Shida ni either mmevamia mada au mmeleta sentiments sababu magari yenu pendwa yanaongelewa weaknesses zake. Mada hii ilianza baada ya mchangiaji mmoja kuisifia RR kuwa inpita kwenye tope, mawe n.k Nasisitiza hii siyo strong point yake, actually kama unataka kuitupa hii gari mapema itumie hivyo hata kama una hela. Hao kina Jay Z ambao mnaonyesha hapa wakishuka kwenye RR na wamarekani wengine mnaosema wanazinunua sana hizi gari tafuteni kujua wanazitumiaje hizi gari, ni kwenye njia nzuri. Chukua LC na hii RR nenda nazo huko mara kwa mara uone nani atakuwa narudi salama au bila ngeu.
RR itabaki kuwa more luxurious, sophisticated with more features lakini least reliable over time when it comes to matumizi kama kwenye hili tangazo compared to LC/LX. Tunaposema its less reliable hatuangalii zimenunuliwa ngapi, tunaangalia matatizo mangapi yamekuwa reported kwa percentage. Kama mnabishia na hizo numbers basi tena.
Mada inahamishwa sana, mara toyota vs other brands, mara Benz vs Toyota. Mimi sikuwahi kusema kila brand tofauti na toyota ni unreliable. Kwanza hata gari nayomikiki siyo toyota.
Na kikubwa cha mwisho, hakuna anayekushauri au kukushawiahi usinunue RR, hapa ni ukweli tu unasemwa kwamba they are less reliable than LC or LX especially kwa matumizi yote (on road na offroad). Kama una data za kupinga hili leta, msilete habari za ipi ni luxury au ipi inauzwa sana, hiyo inajulikana, kwamba ni luxury zaidi, ni comfortable zaidi kuiendesha, ina features nyingi zaidi, na inaharibika zaidi.