Naomba kuuliza jamii check maana Kuna hoja kwamba hii kampuni ya iphone imbayo inasifika kwa kamera nzuri hizo kamera Huwa wananunua kwa kampuni ya Samsung
Hivo naomba uthibitisho wa Hilo Ili tujue kama tunapigwa au laah?
Hivo naomba uthibitisho wa Hilo Ili tujue kama tunapigwa au laah?
- Tunachokijua
- Iphone ni aina ya simu inayotumia programu tumishi ya IOS, simu hizi zimekuwa gumzo sana kutokana na utaratibu wake wa kutoa matoleo mapya mara kwa mara tangu ilipoanzishwa, kwa wakati huu watumiaji wa simu hizo wanasubiri toleo jipya la iphone 17.
Miongoni mwa sifa za simu ya iphone ni uwezo wa Camera jambo ambalo limekuwa kiliteta mjadala camera zao wani
Mdau amehitaji kufahamu iwapo simu za Iphone wanatoa Camera zao kwa kampuni ya samsung ambao nao pia huzalisha simu aina ya samsung zenye programu tumishi ya android.
Taarifa zimekuwa zikieleza kuwa kampuni ya simu ya Iphone imekuwa ikiainisha muuondo wa camera za simu wanazozitaka kisha wanatengenezewa na wazabuni wao.
Vyanzo vinaonesha kwa muda mrefu iPhone wamekuwa wakitumia lenzi za kamera zao kutoka kwa kampuni tofauti tofauti ambazo ni Largan Precisioon kutokea Taiwan, Genius electronics optical na Sunny Optical kutokea China.
Na kwa upande wa sensori za kamera za kwenye simu za Iphone (Camera Sensors) inaelezwa kuwa hizi wanazinunua kwa kampuni ya Samsung. Sensori kwenye camera hufanya kazi ya kuchukua mwanga na kuugeuza kuwa katika mfumo wa umeme ambao unatengeneza picha unayoina kwenye simu yako, sensori ya kamera inaweza na kufananishwa retina kwenye jicho.
Lakini pia zipo taarifa zinazoeleza kuwa kampuni ya Iphone inatarajia kushirikiana na kutumia sensori za kamera kutoka kwa kampuni ya Samsung zenye ukubwa wa Megapixel 48 kuanzia mwaka 2026 na hivyo kuachana na Sony washirika wao wa muda mrefu.