iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

1. Kutengeneza simu kubwa sio kwasababu wengine wamefanya hivyo, ni mahitaji ya wakati na wateja.

2. Apple kutofanya tafiti sio kweli, wanafanya nyingi sana tu, hawakimbilii kuweka au kutoa kitu kwa kukurupuka. Wanaangali mahitaji ya wakati. Mfano, leo hii Samsung ana 5G phones, kiuhalisia watu wangapi wanatumia hiyo 5G. Wewe ukiuziwa simu yenye 5G itakusaidia nini? Ila apple hajaweka kwasababu sio muda sahihi kwa sasa, atleast teknolojia ya 5G isambae hasa kwa nchi ambazo zina wateja wake wengi na yeye aanze kuleta simu za 5G.

3. Kutoona vitu vipya sokoni haimaanishi Apple hawafanyi tafiti, kumbuka apple wana ecosystem yao inayojitegemea. Kuweka au kutoa kitu lazima waangalie kutaathiri vipi mwendendo wa vifaa vingine vinavyotegemea. Ndo maana ni nadra sana kukuta simu za apple zina gimmicks kama samsung.

4. Na mfano mzuri ni jinsi apple walivyowekeza kwenye tafiti mpaka sasa camera za iphone ni the best katika industry ya sasa baada ya google pixels. Chips zao zipo efficient kiasi kwamba uwiano wa ukubwa wa battery na ulaji wa chaji unawiana. Unaweza kuta iphone ina 2600 mah inafanya vizuri kuliko samsung yenye 4000 mah.
 
Kauli mniu ya apple imekuwa tutampa mteja kitu kitachotutajirisha potelea mbali na atachokitaka sisi hakituhusu,

Apple katoa tundu la earphone ili apige hela kwenye earphone zake za wireless ambazo anauza hadi laki 6 😁😁 na bidhaa kama adapter zainazounganisha earphone za kawaida ,wateja wake kawaoma ni cash cows.

Simu kama samsung galaxy s10 ni nyembamba zaidi kuliko hata iphone Xs max lakini ina tundu la earphone huku apple wakilazimisha wateja waamini ni kwajili ya space kumbe apple anataka apige mpunga kwenye earphone zake za wireless ambazo anauza hadi laki 6 na huzikuti ukinunua simu hadi ununue wewe mwenyewe.

Hizi earphones tulizozoea ndio nzuri kwasababu hazina haja ya kuchaji na hata ukiwa na buku 10 mtaani unapata nzuri, hizo wireless ni mzigo kwa wengine maana inabidi uchaji simu na earphone nazo uchaji, hivi vitu ni heri angemwachia mteja aamue mwenyewe atumie earphones za kawaida au za kuchaji

Pia sababu ya kizushi ya mimi binafsi kuzikubali earphones za waya ni pale zinapoiokoa hii simu yangu inapondoka, pia kuna siku kibaka alitaka kunichomolea simu mifukoni nlistuka.😁😁
 

1,ndio pont yangu.

2,ni kweli wanaangali ecosystem zaidi(royalty) . lakini si kweli kwamba hawapendi kuleta vipya sokoni. hiyo 5g ya samsung ni kweli ni gimmick(wanaendelea kukurupuka) , kama 3d tech ilivyoonekana ni upupu apple.

3.rejea 2 hapo juu.

4.sehemu kubwa ya hilo ni matokea ya wao kuwa wazalishaji vifaa na watengenizaji wa software, inawafanya kuwa na nafasi nzuri ya kutoa matokeo tunayoyaona. kama isingekuwa android kuvuruga uwanja wa ule wa kujitegemea, tungekumbana na simu zenye uwezo wa ajabu sana. kutana na simu za windows utanielewa nini namaanisha,BB enzi hizo alikuwa na camera kali sana tu sijui angekuwepo leo na OS yake hali ingekuwaje!???
 
Hio net Profit inamsaidiaje mteja ????

Ni sawa na kusifia kanisa unaloabudu lina pesa nyingi wakati wewe muumini hufaidiki na hizo sadaka
 
Sisi tunao tumia Nokia 2700. ngoja tupite tu
 
Mkuu hizo data za kusema camera ya iPhone ndio best umetoa wapi, kwa taarifa yako tu kwenye upande wa kamera iPhone bado anapumuliwa na wajomba wa hii sekta kama kina Xiaomi, one plus one naha hata yuyo google pixels uliyemweka, iPhone anapiga profit kubwa kwa kuwakamua wateja wake kuwauzia bidhaa aizotengenezea gharama ndogo, ni aibu kwa simu kama Xiaomi ambazi faida yake haifikii hata robo ya apple wanazizidi ubora wa kamera simu za iPhone. Apple yeye ni mwendo wa kupiga pesa tu ataweka atachojisikia yeye maana tayari wateja wake ni loyal.

Na hizo statistics za battery umetoa wapi mkuu, au unatype tu unavyojisikia 😁😁
 
Natumia sumsung galax mega 2 tangu 2016.
I phone siwezi nunua pesa yangu labda ya kuokota
 
Haha.

Watu wana adapt kutokana na mazingira.

Hata hizo earphones wanaweza wanakuuzia kwa bei ya earpods za kuongeza bei ya simu.

Earpods ni kuongeza efficiency kwenye kusikiliza muziki na kupunguza usumbufu wa kuweka mawaya masikioni.

Na sasa kuna wireless headphones nyingi kuliko zenye wire. Fuatilia watengeneza earphones na headphones wakubwa duniani.
 
apple anakuja huku bro, soko ni pumbavu sana.mwaka jana mizigo hiyo sokoni. mwaka huu hatujapoa tumepigwa iphone se2. kabla october hatujapewa packege ya kutosha.

ukijifanya premium, watu wanakaba premium mpaka garbage products[emoji38][emoji38].
Iphone SE ni market segment pekee inayojitegemea na wateja wapo. Refer toleo la mwanzo la hiyo model.
 
1. Una hoja za kitoto. Wakuwekee earphone ili usidondoshe simu? How stupid you must be.

2. Ni suala ka wakati, makampuni almost yote yanayotengeneza simu wana earbuds zao. Samsung, Microsoft, Google, Huawei. Muda si mrefu wataondoa headphone jack. Hiyo ndo industry standard kwa sasa kama vile uone flagships zinawekwa 120 hz refresh rate.

Suala la mauzo halithiri chochote maana sio lazima uzinunue.
 
Hio net Profit inamsaidiaje mteja ????

Ni sawa na kusifia kanisa unaloabudu lina pesa nyingi wakati wewe muumini hufaidiki na hizo sadaka
Samsung au Huawei kuuza simu nyingi zinakusaidiaje wewe mteja??
 
Baki na kile unachokiamini.
 
acha uongo ni chache swali samsung s20 haina earphon jack acha kupotosha samsang walifanya majalibio hio kitu wakaona wanakosa soko wakaachana nayo hayo mambo mfyuuuuuuu

#USITUDANGANYE DANGANYA WASIO JUA

Sent using Jamii Forums mobile app
Kajifunze kuandika kwanza mkuu, headphones jack zinatolewa taratibu na zitaondoka completely kama removable batteries zilivyoondoka
 
ni kweli kabisa

mnafurahia utofauti wa mapungufu, sie tunafurahia gepu tulilowapiga
Kwa mtu asiyekwua na shida na masuala ya customization iPhone ataenjoy sana, kwangu mimi ni simu nzuri sana labda kuliko simu yoyote nyingine kwasababu ya ecosystem ya vifaa vya apple, na ios ilivyo operate. Natumia samsung kwa sasa kwasababu kuna personal app inanihtaji nikae nayo muda wote mtengenezaji hajatengeneza app ya ios, na mimi uwa siwezi kuwa na simu mbili yani achilia mbali smartphones hata kuwa na smartphone na kitoch siwezi. Otherwise ios naipenda.
 
Samsung wa na TV inauzwa hadi milion 50, je ni lazima ununue hiyo TV? jibu ni hapna, hata hizo airpads siyo lazima ununue ni option kwa mwenye uwezo na anayependa. Hivi unajua zina ninii cha ziada kuliko wireless earpods nyingine.
1. Zinatambua zikiwa masikioni na zinatambua zisipokuwa masikion, unaset ukizitoa tu masikion kama wasikiliza mziki kwenye simu zinajipause.
2. Ukirudisha masikion mziki waendelea
2. Unaziconnect kwenye icloud hata mtu akiiba asizitumie au zikipotea uweze kuzipata.
3. Zina mziki mzuri sana.
4. Ukizigonga gonga na kidole, mara mbili mziki unachange
5. Ukizgonga zinaconnect na siri
Je bado unazilinganisha na za kawaida?
 
Android hakwepeki 😁😁

Yani umetoka iPhone imekulazimu uje huku android kwasababu develelopera wengi wa app wanaiwezea android.

Ila mkuu jichange hio app yako nahisi ni kutokana na ufinyu wa bajeti ukaweza kutengeneza app kwa android kwasababu developera wapo shazi.

Andaa hata milioni utengenezewe app kwa ios,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…