Mkuu. Naomba kukurekebisha kwa mambo machache na uchache huu ukawe mwingi kwako. Natumai kama ni mtu wa kujifunza utapata somo kubwa sana. Tambua kwamba kabla iphone hajaingia sokoni kulikua na makampuni tycoon ambao pia walikua sokoni na walikua wanafanya vizuri na bei zao zilikua sio za kitoto. Naomba nikujibu point zako moja baada ya nyingine kama ifuatavyo
1)Kusema iphone ni gharama naomba nikupinge kwa ukali sana. Kwenye sim unatakiwa ujue kuna matabaka ama niseme grades. Kuna Flagship, kuna midrange na budget smartphone. Zunguka dunia nzima ni ngumu sana kukuta Flagship inauzwa hizo bei unazosema za laki nakitu.
Tizama kielelzo cha picha hapa chini
View attachment 1634975
View attachment 1634976
Ukitazama hapo ni iPhone 11Pro Max ya mwaka 2019 na samsung s20Ultra ya mwaka huo huo. Ukitazama kwa UK sim hizo zinauzwa bei sawa kabisa, ukija Marekani, Samsung ni ghali zaidi, ukirudi india sim hio iPhone inauzwa ghali zaidi ya samsung.
Hii inatokana na facts na variable nyingi sana ila trend ni hio. Tizama sim nyingi sana za Android huwa Ghali mwanzo ila miezi baadae zinapungua value pakubwa sana, kinachokufanya uone iphone ni ghali ni sababu market value yake inabaki juu kwa muda mrefu. Mtu mwenye laki nne ni ngumu kumuelewesha kwamba iphone 7/7Plus simu iliotoka mwaka 2016 mpaka leo bado hawezi ipata mpya kwa bei hio atasema ni expensive.
2) Ni ajabu sana mpaka mwaka 2020 bado unashangaa kutokua na tundu la earphone. Hili swala walilalama sana watu 2016 na leo hii ndo trend. Kila sim inayojielewa inaelekea huko.
View attachment 1634985
Hii ni Samsung Galaxy Note 20 ultra. Nioneshe tundu la headphone hapo. Japo wameweza kuweka tundu lote hilo kubwa la S-Pen ila wameignore kabisa earphone. Kubali ukatae hio ni technologia inayokufa taratibu.
3) Mkuu tatizo tupo dunia ya tatu ndo maana unapata tabu kidogo kuelewa na unahisi kwamba kuna tatizo mahala. Kumbuka iphone yuko many steps ahead. Dunia saivi inaelekea kwenye virtual /E-Sim. Inaachana kabisa na mambo ya physical sim. Kama umeona kwanzia iphone Xs- latest zinakua na dual sim. Sasa ziko za dual physical sim ambazo ni HK version na ziko ambazo dual sim yake ni E-Sim (Electronic Sim)
View attachment 1634996
Hii huhitaji kuwa na line. Kwa wenzetu unaenda Kampuni yako ya mtandao wanakupa QR code unascan unapata line ndani ya sim yako. Tanzania tutafika huku ila sijui lini. TCRA walitazame hili.
4) Kumbuka kwamba kuna kitu kinaitwa loyalty. Kwako wewe mtumiaji unaweza ona umebanwa kudownload miziki ila kumbuka illegal download ni kosa kisheria na unaweza fungwa. Lakini pia kwa wasanii hii inawasaidia wao kuboost digital sales zao. Hii ni mbinu ambayo tunakoelekea itakua implemented in most platforms. Imagine wewe kama unauza duka la mangi tuseme (alafu kuna namna 50% ya watu wanaweza kuchukua bidhaa zako bila wewe kunufaika, hio imekaa vipi?)
5)sijaelewa unaamanisha nini kusema shughuli pevu. Nadhani swala la security basi kwako ni dogo sana. Unafahamu kwamba sim nyingi za Android kwa kuwa na option ya Debugging mode, mtu anaweza tengeneza sim virtual kwenye computer alafu akachukua sim yako na akaipaste kila kitu kwenye computer hio virtual na kuwa na uwezo wa kuona kila kilichopo kwenye sim yako. Je hicho ndicho unachotaka? Mimi nimetumia iphone tangu mwaka 2007 na android pia nimetumia. Sijawai ona hio shughuli pevu unayoisema wewe labda unieleweshe.
6)Naomba nikusahihishe hapa. Na nikutume ukafanye tena research. Ichi unachozungumzia kilikua kweli 2016 kurudi nyuma. Sasaivi tizama kampuni nyingi kubwa za apps, kuna hata tweaks au niseme vionjo ambavyo vinawekwa kwenye iphones tuu. Kuna apps ambazo huanza na kuingia kwenye iphones kwanza kabla ya android “mfano hai games kama Fortunite” pia application kama instagram na whatsapp na snapchat zinafanya vizuri sana kwenye iphone sababu kila iphone inapata a tailor made app. Mfano mwaka huu 2020 zimetoka iphone nne zenye ukubwa tofauti wa screen iphone seii, iphone 12mini, iphone 12/12pro na iphone 12Pro Max, ni rahisi kwa izi application kutengenezea kila sim application iliokua edited special for hio sim. Ila kwa android sababu ni soko zima la sim zaidi ya 500 tofauti tofauti basi inatengenezwa one app fits all ndo unaona kunakua na mvutano wa picha na video.
7) SECURITY IS KEY FEATURE KWENYE SIM NDO MAANA NILIKUAMBIA MWANZO WEWE KUA NA UWEZO WA KUGARAGAZA SIM YAKO KUMBUKA UNAWAPA UWEZO HUO HUO WATU WASIO NA NIA NZURI NA WEWE
8)nataka uchukue samsung Flagship yeyote ya latest toka 2018-2020 alafu sikiliza nayo offline radio alafu njoo tena hapa leta argument. Again iphone wapo mbele technological. Vitu wanavotoa na kuviacha wengine hufuata muda mfupi badae.
9)Mkuu naanza kuamini kwamba kuna uwezekano hii kitu umecopy paste mahala ukabadili lugha na hii ilikua post ya 2016 kurudi nyuma.
View attachment 1635005
Hii ni Note 20Ultra. Kubadili battery kwenye hii sim ni mtihani and so is many Androids. By standards iphone ni moja kati ya sim rahisi sana kubadili battery tofauti na hizo android zako.
Kwenye swala la storage na kuback up sim kwenye memory card, nikurudishe tena SECURITY
10) Kama kitu hujui sema sijui, ukiskia mtu kasema kitu flani hakiwezekani embu fanya research kwanza kuliko wewe nawe kuruka kwamba haiwezekani.
View attachment 1635006
Hii ni sim yangu na utaona nina Ringtone ya Ratvanny naogopa. Sasa wewe sijui uliona wapi kwamba haiwezekani.
11) Again technology inapoenda taa zinatoka. Na kuna option kwenye iphone ya kuset flash light ikuallert.
12)Tena narudia kama hujacopy paste hii kitu kutoka mwaka 2016 basi hujawai tumia iphone ama hujafanya research. Default apps unaweka vizuri tuu.
View attachment 1635014
Email zangu zote nafungua kwa Gmail app, Safari ndo Default browser nilioweka. Kuweza kuset hivi nenda settings alafu app unayotaka mfano Google Chrome alafu utapata option ya make this Default browser.
13) SECURITY. Kasome kuhusu uwezo wa ADB na SDK alafu hutathubutu tena kulog in kizembe zembe kwenye sim za watu.
14)[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hao wenzako wanatumia iphone gani boss? Na hizo Powerbank wanatembea na powerbank gani? Naomba nikupe mfano, mtu mwenye iphone 11Pro Max anauwezo wa kukaa na chaji kwenye sim yake kwanzia saa moja asubuhi mpaka saa tisa mchana. Thats a fact. Iphone huonekana ina battery ndogo ila hakuna sim yenye optimization kama iphone, ukizingatia na kuwa na ABionic Chips basi hii inawapa mileage kubwa zaidi tofauti na sim ambazo zinatumia 3rd part chipsets.
View attachment 1635022
Utaona hapo tofauti ya iphone na zingine ni ndogo sana and by 2020 standards, still promising.
15)ECO SYSTEM MKUU ndo maana unaona hata kwenye sim tu skuizi app zinataka ubaki kwneye app zao. Unafungua link inafunguka in app built browser kukuweka built in. And thats what apple is doing. Ndo maana as a company wanazidi kua successful.
16)Hili linaweza kuwa na ukweli kwa asilimia kadhaa but as research shows, video zinazochukuliwa kwenye iphone zinakua more stable na vivid kuliko on anyother smartphone. Nikutume ukaangalie iphone big event wakati wanazindua hizi 12lineup utaona jinsi gani wamechange game la camera kwenye sim.
Nimechukua muda kidogo kukuandalia makala hii natumai utaisoma kwa upana na utaelewa sana.
0786371107 kama kuna ziada.