iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

mkuu mimi binafsi huwa namshangaa mtu mwenye mtizamo kama wa kwako.

kusema mtu mwenye tecno ama itel ya 250k, hawezi kununua iphone, ndiko kunafanya wamiliki wa iphone waonekane watu wa hovyo hovyo na wafuata mkumbo,wanaotumia nguvu nyingi na muda kuonekana wako vyema. kumbe maskini si wote, wengine wamefuata ubora, upekee nk.

sababu ni kweli 100% kwamba simu za watoto wengi hizo iphone 6 mpaka 7,kwa uzee wake sasa zimepoteza ubora na kufanya watu wa android hata za bei chee kuona apple si kitu si lolote,hazikai na charge tena, camera zake zimeshapitwa na wakati nk.

hata mtu akikukuta na iphone yako,akaisifia itel yake unatakiwa tu umthibitishie ni kwa jinsi gani ni bora yako kwa itel yake, ukianza mambo ya bei,sijui mara huna hela unaweza ukaaga shindano huku umepanick.
 
Jailbrek checkra1n hizi simu nzinto sana lakin wameanza kufeli ata Kwa protection zao uki Jailbrek unbypass tu aan ndo simpo kabsa wanazingua hawa jamaaa
 

Swala la chaji usisingizie iphone. Simu nyingi zina shida la chaji. Mimi nna iphone x simu yangu inakaa na chaji sana kuliko simu za android nyingi sana. Swala la chaji inategemea na simu . Ziko simu kibao za android betri kimeo. Usijifanye hujui kwamba swala la betri inategemea na simu.
 
ndio ubaya wa iPhone , zinachuja fasta sana

nina jamaa yangu ana sony xperia z ya mwaka 2013, mpaka leo kitu kinagonga kazi.
 
saizi moja haitoshagi kwa wote.

kama umezoea kula ugali robo sahani basi kuna wengine huo ugali wako ni mdogo sana kwao.

hii ndio inapelekea hadi watu wafanye jail break kwenye iphones kwasababu wanataka vya ziada kama vilivyopo tayari huku android.

watu wangekuwa wameridhika kusingekua na haja ya ku jail break.

headphones guku android ushindani ni mkubwa, kampuni ikijidai inaleta za kuleta kututolea ear phone za waya sisi tunahama kwengine, kampuni zipo kibao sio kama huko iphones wateja no kama ndege wa bandani
 
point yako haina nguvu / umeropoka kama vile kila unachojua umefundishwa na mtoto

mtu anaeweza kununua samsung galaxt s10 plus ya milioni 3 kashindwa kununua iphone za milioni 1 ???

watu hatununui vitu kwajili ya bei ama show offs, we do it for demand.

demand = uwezo wa kununua kitu (pesa) + kutaka kununua unachokipenda

rudi darasani isije ikawa ulikula ada kwenda kununua i phone
 
Msaada, kwa anaetumia Android phone ila haina built in radio anafanyaje ili kusikiliza redio? Sio kwa kutumia apps ambazo olazima u-stream na zinatuma data. Ningependa kujua namna ya kusikiliza radio bila kutumia data.
download hii app

FM Radio-7 - Apps on Google Play



Hakuna kiongozi, radio tunazosikiliza hizi ni analogue kwa format yake now days ni online tu no way out kiongozi wala usihangaike stream tu online
nani kakudanganya wewe, endeleeni kutumia bando, sisi hata vijiji visivyo ns=a internet radio si tatizo
 
Iphone ios vs android os
Ipo tofauti kubwa sana kati ya Iphone na simu zingine za android
1: iphone inatengenezwa na kufanya mauzo katika kundi la juu wanahita high end device na ndio maana bei yake ipo juu sana

Android sasa simu zipo kwenye makundi matatu adi manne
Zipo simu za android za high end ,middle,na low ,na nyingine copy

High end device za android ni kama Samsung S series na Note series,
0ne plus
Huawei mate series
Huawei p series
Xiaom note series
Na zingine nyingi

Samsung wanatoa simu vilevile za middle kama A series
Wanatoa na za low kama J series nk

Sasa unapotaka kufanya comparison ya iphone unapaswa ku compare na s series au note price kalibi sawa na specification sawa au zaidi zipo simu za android zinazizidi sana Iphone kwa specification

Simu kama Tecno,itel na nyingine nyingi ni low device class tofauti sana na high end so kufanya comparison na iphone ni vichekesho

2:ios vs android
Program endeshi za iphone imetengemezwa ku run kwenye specific device yao hardware na kila kitu ni compatibility
Android os ikitoka inakwenda kufanyiwa modification kibao na makambuni ya simu ili ziweze kundana na hardware zao hivyo kufanya kuwana bug (error)nyingi iphone yenye ram 1 gb inafanua kazi vizuri kuliko simu ya android yenye ram 3gb hayo ni matatizo ya android
3: android ni free hivyo ina vamiwa ma na matangazo na program ambazo ni sumbufu kweli na kuzifanya simu za android kuwa nzito kupita kiasi hivyo kama mtu yupo serious hataki program sumbufu atachagua iphone ios kuliko android os

4:copyright patent
Mziki na vitu mbalimbali vinalindwa ma sheria,afrika ndio hatujui mambo haya nyimbo watu wanarushiana tu na kudownlod bure ndio maana wengi wabazungumzia kwenye iphone hakuna uhuru
Wanamziki wengi ufanya biashara zaidi na iphone kuliko na android sababu ya copyright management yake ipo juu

5: je iphone hakuna redio ipo ila sio fm inaitwa itune redio ili uipate unatakiwa uwe na apple id ya usa ukiwa na apple id ya Tz iTunes redio upotea
Kwa nini hakuna fm sanabu ni wanahitaji kufanya biashara na kuna app maalumu kwa ajili ya music,movie nk unalipa kwa mwezi hivyo wasanii wao kupata maendeleo leo huku bongo mwamziki ili apate pesa sio kuuza kazi zake sana ila ni kupiga show ila ukifanya kaxi na app za mziki za iphone unalipwa kulimgana na wimbo watu wanavyo nunua

6: utaifa
Kila taifa lenye nguvu lina vitu vyake na kujivunia iphone ni ya usa hivyo inapewa promo sana kila mmalekani ujivunia kutumia iphone

7:usalama
Iphone ni salama zaidi kuliko simu zingine za android

8:kwa nini iphone kuanzia 7 hakuna headphone sababu ni kupinguza matundu ili isipitishe maji

9:sharing berries
Ni vigumu ku share kati ya android na iPhone wana force uwe na ios device ili ni shwala ka biashara sio kwana haliwezekani zilikuwepo simu kama blackberry,lumia zilikuwa na tabia hiyo na sio tu iphone

10:kama unapenda vitu vya free iPhone haikufai ,

Nategemea kumununulia wife iphone kwani simu yake ya android imejaaa matangazo na notifications kama zote ili kumpunguzia makolokolo iphone itamfaa zaidi
Android nayo inauzuri wake hasa ukitumia high end device
 
Spoken like a true sheep.
 
Acha kudharau wabongo..
 
ndio ubaya wa iPhone , zinachuja fasta sana

nina jamaa yangu ana sony xperia z ya mwaka 2013, mpaka leo kitu kinagonga kazi.
Eti iPhone zinachuja sana πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ , nimenunua iPhone 6S mwaka 2016 mpaka sasa nadunda nayo, nilichobadili ni betri tu, mpaka sasa napata support ya software na security patch na baadae nategemea kupata iOS 14, kama zinachuja hebu niambie simu angalau moja tu ya android ya mwaka 2015 inayopata support hadi leo, ukija kwenye perfomance hii iPhone yangu toleo la mwaka 2015 ipo vizuri hata kuliko baadhi ya android toleo la mwaka huu au unazungmzia kuchuja rangi?
 
tecno uongo tumia ata samsung wewe na kuna na ndugu zake tecno wana fanya poa kuliko tecno.. huawei,oppo na infinix
Sasa unaruka mavi unakanyaga mkojo kwani TECNO na INFINIX si tofauti jina tu ila ukichukua mfuniko wa TECNO SPARK 4 ukafunga kwenye INFINIX 8 huwezi jua mpaka uingie kwenye setting
 
kweli kabisa, ziko soo limited na mimi ni mpenzi wa iphone lakini hata cjui nazipendea nini, labda ndo hizo show off ila nna ka samsung pia kurahisha mambo mengine
Zile ndogo hazina 4G mwenye Tecno anaangalia mpira mwenye iPhone anabaki kulalamika tu ni upuuzi mtupu kununua jina
 
Hizo iPhone 6S zimekuwa kama yebo yebo saizi hata kwa laki 3 unapata, iPhone ni simu za Prestige zinapendeza ukiwa na matoleo mapya, Tafuta milioni 2 na nusu ukavute apple kali maana wenzako saizi hawaoni haja ya tundu la earphone za pini kama la kwenye simu yako ya kale πŸ˜‚πŸ˜‚

android ni open source, hata simu za mwaka 2012 zinaweza kuwekewa rom na feauture za latest android system, vitu custom yani kuna community kama xda wanafanya mambo, Huko apple mmepigwa kamba ya mguuni, apple akisusa kuendeleza support basi simu haina maana tena

Hio simu yako ya 6s nayo ipo mbioni kuchinjiwa mbali kama iphone 6 plain, 5c, 5s, 5 plain, 4, 4s, 3, n.k.

Halafu iPhone ni Prestige goods mkuu, hilo kopo tangu mwaka 2016 unalo tu?? Watu wanadunda na iPhone 11 saizi wewe upo na 6, Jichange mkuu, Simu zenyewe milioni 3 tu zinakushindwaje, Au bajeti ni finyu?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Usiige kukaa na simu muda mrefu kwa sisi kina android simu zetu hazichuji
 
Sasa unaruka mavi unakanyaga mkojo kwani TECNO na INFINIX si tofauti jina tu ila ukichukua mfuniko wa TECNO SPARK 4 ukafunga kwenye INFINIX 8 huwezi jua mpaka uingie kwenye setting
Mkuu uzuri wa android huku kuna simu za chini, za kati na za juu flagships.

Kutegemea na uchumi wa mtu anaweza kuchagua wapi panamfaa

Huko apple wana simu za juu tu flagships ambazo ni za kawaida tu hazina vitu vingi, Bila kusahau kuna simu za android ambazo zina bei mbaya kuliko hata hizo iPhones.
 
We jamaa vuta kiti nikupe somk
Nimevuta kiti nikajua unaleta madini
ansroid ni open source, hata simu za mwaka 2012 zinaweza kuwekewa rom za latest android system, vitu custom yani kuna community kama xda wanafanya mambo.
Hii si kwa geeks tu, inakuwaje kwa mtu wa kawaida ambaye hajui hata custom rom ni nini!? Kwenye iPhone inakuja notification ya update na unabonyeza mambo yanajipa
Huko i Phone simu kongwe ambazo zinaendelea bado kupata support ni iphone n6s na 6s plus, hata iPhone 6 plain washaikatia msaada.
At least iPhone 6S ni toleo la mwaka 2015 hadi sasa inapata support, hebu nitajie ni simu gani ya Android toleo la mwaka 2015 ambayo OEM bado anatoa support hadi leo
Hio simu yako ya 6s ni ya kikongwe sana na hivi karibuni wataichinjia mbali kama iphone 6 plain, 5c, 5s, 5 plain, 4, 4s, 3, n.k
Nashukuru kwa kukiri kuwa ni kongwe maana tayari ushasema iphone zinachuja. Hata kama wataichinjia mbali lakini sio kama Android phone zinavyochinjwa mapema, si ajabu hata hiyo simu unayotumia haina support yoyote, imejitahidi sana labda security patches tu,
Nafurahi kutumia iPhone maana kila nikifanya update nahisi nina simu mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…