ha guys maringo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu...wengine hatuwezi kuwa na maringo sababu hatuna maisha mazuri!
 
Mwanaume kumjadili mwanaume mwenzie hii kwa sisi tunaobeti tunaiita kuchanika kwa mkeka
 
Sina team ila Kiba mshamba sana kwenye interviews,yani kama jana kwenye interview msanii kaulizwa anafanya nini apart from music akasema biashara alafu akakata kuitaja wakati hapo ilikuwa promo ya bure
 
Ndugu unatakiwa utambue kuwa wale watangazaji ni watu wenye elimu na kazi yao pamoja na maadili kwaiyo awawezi kumuuliza maswali nje ya utaratibu na misingi ya utangazaji kwaiyo yeye mwenyewe ndo anatakiwa atumie akili kujibu na sio kuacha nafasi wazi, je atajibu nani ayo maswali kama sio mhusika? Ajipange upya next time ali.
Nyie washabiki wa chaijaba..mtafutieni chaijaba interview ili ajibu mnavyotaka nyinyi...alikiba tuachieni c washabiki wake tunampendea hiyo life style yake...tangu lini nyi mashabiki wa chaijaba mmeanza kuwa washauri wa alikiba kimuziki
 
Ali kiba ni MTU maarufu,

Umaarufu wa Ali kiba unatokana na kazi zake za Burudani za Mziki.

Na

Wala hautokani na Maisha take binafsi.

Mtoa mada,
Jifunze kutofautisha kati ya:

Ali kiba (Mwanamuziki) na Ali kiba (MTU binafsi)

Kwenye ile interview nyingi,
Ali kiba hualikwa kama Ali kiba (mwanamuziki) na Sio Ali kiba (MTU binafsi)

Kwahyo:
Sio vema kabisa kumuuliza maswali ya binafsi(personal)

Kwenye interview alokwenda kama Ali kiba (mwanamuziki) na sio Ali kiba (MTU binafsi)

Hitimisho:
Alikiba yuko sahihi kabisa
Na ningependekeza wasanii wengine waige tabia km hiyo.

NI VEMA KUKAWEPO MIPAKA, MAISHA YA KAZI (USANII) YASICHANGANYWE NA MAISHA BINAFSI(PERSONAL LIFE)

Wasanii nao ni binadamu kama sisi, Wana Uhuru wa kua na Faragha ktk MAISHA yao.

Ova
 
Back
Top Bottom