Kila ki
Kila mtu ananunua sim kutokana na mahitaji yake, na sio watu wote wanahitaji kutumia hizo features, kwa hio sio sawa kusema watu kwa sababu wanatumia aina ile ya sim au wanaendasha gari ile au wanavaa nguo zile, kila mtu na maisha yake na anafanya anachopenda, bila kuvunja sheria.1. i phones ni gharama, Hapa sitazungumza sana, nachoomba tu nenda duka linalouza i phones mpya (sio mitumba / refurbished) kaulize bei, Inabidi uwe vizuri kiuchumi tofauti na huku android kuna simu hata za laki kwa wenye bajeti finyu ila pia kuna simu za gharama kuliko hata iPhone kwa wanaojiweza kiuchumi. Hata hivyo bado wapo wasiojiweza kiuchumi wanaolazimisha kununua i phones, kundi hili hununua simu hizi kwa lengo la kufeki maisha waonekane wapo vizuri kimaisha.
3. Hakuna tundu la kuingiza earphone hizi zilizozoeleka za pini, hapa hadi ununue vifaa vya ziada, huku android ukinunua ear phone unaitumia hapo hapo
3. Andaa laini moja tu, kuna matoleo machache sana yenye laini 2.
4. Kudownload nyimbo hata humu jamiifroums ama mtandaoni ni ishu nzito
5. Kuhamisha vitu kutoka kwenye simu kwenda kwenye pc ni shughuli pevu.
6. Apps kibao zipo android kuliko iphone
7. Unaweza ku root android ukabadili hata os na kuipiga sarakasi simu kadri utakavyopenda , Kwa iphone kuna zoezi la jail break, hapa utaweza tu kufanya baadhi ya vitu ambavyo android vinawezekana tayari hata bila kufanya rooting kama kubadili mwandiko, kuseti ringtone iwe muziki anaotaka, n.k Jail break ni kama mtu aliyefungwa kitambaa machoni kutolewa kitambaa ili aone, rooting ya android ni kama kupewa darubini
8. Hutaweza kusikiliza radio bila bando, kama upo vijijini sehem isiyo na internet fanya utaratibu wa kununua radio.
9. Android utaweza kuback up vitu vyako kwenye memory card na pia unaweza kubadili battery kwa wepesi bila hata kwenda kwa fundi, lwa iphone hizi feautures sahau.
10. Kwenye i phone ku customize vitu kuna vikwazo, mfano ringtone utachagua tu wanazotaka wao iphone na inakuwa sekunde 30 tu, huku android ringtone uutaweka hata ya kingwendu ni wewe
11. kitaa cha notification hakipo kwenye iphone, mfani message ikiingia kama simu ipo silent huku android kataa kanawaka.
12. hutaweza kuseti default app, utaweza kudownload app mbadala ya kufungua mafaili lakini hutaweza kuiseti iwe ya moja kwa moja, kika ukifungua faili litafunguliwa na app ya mwanzoni
13. andoid kuna feauture ya multiple user account, simu inakuwa kama facebook, kila moja ana user name yake na password, naweza kumuazima mtu simu akaitumia bila kujua taarifa zangu na akiniruduishia basi na login kwenye user yangu.
14. Battery kwa iphone ni tatizo, wenzangu wenye i phones wanajiteteaga i phone sio simu ya kutumia tumia kila muda basi naishia kucheka tu napoona wanatembea na power benki simu zao zinapokata moto.
15. Kwenye android unaweza kutumia simu kama remote kwa vifaa kama samsung, lg ,n.k....huko kwa apple so rahisi labda kwa tv zao za apple tv
16.Watu wengi huwa wanadhani iPhone ndio kinara kwenye kamera, hili si kweli, Kuna simu kibao tu kama xiaoni, google, oneplus 8 zina kamera nzuri zaidi kuliko iPhone yoyote
Mapungufu ni mengi ila wacha niishie hapa