Ione meli mpya ya Songoro Marine, gumzo Kanda ya Ziwa

Ione meli mpya ya Songoro Marine, gumzo Kanda ya Ziwa

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Ni meli mpya ya mwendokasi iliyotengezwa na kampuni ya wazawa Songoro Marine Yard ya jijini Mwanza iliyozinduliwa katika Ziwa Victoria ambayo imejizolea umaarufu kutokana na ubora wake pamoja na kurahisisha zaidi huduma za usafiri kati ya Mwanza na kisiwa cha Ukerewe.

Kampuni za wazawa zinao uwezo pale zinapoaminiwa.

Pia Soma....
Kampuni Ya Songoro Marine yanyimwa tender ya ukarabati wa kivuko "MV Magogoni" - Songoro Marine waanza kuisoma namba, wanyimwa kazi ya Kivuko cha Magogoni
 
Ni meli mpya ya mwendokasi iliyotengezwa na kampuni ya wazawa Songoro Marine Yard ya jijini Mwanza.Iliyozinduliwa katika Ziwa Victoria
Ambayo imejizolea umaarufu kutokana na ubora wake pamoja na kurahisisha zaidi huduma za usafiri kati ya Mwanza na kisiwa cha Ukerewe.
Kampuni za wazawa zinao uwezo pale zinapoaminiwa.

Hongera Songoro
 
Kama naiona vile serikali ya awamu hii na yale majungu yake ya kuwaza 10% tu kwenye manunuzi yake, badala ya kuwaimarisha wawekezaji wazawa ili kuinua uchumi wa nchi.

Wako radhi wakanunue bidhaa nje ili wapate 10%, kuliko kununua bidhaa ya aina hiyo hiyo inayotengenezwa nchini. Uzalendo 0! Ubinafsi na upigajj ndiyo vimetawala.
 
Uliziona meli zake za Ziwa Nyasa zilizotaka kuua abiria ?
Wewe Erythrocyte tayari tumekuona ukiwa na chuki binafsi kwa Songoro Marine.
Ushahidi ni hiyo thread yako hapo chini
Erythrocyte Ngoja nikueleze kuhusu Songoro Marine.

Hii kampuni iko kwenye hiyo industry kwa miaka si chini ya arobaini.
Songoro wamejenga Meli na vivuko vingi sana hapa nchini na hata nchi za nje,hususan Uganda na Kenya.

Pia ndio waliojenga kivuko kipya cha MV Nyerere huko Ukara.
Baada ya kile cha Mv Ukara kuzama.

Si hivyo tu...
Vivuko ba Boat karibia zote zinazofanya kazi ndani ya Ziwa victoria,vimejengwa na Songoro Marine.

Hizo Meli unazozitaja wewe kule Ziwa Nyasa,zilisimama kwa hujuma.
Baada ya kuwa zinabeba mzigo wote kwa urahisi na kuwakosesha biashara wamiliki wa boti ndogondogo,ambao kimsingi ndio walikuwa wamehodhi biashara hiyo.

Kama ni uongo. Erythrocyte lete vielelezo au hata headline moja ya press

Iliyowahi ripoti ubovu wa vyombo hivyo kutokana na kujengwa vibaya.
 
Juzi nimeona habari jinsi China ilivyoipiku Korea kusini ktk uundaji wa meli za kisasa.
Waafrika tunaweza amua fanya mapinduzi kama tunadhamira, kama China imeweza hata susi tunaweza. Kampuni hio ionwe kwa jicho la tatu, ni uthubutu mkubwa wa kimapinduzi.
Revolution is a hard and long process
Waafrka huwa wanapenda kujibeza na kujidunisha, ingekuwa ni kampuni ya mzungu,muhindi,mwarabu au mchina viherehere wengi humu wangepongeza.
 
Songoro Marines ni tafsiri halisi ya BBM ya Young D.

Nchi ya majungu na umbea hii,wenzetu watu kama hawa wanawezeshwa zaidi.

BTW:KP Motors ya Kipanya imeishia wapi? Nilimuona Katibu Mkuu wa "nyokanyoka" akipiga siasa za uwezeshaji.
 
Umenikumbusha. Kitu kuhusu Kipanya Motors!
 
Katengeneza meli nyingi tu na vivuko na tena hajaanza wakati we ulipomjua. Je umeuliza hiyo meli ilikuwa na hitilafu gani?
Wewe ndie ungeleta hapa,sio sisi tunaomuamini Songoro bali wewe unaemchukia Songoro Marine!
Ili tuone ukweli wako!
 
Bar ya vichaa watakuja kuwambia Songoro alikuwa na kadi ya CCM so hakupaswa kupewa tenda

USSR
Songoro Marines na Mayanga Constructions mmiliki mkubwa kalala Chato.
 
Kama naiona vile serikali ya awamu hii na yale majungu yake ya kuwaza 10% tu kwenye manunuzi yake, badala ya kuwaimarisha wawekezaji wazawa ili kuinua uchumi wa nchi.

Wako radhi wakanunue bidhaa nje ili wapate 10%, kuliko kununua bidhaa ya aina hiyo hiyo inayotengenezwa nchini. Uzalendo 0! Ubinafsi na upigajj ndiyo vimetawala.
Yaani inafikirisha sana. Mtu yuko radhi atoe pesa zetu za kigeni nje kuliko kumpa Mtz mwenzie ndani kisa 10%
 
Amekimbia Bukoba, kaipeleka Gozba, huko tunapeleka clarias, ukerewe tunapeleka chombo ingine.

Hizo meli za JPM mpaka akaziuze kisumu
 
Amekimbia Bukoba, kaipeleka Gozba, huko tunapeleka clarias, ukerewe tunapeleka chombo ingine.

Hizo meli za JPM mpaka akaziuze kisumu

Mwanza Goziba masaa hayazidi 4 afu nauli sio kubwa jamaa katisha sana
 
Back
Top Bottom