iPhone yapoteza nafasi ya kuwa simu namba 1 China. Watu wengi wanahamia Huawei

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
China kulikua na Iphone nyingi kuliko nchi yoyote Duniani ila sasa Iphone inapoteza nafasi ya kua simu namba moja China.
Watumiaji wengi wa Iphone wanahamia Huawei, Iphone inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa makampuni ya China kama Huawei, One Plus, Oppo, Honor, TCL, ZTE na kadhalika.

Wengi walioulizwa kwa nini wanahamia Huawei walidai Iphone bei ghali halafu inakosa vitu vingi ambavyo vinapatikana kwenye simu nyingine kama fast charging, multiple cameras na kadhalika.

Wachina naona wameamua kuwekeza kwao.

Apple is no longer China’s biggest smartphone brand
 
gharama za huawei pia ni kubwa jaribu kuuliza p40 pro bei ni kama iphone tu.
 
Mbona zaidi ya miaka 5 sasa iphone haina mauzo makubwa china?
Nadhani sasa Apple wanahamia India. India ina soko kubwa sana ambalo limeachwa muda mrefu bila kutumika.

Naona big tech companies sasa ndio zinaipa macho India, Google, Apple, Amazon na nyingine zimetangaza kuanza kuwekeza India.

India pia imetengeneza mazingira ya kuvutia wawekezaji wakubwa, kuwapa tax credit and incentives, pia China gharama za ajira zimepanda sana hivyo macho ya watu yako India.
 
Apple hawezi kufanikiwa India unless aanze kutoa bidhaa za Bei rahisi, average smartphone price India ni $159, hao ni kama sisi tu watu wengi simu zao ni za Around laki 3.

Hao wanaokwenda kuwekeza wanatafuta tu Cheap labour, then vifaa vitauzwa nchi nyengine.
 
I

Ila mkuu hata China, purchasing power yao haina tofauti na ya wahindi.
 
Unaweza ukaangalia hapa mkuu
List of Chinese administrative divisions by GDP per capita - Wikipedia

China wana Income inequality kubwa sana, kuna eneo la East ambapo ndio mambo Ya It yalipo GDP per capita ni Zaidi ya dola 20,000 wana Income kama Nchi nyengine tu za Ulaya.

Then kuna Majimbo mengine yana masikini wa Kutosha tu, per capita hadi dola 4000,

Hivyo hao Wa east wanaweza Ku afford vitu vya Gharama.

India wao ni kama Sisi wana project za kujenga vyoo bado
 
Sahihi mkuu,majimbo kama Beijing, Shanghai, Macao, Hong Kong hao per capita ni Dollar 50,000 kwa mwaka.

Hadi inachekesha, Tanzania watu wa masaki tu ndio wamefikisha per capita income ya $1,030 tumeunganishwa watanzania wote kua tumefikia uchumi wa kati wa $1,030.

Kule kijijini kwetu watu wana per capital income ya $200 kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom