Kuroot ni kama kufungua mlango kwenye Android ambao utakuwezesha kubadili mpangilio wa simu yako jinsi unavyotaka. Kwa hiyo kuroot kunategemeana zaidi na model na version ya simu yako, kuna nyingine kuroot itakubali kwa root file ambalo utaflash, kwa wengine itakubali kwa adb na command line ya windows, kuna wengine wataroot kwa app ya simu, inategemeana na mfumo wa software na hardware kwenye simu yako. Kwa hiyo unaweza kufanya utafiti kidogo kama simu yako inaweza kupata root access, halafu unatafuta files specific za simu yako. Hapo inakuwa rahisi zaidi.