Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,496
1. Kutengeneza simu kubwa sio kwasababu wengine wamefanya hivyo, ni mahitaji ya wakati na wateja.wenzie wanagombania 40 sababu yeye hawekezi katka research na kutumia pesa nyingi. ndio sababu anakuwa mtu wa kurudia vilivyokwisha fanyika tayari.
halafu swala la kutumia software sio la kuiiba, ni mapatano na makubaliano ya biashara. tokea kampuni inaanzishwa jobs alikiri wazi kwamba,kama unataka kuwa serious kwenye ulimwengu huo tengeneza software na hardware mwenyewe. so kinachofanya apple wasigawe patents kwa wadau ni hiyo woga ya kutoamini ubora wa vifaa kutoka eneo lingine, wakafunga milando ya ofa.
lakini kama ilivyo ada, tech ndio inaamua, leo hii apple wanatengeneza simu kubwa(haukua msimamo wao),wana line mbili(haukua msimamo wao). hatujui mbeleni itakuwaje.
2. Apple kutofanya tafiti sio kweli, wanafanya nyingi sana tu, hawakimbilii kuweka au kutoa kitu kwa kukurupuka. Wanaangali mahitaji ya wakati. Mfano, leo hii Samsung ana 5G phones, kiuhalisia watu wangapi wanatumia hiyo 5G. Wewe ukiuziwa simu yenye 5G itakusaidia nini? Ila apple hajaweka kwasababu sio muda sahihi kwa sasa, atleast teknolojia ya 5G isambae hasa kwa nchi ambazo zina wateja wake wengi na yeye aanze kuleta simu za 5G.
3. Kutoona vitu vipya sokoni haimaanishi Apple hawafanyi tafiti, kumbuka apple wana ecosystem yao inayojitegemea. Kuweka au kutoa kitu lazima waangalie kutaathiri vipi mwendendo wa vifaa vingine vinavyotegemea. Ndo maana ni nadra sana kukuta simu za apple zina gimmicks kama samsung.
4. Na mfano mzuri ni jinsi apple walivyowekeza kwenye tafiti mpaka sasa camera za iphone ni the best katika industry ya sasa baada ya google pixels. Chips zao zipo efficient kiasi kwamba uwiano wa ukubwa wa battery na ulaji wa chaji unawiana. Unaweza kuta iphone ina 2600 mah inafanya vizuri kuliko samsung yenye 4000 mah.