Ipi bora kati ya Diploma ya Sheria ya Chuo cha LUSHOTO na Diploma ya Biashara CBE Dodoma?

Ipi bora kati ya Diploma ya Sheria ya Chuo cha LUSHOTO na Diploma ya Biashara CBE Dodoma?

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,810
Reaction score
6,599
Wadau, kuna kijana kachaguliwa kusoma Diploma Sheria ya Chuo cha Lushoto na pia kachagulia Diploma ya biashar aCBE Dodoma, kwa wazoefu wa hizo anga na maisha ya Kitanzania unamshauri wapi labda. Bahati mbaya siyo mjuzi wa hizo fani ukiachana na herasay
 
Wadau, kunakinyana kachaguliwa kusoma diploma sheria ya chuo ch Lushoto n pia kachagulia Diploma ya biashar CBE DODOM, kwa wazoefu wa hizo anga na maisha ya Kitanzania unamshauri wapi labda. Baati mbaya siyo mjuzi wa hizo fani ukiachana na herasay
Duuh. Achana na Shisha ndugu
 
Nashauri aende IJA akasome hiyo diploma ya sheria ila asiishie hapo akatafute na digrii kisha aende Law school ni jambo la miaka mi 5 au 6 tu itategemea digrii atasoma chuo gani sababu kuna digrii kwa miaka 3 na kwa miaka 4.

Faida zake:

- Akifanikiwa kufika na kufaulu Law school atakuwa na uwanja mkubwa kujiajiri.

- Akiamua kutaka kuajiriwa hasa serikalini diploma ya IJA itambeba sana ajira za mahakama

- Ataweza kuwa msaada mkubwa kwenye maswala ya kisheria kwenye familia/ukoo. Wanasheria ni muhimu sana kwenye familia.

Mambo ya fani za biashara sizijui sana ila naamini haziwezi kuifikia fani ya sheria kwenye hizo nyanja hapo juu kuanzia kujiajiri, ajira na kutegemewa. Nikisema kujiajiri na maanisha kujiajiri ndani ya fani husika sio kufanya biashara sababu hata bila kwenda shule mtu anaweza fanya biashara tu.
 
Back
Top Bottom