iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

Kila ki
Kila mtu ananunua sim kutokana na mahitaji yake, na sio watu wote wanahitaji kutumia hizo features, kwa hio sio sawa kusema watu kwa sababu wanatumia aina ile ya sim au wanaendasha gari ile au wanavaa nguo zile, kila mtu na maisha yake na anafanya anachopenda, bila kuvunja sheria.
 
Wakuu kuna simu ya iPhone 11 nimeipata mahali.

Ila ina tatizo la kutokuwa na internet pindi uwekapo line.Je tatizo hapo ni nini...?

Maana nimeangaika nayo sanaaa.

Na hisi na mengine mengi tuu bado shida.

Ila hili lakutokuwa na mnara wa internet imekuwa shida japo line husika inapandisha Bar.

Msaada tafadhali
 
Majority can't afford one. Mid range users aka Tecno wherever.

Huwezi mkuta mtu anaetumia flagship yeyote recent ya android, ukamkuta analalamika hovyo.
 
Majority can't afford one. Mid range users aka Tecno wherever.

Huwezi mkuta mtu anaetumia flagship yeyote recent ya android, ukamkuta analalamika hovyo.

[emoji3][emoji3]
 
iPhone simu gani hata micro sd card huwezi kuweka wewe?

Mimi naunga mkono hoja kwamba hii simu ni fasheni ya urembo.

Na unaruhusiwa kuchagua unachotaka, lakini tukiangalia features objectively, iPhone si simu ambayo power user anaweza kuridhika nayo.
 
Yawezekana ni feki, simu feki kwa hapa bongo zilishafungiwaga network, Ila yawezekana ilikuwa ya huko marekani ilikuwa ni toleo la mtandao flani kwa hio inaingiza tu laini ya mtandao flan
 

Umeongelea mengi lakini nadhani inakuja kwenye ni namna gani hasa wewe mtu unakuwa unatumia iPhone. Kujibu baadhi ya vitu:

3. iPhone zinatengenezwa specifically kwa ajili ya soko fulani; Africa ndio tupo katika kuhangaika na line mbili lakini nado hakujawa na iPhone ambayo imekuwa developed for African market. Marekani na Ulaya hawatumii sana mambo y line mbili ndio maana utaona hata Androids katika masoko hayo asilimi kubwa ni line moja.

4. Suala la kudownload nyimbo ni rahisi tu kama unatumia Music app... sema ni kwa subscription; na since sisi Watanzania tunapenda mno vitu ambavyo hatulipii basi ndio tunaona ni tabu. [emoji4]

5. Inategemea na unaongelea vipi shughuli pevu kuhamisha vitu, mimi natumia iPhone, Macbook na iPad na hivi vyote kwanza viko synchronized na pili naweza hamisha vitu urahisi sana kwa AirDrop (I hope unafahamu hii inafanyaje kazi).

6. Wingi wa App na uhitaji wa App fulani ni vitu viwili tofauti; kwangu mimi App zote ambazo nahitaji kuzitumia katika iPhone zipo (sema kuna tendency ya hawa App Developers ambao hawataki kulipia ile fee associated na kuweka App kwenye Appstore wanaona ni bora wabaki na kuwa na App kwenye Android tu).

7. Unaweza set ringtone unayotaka ingawa namna ya kuset sio moja kwa moja kama Android; lakini huitaji jailbreak iphone yako kufanya hivyo.

9. iPhone unaweza backup vitu vyako kirahisi kabisa kwenye iCloud au hata PC. Kama hutumii Macbook then unahitaji kuwa na iTunes on Windows PC kuwezafanya yote kirahisi. Piakama una vifaa sahihi ni rahisi sana kubadili battery au display ya iPhone.

PS: Nadhani unaongelea Android zenye mfuniko wa betri na hujawahi jaribu badili battery kwenye simu kama Blackberry Motion.

10. Nimelijibu kwenye jibu la 7

11. Katika setting unaweza weka ukawa unapata notification message zikiingia kwa mwanga kutoka kwenye flash. Inakuwa inawaka. [emoji4]

12. Unaweza set default app kwa mafile unayofungua. Kama ni .pdf au .pptx ama .xlxs.

14. Inategemea ni iPhone ipi unatumia. Ninaweza kaa na simu yangu ikiwa katika matumizi makubwa kwa mpaka masaa 18 kama nikitoka nyumbani ikiwa katika asilimia 100.

16. Mimi naamini iPhone ndio ina kamera nzuri zaidi. The fact kwamba umekusanya android zote kuzifananisha na simu moja inaongea zaidi.

Kuna vitu vingi sana hujaongelea kama security na durability to say the least. Lakini ni uchambuzi mzuri.
 
Kilichojaa kwenye huu uzi ni Uswahili na Inferiority Complex tu. Kila mtu ananunua na kutumia kitu kwa mahitaji pamoja na utashi wake. Na kuna vitu ambavyo wewe unaona muhimu kwa mwingine siyo na wala si kipaumbele kwake. Mimi naweza kuwa natumia I phone 5s au Samsungu S3 na isiwe tatizo kwangu kutegemea na matumizi yangu ya simu. Mwingine anaona fahari tu kuwa na latest Phone bila kujali matumizi. Maisha ni rahisi sana sema wanadamu tunayacomplicate mnooo.
 

hivi kuna watu mnatumia memory cards mpk leo heee!!!
 
hivi kuna watu mnatumia memory cards mpk leo heee!!!
Watu wanatumia tapes kwenye LTO drives, na model mpya zinatoka mpaka kesho, na wanaulizia capacity ya tapes mpya ni ipi, nini memory cards.

Tusitumie kwa sababu gani?

Nyie ndiyo watu mkiambiwa kuna watu wana data za terabyte 800 wanakimbiza petabyte mnashangaa.

Hatuna historia sawa, hatuna matakwa sawa, hatuna use cases sawa, hatuna appetite sawa.

Hatuna philosophical outlook on life sawa.

Wewe mahitaji yako yakiwa ni finyu, lazima uridhike na simu yenye features finyu.

Mimi mahitaji yangu yakiwa mapana, huwezi kunielewa nikitaka simu yenye features nyingi.

Huwezi kunielewa.Unavyofikiri wewe na ninavyofikiri mimi ni namna mbili tofauti.

Kwenye suala la features, kukosa memory card support kwa iPhone kunaifanya iPhone kuwa simu nyanya mbele ya simu zinazo support card.
 
Mimi situmii iphone na sina mpango wa kununua hiz simu kama nipo ndani ya nchi mfano wa Tanzania au nchi maskini zaidi ya Tanzania, lakini iphone ni moja ya simu zenye features zinazotakiwa kwa dunia5ya Leo.
Tunachoashindwa kujua ni kwamba Dunia hipo mbali sana kiteknolojia na internet ndiyo kila kitu ndiyo maana iphone wanahitaji internet connections hata kama radio, wenzetu nchi za mbele internet siyo tatizo .

Kwa maandaleo ya technology sasa vitu kama earphone za pin/wire, memory card, slot za kuweka sim kadi zaidi ya moja kwenye simu, mambo haya yanafikia mwisho zimebaki nchi ambazo hazijapiga hatua kiteknolojia.

Nina mengi ila muda unanibana kuandika, lakin iphone ni simu ambazo wewe na Mimi tulio ktk maandaleo finyu ya technology siyo walengwa rasmi.
Tambua features za iphone ndizo zinazo takiwa kwa Dunia ya Leo, hasa ukizingatia uharifu sasa unahamia ktk mitandao.

Kwa nchi ambazo hazijapiga hatua kiteknolojia simu kama Samsung, nokia ndiyo type yetu kwa wale wapenda simu za cheap simu kama techno na infinix zinatosha.
 
matumizi ya micro card ni yapi?

Umetengenezewa simu ina storage 500GB una pc ina 500GB una external ina 1TB hizo zote unatafuta micro card ya nini? maonesho? Kuwa serious na vitu unavyojadili
 
iPhone ni za hovyo sana...sema wamiliki wakishaibiwa wanashindwa kubadilisha ili wasionekane wamechoka...mimi binafsi sijaielewa kabisa hata nikipewaga kama zawadi nami naigawa
😂Uko sahihi kuna watu hadi leo wanatafuta microsoft/window phone na wengine wanatafuta blackberry maana ndizo wanazozielewa hivyo uko sawa kabisa kuipenda android ndo hivyo hivyo wenzio wanazipenda iPhone.

Swali langu ni kwa nini wanaolalamika kuhusu iPhone ni wale ambao sio watumiaji?
 
Me nahisi android user wanajaribu kulazimisha iOS user wahame kutoka kile kitu wanakipenda.

Pia kuna watu hawataki kutumia android sio kwamba hawawezi kununua au hawajawahi kuzitumia ila wameona iPhone ndo pendeleo lao hivyo ni bora watu waache kuaminishana kile wanachokipenda wao ndo kipendwe na watu wengine.
 
iPhone ni za hovyo sana...sema wamiliki wakishaibiwa wanashindwa kubadilisha ili wasionekane wamechoka...mimi binafsi sijaielewa kabisa hata nikipewaga kama zawadi nami naigawa
😂Binafisi blackberry na ile os yake au microsoft/window phone zikirudi naweza hamia huko lakini sio operating system ya android
 
Watumiaji wa iPhone mara nyingi ni malimbukeni...huwa wanajisikia sana kwamba wapo daraja la juu.....mimi ninakaa na mtu anayetumia iPhone huwa ananisumbua sana Apps nyingi hawezi kudownload kwake
Taja hata apps mbili ambazo haziko iphone ziko android
 
matumizi ya micro card ni yapi?

Umetengenezewa simu ina storage 500GB una pc ina 500GB una external ina 1TB hizo zote unatafuta micro card ya nini? maonesho? Kuwa serious na vitu unavyojadili
Kwako unaweza usione umuhimu.

Kwa sababu labda huna 800 terabytes za data kama mimi. Ambazo kabla ya robo ya kwanza ya 2021 zitafika petabyte.

That is, 1024 terabytes, or a million gigabytes.

Kama hatuna data sawa, hatuwezi kuwa na mahitaji sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…