Ipe jina ulipendalo

Mrs Kharusy

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
1,244
Reaction score
671
Mimi nimeona picha nikajaribu, ni nzuri sana!

Umua unga kama wa mabanzi na uache uumuke kwa nusu saa.

Kwenye sufuria safi chemsha samaki(nguru/jodari au yyt mwenye steki) mchapuze vile upendavyo kwa ndimu ,pili pili, thomu ,tangawizi etc

Akikauka mchambue na ueke pembeni. Kata kitunguu maji km cha sambusa, pili boga na carrot ipare, vikaange kidooogo then mix na samaki vikipoa, add mayonnaise na cheese(mozerella)kiasi upendacho tegemea na wingi wa mchanganyiko wako.

Sukuma donge la unga km chapati then kata kwa glass viduara hadi uishe.

Weka mchanganyiko juu ya viduara na uukunje bila ya kuufunika juu.

Grate mozerella kiasi na utupie juu ya viduara ulivyovifunga
Wacha uumuke na uchome.

Vizuri ukila vikiwa vina uvuguvugu yaani havijapoa!
 
Wapendwa ukishaweka kwenye trey kwa ajili ya kuchoma ipake mayai kwa brush
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…