iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1. i phones ni gharama, Hapa sitazungumza sana, nachoomba tu nenda duka linalouza i phones mpya (sio mitumba / refurbished) kaulize bei, Inabidi uwe vizuri kiuchumi tofauti na huku android kuna simu hata za laki kwa wenye bajeti finyu ila pia kuna simu za gharama kuliko hata iPhone kwa wanaojiweza kiuchumi. Hata hivyo bado wapo wasiojiweza kiuchumi wanaolazimisha kununua i phones, kundi hili hununua iphones za bei chee refurbished, wanunuzi wa hizi simu wengi lengo ni kufeki maisha waonekane wapo vizuri kimaisha ila zikija bili hata za elf 50 ni visingizio au kutokomea kusikojulikana.

2. Hakuna tundu la kuingiza earphone hizi zilizozoeleka za pini, hapa hadi ununue vifaa vya ziada, huku android unanunua simu utajua wewe utumie earphones za kawaida au wireless, uchaguzi ni wako.

3. Andaa laini moja tu, kuna matoleo machache sana yasiyozidi matatu yenye laini 2, na bei zake zimechangamka.

4. Kudownload nyimbo hata humu jamiifroums ama mtandaoni ni ishu nzito, inabidi uwe mtundu kidogo wa simu ili kufanikisha hili zoezi.

5. Kuhamisha vitu kutoka kwenye simu kwenda kwenye pc ni shughuli pevu, huku android ukichomeka tu waya unahamisha mafaili kwenye computer, kwa iphone hali ni tofauti kidogo.

6. utapata apps kibao kwa android kuliko iphone, Mbaya zaidi huko iphone apps nyingi inabidi ulipie kila mwezi au baada ya mda flani, Kwa android apps nyingi ni bure na hata kama ni za kulipia unaweza kidownload ambazo zimechakachuliwa na hutalipia hata senti.

7. Unaweza ku root android ukabadili hata os na kuipiga sarakasi simu kadri utakavyopenda , Kwa iphone kuna zoezi la jail break, hapa utaweza tu kufanya baadhi ya vitu ambavyo android vinawezekana tayari hata bila kufanya rooting kama kubadili mwandiko, kuseti ringtone iwe muziki anaotaka, n.k Jail break ni kama mtu aliyefungwa kitambaa machoni kutolewa kitambaa ili aone, rooting ya android ni kama kupewa darubini

8. Hutaweza kusikiliza radio bila bando, kama upo vijijini sehem isiyo na internet fanya utaratibu wa kununua radio.

9. Android utaweza kuback up vitu vyako kwenye memory card, matundu ya memory card hakuna kwenye iphone.

10. unaweza kubadili battery kwa wepesi bila hata kwenda kwa fundi, ukiwa na android, sio zote ila kina simu za android battery inatolewa nanunaweza kuweka nyingine kirahisi, lwa iphone battery yake ipo ndani kwa ndani.

11. Kwenye i phone ku customize vitu kuna vikwazo, mfano ringtone utachagua tu wanazotaka wao iphone na inakuwa sekunde 30 tu, huku android ringtone uutaweka hata ya kingwendu ni wewe

12. kitaa cha notification hakipo kwenye iphone, mfani message ikiingia kama simu ipo silent huku android kataa kanawaka.

13. hutaweza kuseti default app, utaweza kudownload app mbadala ya kufungua mafaili lakini hutaweza kuiseti iwe ya moja kwa moja, kika ukifungua faili litafunguliwa na app ya mwanzoni

14. andoid kuna feauture ya multiple user account, simu inakuwa kama facebook, kila moja ana user name yake na password, naweza kumuazima mtu simu akaitumia bila kujua taarifa zangu na akiniruduishia basi na login kwenye user yangu.

15. Battery kwa iphone ni tatizo, wenzangu wenye i phones wanajiteteaga i phone sio simu ya kutumia tumia kila muda basi naishia kucheka tu napoona wanatembea na power benki simu zao zinapokata moto.

16. Kwenye android unaweza kutumia simu kama remote kwa tv zinazotumia jina kama la simu, mfano ukiwa na tv ya samsung itaweza kutumia simu yako ya samsung kama remote, kwa lg nako pia,n.k....huko kwa iphone utaweza kufanya hivi ila ni kwa tv za apple ambazo ni gharama sana na mimi sijawai kuziona bongo japo zinaweza kuwepo kwa uchache.


17.Watu wengi huwa wanadhani iPhone ndio kinara kwenye kamera, hili si kweli, Kuna simu kibao tu kama xiaoni, google, oneplus 8 zina kamera nzuri zaidi kuliko iPhone yoyote


Wewe mahitaji yako yakiwa ni finyu, lazima uridhike na iPhone yenye features chache, Mimi mahitaji yangu yakiwa mapana, mwenye Iphone huwezi kunielewa nikitaka simu yenye features nyingi


Mapungufu ni mengi ila wacha niishie hapa

kuna ile tendency kwamba ukitumia kitu fulani ambacho ni cha gharama unaonekana tajiri...huo mkumbo ndo unaopelekea mtu fulani kuhisi akimiliki Apple ataonekana class yake ni ya juu...japokuwa watu wengine wanamiliki just kama kitu cha kawaida, wengine wanamiliki kwa sababu ni watu wachache wanamiliki....

Nakumbuka nilikuwa na iPhone 5s kipindi hicho nilikuwa naichaji hata mara 4 kwa siku
 
Tundu la earphones lipi ilo unalolizungumzia? nmeandika huku nachungulia simu yangu😂😂
kuhusu nyimbo tunadownload kirahisi tu mbona audiomack na bolt zipo kwa ajili yetu ayo mengine sawa ila tumeridhika tuu 😂😂😂
 
ukisema haya wanaishia kuja na hoja nyepesi eti tatizo pesa huna.
naishiaga kucheka sana.😀😀
yaani kitu nitolee hela na bado unanilimit kwenye matumizi.
ukiondoa ulinzi iPhone ni simu za kawaida tu.
 
ukisema haya wanaishia kuja na hoja nyepesi eti tatizo pesa huna.
naishiaga kucheka sana.😀😀
yaani kitu nitolee hela na bado unanilimit kwenye matumizi.
ukiondoa ulinzi iPhone ni simu za kawaida tu.
Ishu ya ulinzi labda kwa wenzetu huko ambako watalamu wapo kibao wa kuvunja simu ila kwa hapa bongo IT anachojua sana sana ni ku burn cd na kuweka whatsapp kwa simu sidhani kama ishu ya ulinzi ni serious.

Pia apple imewahi kudukuliwa picha kibao za masupastaa waohifadhi picha zao kwa i phone zilivuja na pia kuna simu ya iphone iliwahi kufunguliwa ndani ya muda mchache tu na mapolisi.

Ila kwa hapa bongo screen lock ukiweka umemaliza mchezo,
 
Back
Top Bottom