Mkuu Paskali, bahati mbaya leo sikuangalia kipindi cha "Jicho letu ndani ya habari". Mimi ni miongoni mwa wafuatiliaji wasiopenda kukikosa bila kujali aina ya wageni wa siku husika. Mchango wangu unaweza kuwa na mapungufu kwa kuwa nitategemea tu ndondo ulizotuwekea. Nionavyo mimi:
1. Suala la gharama/fedha sidhani kama ni kikwazo kama ambavyo wachangiaji wengine walivyoeleza. Nafahamu kwamba Tanzania Media Fund (TMF) huwa wanafadhili kazi za uchunguzi wa kihabari wanapopelekewa wazo. Nafahamu pia zipo habari za uchunguzi ambazo kuchunguzwa kwake hakuhitaji gharama kubwa.
2. Mazingira ambayo akina marehemu Stan Katabalo walifanya "investigative journalism" ni tofauti mno na mazingira ya sasa, kwahiyo wakati mwingine tunapofanya reference kwao tunaweza tusiwe sahihi sana.
3. Hivi ni kwa kiasi gani wamiliki wa vyombo vya habari ambako tunataka hawa waandishi wa habari za uchunguzi wako tayari kuona vyombo vyao vinachapisha/kutangaza hizo habari? Vipi kuhusu wahariri, ni kwa kiasi gani wako tayari kupokea ideas kutoka kwa waandishi wao, za kufanya hizo habari za uchunguzi hata kwa waandishi wenyewe kujigharimia? Hivi hawa wahariri ambao tunaona wakikabidhiwa cheki za mamilioni ya fedha ili kuendeshea jukwaa lao wako tayari kupokea mawazo hayo na kupokea habari za uchunguzi zinazohusu taasisi zinazowamwagia hizo fedha?
4.Serikali iko tayari au inaruhusu kiasi gani habari za aina hiyo? Sio kwamba kuna ukomo? Hili tunaweza kufanya comparison kidogo kwa kuangalia namna vyombo vya habari vilivyokuwa vikifanya hiyo investigative journalism katika awamu iliyopita na hii ya tano. Paskali, hata gazeti lililotolewa hapa kama mfano-Mwanahalisi-halifanyi tena hiyo investigative journalism awamu hii, bali "linaokoteza" tu!
Mimi ninaamini kwamba nchi hii ina hazina ya waandishi wa habari wengi tu, ukiwemo wewe, ambao wanaweza kufanya investigative journalism lakini hizo kazi zitachapishwa au kutangazwa na chombo gani leo?
Karibu "mbuzi katoliki" hapa Banana!