Iphone effect: Xiaomi Mi11 itauzwa bila charger.


mkuu mbona kama unamhusisha samsung kwenye ujinga wa wengine!!!

samsung ametoa s8 mwenzi march ikiwa na bezzle ndogo kabisa,iphone x ikaja miezi 7 baadae ikiwa na hilo notch,nani alifata trend ya mwenzie hapa.mbali na hilo baada ya notch la x ndio samsung waliponda,wakatoa tear drop,na eject camera.samsung kama android giant hana simu hata moja yenye notch,labda hao wengine.

kama kawaida ya apple,ataleta hayo miaka 2 mbeleni kutokea sasa,na mtashukuru sana na kuona ni ugunduzi ambao haujawahi kutokea[emoji23][emoji23][emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaida ya watu Apple akifanya jambo atapondwa weeeee..... sasa subiri wengine wafuate... utawasikia wakiimba nyimbo za mazingira kama Apple 😀
Xiaomi nisimu nzuri Sana kwangu nazipenda lakini ukitaka na charge unaweza kupata
 
Ujinga wanao wote kwenye smartphone industries. Suala la kuwa na small bezels ni jambo general. Kama kusema kuwa na colored display. Na by the way, sikuzungumzia suala la bezels as a trend, nimezungumzia SABABU ya Apple kuweka Notch. Hakuweka kwa sababu tu ya kuwa na front camera, Notch ya iphone ipo kwa sababu chini yake kuna sensors ambazo zinatumika kwenye Face id. Hio ndio sababu ya wao kumega ile display. Sasa wewe unaziita tear drop, au unaweza ukaita ya Samsung jina utakalo, lakini haiwezi kuondoa fact kwamba imekula sehemu ya kioo ambayo ingetumika kuonesha kitu. Kwaio Iphone na hizo samsung zimemega sehemu ya kioo, call it whatever you want, hizo ni marketing tu kuwafanya mu feel better. Sasa ukitizama utaona kuwa Apple kwa vile ametaka kuweka Sensors hapo mbele, ndio amelazimika kuweka hio Notch kwa sababu hana technology ambayo anaweza kuweka sensors under the display ama within the display without affecting the image/video. Lakini unaweka notch au tuite hio tear drop kwa sababu simply ya Camera tu ambayo nikiitiza could have been squeezed hapo kwenye bezels without kumega display?!

Suala la kuja nalo miaka miwili mbele, lisikutie shaka, kama akija nalo na ikawa na face id huku wengine hawana face id, huoni kama itakuwa ugunduzi tayari? Unafikiri Camera ya kawaida kwenye tear drop na camera yenye sensors za face id itakuwa sawa in terms of advancement?
 
Xiaomi nisimu nzuri Sana kwangu nazipenda lakini ukitaka na charge unaweza kupata
Mleta amejaribu kusema kuwa xiaomi na wao wanato simu bila ya charger, sio kwamba kutakuwa hakuna charger zake, hapana zitakuwepo, ila ukinunua kwenye box hamna, ukanunue au utumie ya zamani, iphone 12 ndio ivo ivo, unaweza kutumia charger za zamani kuichaji na kama huna utaenda kununua dukani, choice is yours, ya tolea jipya au ya zamani, lakini zote zitachaji.

Hizo kampuni zote za simu zinakuja na mbinu za kupiga wateja
 
yeah hapo ni sawa.

kimsingi hiyo notch ni kipande kikubwa sana kulingana na matumizi,na hata hizo camera za samsung bado ni upuuzi flani,zinazingua maana ni kama doa kwenye kioo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kitu walichofanya Apple mwaka huu nikakikubali ni kuachia macbook yenye M1 chip. Nimekuwa najiuliza sana kwanini CPU za kwenye simu ni powerful na low power consumption kuliko za kwenye PC/Laptop na hazitumiki kwenye hizi mashine instead tunawekea kashata za intel, mafeni kama yote na bado perfomance inakuwa sio nzuri. Naona Apple sasa wanaanza ku shape upya Laptop/notebook market huku intel akianza kupata homa
 
yeah hapo ni sawa.

kimsingi hiyo notch ni kipande kikubwa sana kulingana na matumizi,na hata hizo camera za samsung bado ni upuuzi flani,zinazingua maana ni kama doa kwenye kioo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli sijawahi kuifungua iphone yenye hio notch nikaona mpangilio wa hizo sensor, na itabidi niingie youtube nitafute nione. Kwa vile sijaona ilivo ndani siwezi kutoa maoni kama the notch is too big au right size. All i know ni kwamba watu wali expect itakuwa ndogo kuliko matoleo ya nyuma but imeendelea pale pale, kama vile aidha Apple wamekwama kupata njia ya kuipunguza ama ni unyambi tu wakijua watu watanunua na watasahau kuhusu size yake.

Kwa vile saivi makampuni yanataka kuweka display itawali front face yote na wanataka lazima camera iwepo, ni wakati wakafanyia research camera sensors zikawa embeded within the display. Namaanisha mtu ukitaka kupiga selfie, kama vile pixels kadha zinazima na kuachia camera sensors kufanya kazi yake, mimi sio mwanasayansi kujua vipi inawezekana lakini naamini tu inawezekana wakiwekeza fedha 😀
 
Issue kubwa ni compability, Arm ni Risc Haina uwezo wa ku handle complicated things kama cpu za cisc (x86)

Japo siku hizi zinajitahidi ila still zinalag. Mfano encoding/decoding ya video ipo advanced sana kwenye Arm kama x86.

Hata kwenye Rosetta M1 ina perfomance penalty hadi 50%.

Intel na Amd Wana advantage kubwa ya legacy x86 apps. Ambazo mambo yote complicated yanafanyika humo.

Na sasa hivi king wa CPU ni Amd sio Intel, zen 3 (ryzen 5000 series) ni nzuri zaidi kuliko M1 Hali ya kuwa inatumia 7nm manufacturing process, compare na 5nm ya M1.

Na Kuhusu feni cpu nyingi mpya zinaweza kuwa fan less, kote kwa Amd na Intel.
 
Mkuu, naomba ubora wa AMD unaoitofautisha na jamaa zangu Intel
 
Mkuu, naomba ubora wa AMD unaoitofautisha na jamaa zangu Intel
Kwanza Amd hii tunayoizungumzia hapa sio zile ambazo zimezagaa mtaani, ni processor mpya za ryzen.

Ryzen ambayo imeipita Intel ni zile zilizotengenezwa kwa Architecture ya zen 3 na zipo kwenye series ya 5000,

Kuhusu ubora wa zen 3 vs Intel ni karibia kila idara, ya Amd inakula umeme kidogo zaidi, ina perfomance kubwa zaidi kwenye single thread na hata multi thread, hazipati joto sana etc.

Na hili limetokana na Intel kupata matatizo kwenye viwanda vyake, tokea 2015 wanatumia Architecture ile ile.

Sema mwaka huu watazindua cpu mpya za Rocket lake ambazo zinategemewa kumrudisha juu tena.
 
Charger ni Optional. Yaani unaweza ukapewa na charger au bila charger ila bei ni ile ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…