iOS 16 kuanza kutumika leo saa 2 usiku

iOS 16 kuanza kutumika leo saa 2 usiku

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
iOS 16 inategemewa kutoka leo kuanzia mida ya saa 2 Usiku, na latest report ya mwisho ambayo imevuja inaonyesha mabadiliko mapya ambayo yatawakuta wale ambao wanatumia AirPods feki!

1662986663417.png


Code ya iOS16 iliyotoka wiki iliyopita inaonyesha iOS 16 ina uwezo wa kutambua kama AirPods ni original au ni feki. Apple inaweka utaratibu mpya wa iPhone kumkumbusha mtumiaji kuwa AirPods ambazo anatumia ni feki, wakati akiwa anajaribu kuunganisha AirPods ambazo sio original.

Tayari Apple ina utaratibu huo katika Battery, Kamera, na Display ambazo sio original; katika Sehemu ya Settings kuna ujumbe wa Warning ambao unaonyesha kuwa simu inatumia kifaa ambacho ni feki.

Ukiunganisha AirPods feki, iPhone itakuwa inakupa ujumbe ambao unasema ; “These headphones could not be verified as genuine AirPods and may not behave as expected,”.

Hii itasaidia kwa wale ambao wanauziwa AirPods ambazo sio original na kudanganywa kuwa ni original. Itasaidia kutambua kama AirPods ambazo unazitumia ni feki au ni original.

Ila kwa wale ambao wanafahamu kuwa wanatumia AirPods feki, hawatapenda ujumbe wa Warning za kuwakumbusha kuwa wanatumia kifaa feki. 😅

Let’s wait ikitoka, tuone message yake ya Warning inavyoonekana.

CREDIT @itsapolloo
 
Wamechemka! maana huo muda mi ntakuwa tayari nimelala
 
mara saa nne asubuhi mara saa mbili.hawaeleweki.
 
Iwe kweli leo maana nasubili kwa hamu sana
 
Back
Top Bottom