iPhone za Makumbusho zina nini?

Thread Starter

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2017
Posts
1,378
Reaction score
1,045
Habari zenu wanazengo, naombeni kupata ufafanuzi kidogo kuhusu iPhone zinazouzwa madukani makumbusho dar...nilikuwa nataka kununua ila nikafanya utafiti kidogo wengi wakaniambia nenda makumbusho

Ila kabla sijaenda nikatonywa na fundi wang wa simu akasema usiende kule watakupa simu feki, mara wengine wanasema second hand, mara refurbished, mara hazidumu kwa sababu sio orijino.

naombeni mnisaidie jaman nijue kiundani zaidi kama kuna aliyewah kununua na kujua mapunguf ya hzo simu..na pia mnielekeze sehem wanazouza hizi simu original kwa bei ya kawaida maana ni ndoto yangu na mimi kumiliki iphon... iphone 5,5s au 6 zenye storage ya 16 had 64

sijaandika huu uzi kwa lengo la kuharibu biashar ya watu,

nisamehe kwa mwandiko wang kama utawakera
 
Nenda Mlimani City zipo original sema Bei zake zimesimama sana zipo kuanzia iPhone 6 na Bei wamepunguza ni Tshs 750,000 Hawana izi za plus
Safari njema na karibu katika dunia ya iPhone
 
Uzi umekaa kichawi Sana huu, sasa kama wamekuelekeza zinakopatikana original kwa usiende kununua huko.

iPhone nyingi zinazouzwa bongo ni usied ila sio feki.

Acheni kuharibu biashara za watu walizogharamia kuzitangaza.
 
Nenda Mlimani City zipo original sema Bei zake zimesimama sana zipo kuanzia iPhone 6 na Bei wamepunguza ni Tshs 750,000 Hawana izi za plus
Safari njema na karibu katika dunia ya iPhone
Iphone 6, 750k ndio wamepunguza? Wafanye hata 500k bana..
 
Uzi umekaa kichawi Sana huu, sasa kama wamekuelekeza zinakopatikana original kwa usiende kununua huko.

iPhone nyingi zinazouzwa bongo ni usied ila sio feki.

Acheni kuharibu biashara za watu walizogharamia kuzitangaza.
mkuu nimesema sina lengo la kuharub biashara ya mutu
 
Makumbusho huko ni refurbished,,mixer second hand..kingine hakuna iPhone fake

Nenda Apple store Mlimani City,bei zimechangamka kuliko kawaida..wewe si umesema unataka original??,,sogea hapo
zimechangamka kvp ntajie mfano mkuu
 
Nenda Mlimani City zipo original sema Bei zake zimesimama sana zipo kuanzia iPhone 6 na Bei wamepunguza ni Tshs 750,000 Hawana izi za plus
Safari njema na karibu katika dunia ya iPhone
750,000 kwa maisha haya ya baba jeska ntaweza kweli, bajet yang haifik huko bosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…