Investment In Livestock Industry

Chibingwa

Member
Joined
Jan 17, 2008
Posts
49
Reaction score
7
Wakuu heshima zenu.
Nina interest ya kuwekeza kwenye hii sector ya ufugaji either kwa kushilikiana na NARCO au na watanzania wenye blocks.
Eneo liwe kwenye Kikula Ranching complex ambayo inajumuisha Kikula yenyewe, Kagoma na Mabale, eneo la pili ni Missenyi Ranch.
Kama kuna mudau mwenye kuelewa mchakato mzima wa upatikanaji wa blocks (ingawaje indaiwa blocks zote zimeshachukuliwa na wajanja) basi naomba anijuze pia kama kunamtu mwenye block na anahitaji mtu wa kushirikia nae pia aniambie.
Shukurani
 
Nadhani Umeshachelewa..............ushauri wangu..........sio lazima uwe karibu na hayo mashamba ya serekali...kwani hayana msaada wowote...tafuta eneo...cha msingi....uwe na chanzo kizuri cha maji...jifunze kuotesha na kusindika chakula cha mifugo...ingia kwenye biashara....ukitaka mbegu ya myama yeyote hapa duniani inapatikana ......kila la kheri
 

ni kweli ushauri mzuri. Swali langu wapi unaweza kupata mbegu bora kupandishiwa ng'ombe wako na wataalam pia. Nafikiri Kenya wanafanya artificial insemination, Tanzania ipo na gharama zake?
 
ni kweli ushauri mzuri. Swali langu wapi unaweza kupata mbegu bora kupandishiwa ng'ombe wako na wataalam pia. Nafikiri Kenya wanafanya artificial insemination, Tanzania ipo na gharama zake?

Mama Joe kwa TANZANIA kwa hivi sasa ukitaka mbegu kutoka SOUTH AFRICA Marekani na kwingineko zinapatikana tena kwa wingi.....na maanisha artificial insemination.......wapo watu wanaziuza wewe ukiwa tayari niambie nikuunganishe nao...kuna aina Fulani ya ngombe wanaitwa FLECKVIEH ni wazuri saana hawa jamaa Fleckvieh Genetics East Africa Ltd - Fleckvieh Genetics Sire Waterberg wanauza shahawa zake Kenya wanamanufaa saana hususan kwa huu ukanda wa pwani....kuna agent wao hapa Tanzania nimewasiliana nao kwa mail hawajanijibu bado
 
Blocks nazozijua mimi ni za Kitengule Ranch. Part of it was sold to Kagera Sugar and blocks were leased to groups of people on 35yrs tenure. Kama uko serious PM nikupe namba ya mzee mmoja unaweza kushirikiana nae coz anayo block imepakana na mto wa Kagera.
 

i see utakuwa umenifaa sana nitahitaji kuanzia october mwishoni ili nikiweza nipandishe wawili, ngoja nijaribu ongea na vet kama anajua kuwawekea inabidi nitafute mtaalam. Nikifika nitapitia hii link vizuri. Blessings
 

Ukiwa na Vifaaa unawafuata mwenyewe, Sisis tuliwafuata Nairobi wakatupatia Mbegu, Ingawa hata Ndama unaweza pata ila muda wa kusubilia unaweza kuwa hata miaka miwili.
 
Serio, shukurani sana na nimesha ku pm.
waweza nipatia namba yako au nipigie kwa hii namba 0784558677.
 
Ukiwa na Vifaaa unawafuata mwenyewe, Sisis tuliwafuata Nairobi wakatupatia Mbegu, Ingawa hata Ndama unaweza pata ila muda wa kusubilia unaweza kuwa hata miaka miwili.

asante Chasha ila hii ya vifaa na kwenda kuzileta mtu wa kukuwekea anapatikana wapi? Nafikiri hao walio agent hapa Tanzania ndio wanatufaa wafugaji wadogo tunaoanza.
 
asante Chasha ila hii ya vifaa na kwenda kuzileta mtu wa kukuwekea anapatikana wapi? Nafikiri hao walio agent hapa Tanzania ndio wanatufaa wafugaji wadogo tunaoanza.

Mama Joe, Semens haziuzwi gali saana, cha msingi tafuta ngombe hawa wa kisasa ambaye ameshazaa mara moja, ukishapata ndio uanze kufikiria hizi mbegu....sio madaktari tu wa mifugo wanapandisha hata vijana waliomaliza Tengeru wanafanya kazi hiyo...swala la mbegu sio tatizo hata kidogo,,,hata ukienda hapo ubungo angalia maduka ya kuuza madawa ya mifugo utaona kuna mtungi wa hizo semens kuwekewa haizidi shilingi za kitanzania elfu 40....huo ni ukweli kabisa...kuhusu hawa fleckiveh kama SHASHA alivyosema ukiwa na huo mtungi hata hao watu unaweza arrange nao waaaaaakakutumia kwa njia ya basi...hawa ni ngombe wazuri saana
 

i see nimejifunza kitu hapa najua ivo vifaa havipo wala hii elimu haijaenea kumbe inawezekana kabisa. Asante Prodigal Son wiki ijayo nitapita kuulizia vifaa, hadi end of october kitaeleweka tu. Ubarikiwe
 
i see nimejifunza kitu hapa najua ivo vifaa havipo wala hii elimu haijaenea kumbe inawezekana kabisa. Asante Prodigal Son wiki ijayo nitapita kuulizia vifaa, hadi end of october kitaeleweka tu. Ubarikiwe

Mama Joe hakuna haja ya kununua hicho kifaa cha msingi tafuta kwanza ngombe watakaopandikizwa hizo semen,,,naamini ukishapata hizo semen upatikanaji wake sio tatizo hata kidogo kwa mfano ukitaka VIKING GENETICS ASAS ni agent wao kwa Tanzania,,, Fleckiviah zinapatikana hapo Kenya uakachokifanya ikishapata Ngombe ukijua labda wanaweza pata heat mida gani hata ukija hapa jukwaani kutafuta mtu mshirikiane kuchukua semenkutoka Kenya mbona rahisi saana....cha msingi tafuta hao ngombe utakaokuja kuwapandikiza kwanza ukishawapata uingie kwenye hatua ya kutafuta hay mashahawa
 

ng'ombe ninao sema unaposema hiyo ya kuwa weshazaa ndo sijaelewa maana mmoja nilipewa ndama anaanzia kwangu huyu haitawezekana basi nitaanza na mmoja ambaye tayari tunamtazamia kuingia kwenye joto ila mbegu za jirani sikuzipenda. Nitawasiliana na wewe kwa ushauri zaidi
 

Mama Joe, ngombe aina ya fleckivieh ni wakubwa na kama utawapandikiza, ngombe anatakiwa awe na maumbile makubwa ndio maana nkakuam bia angalau awe amepata uzao moja,.....kama anaumbo ndogo ukijakupandishia hayo mashahawa wakati wa kuzaa au kipindi akiwa na ujauzito anaweza zidiwa uzito ukaishia kupata hasara....akafa kabla au kipindi anajifungua..... kama nilivyokuambia mashahawa ya fleckivieh( kumbuka wana aina mbalimbali sio gali mfano as of wiki hii Fleckivie genetics east Africa walikuwa na mbegu BFG - MERU BEI 2,500/= KSH NA MANGFALL BEI 4,000/= Pesa ya Kenya ukibadilisha na ya TZ sidhani kama inazidi TSH 22 KWA KSH MOJA,,bei ya A.I CONTAINER ya litres 02 ni KSH 26,000/= naamini haya mambo yanawezekana mkiwa watu kuanzia wawili mbegu zinapatikana
 

okay sasa nimekupata vizuri sana. Nashukuru umenifumbua macho sana, haya ya ukubwa au aina nitamuuliza Vet akija next week. Kama hawafai nitajipanga niongeze hata mmoja wa kutengenezea mbegu. Pia najaribu kuwasiliana na mfugaji jirani kama atakubali ku share cost. Greatly inspired! Stayblessed
 
Wakubwa naomba kutoa feedback ya huu mchakato wangu.
Kwanza nianze kutoa shukurani zangu kwa wote waliochangia hii mada, pili niwashukuru wale wote walio weza kutoa mwongozo wa nini nifanye ili kufanikisha swala hili.
Kimsingi nimeweza kutembelea mashamba yote yaliyopo katika mkoa wa Kagera (Missenyi, Kagoma, Kikukula, Mabale) na kuweza kukutana na watu walio pewa vitalu na wachache wawo wanatafuta watu wa kuweza kushirikiana nao kuendeleza hivyo vitalu.
Kwasasa niko katika hatua za mwisho kukamilisha makubaliano na mtu ambaye tushirikiana nae kuwekeza kisasa kwenye moja ya block za Kagoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…