HOJA Ipi hatma ya fedha za Basket Fund(HSBF) kwa vituo vya kutolea huduma za Afya?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Fedha za basket fund ambazo huwa zinaingizwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kila baada ya robo mwaka haijaingia tangu mwezi disemba 2025.

Hii imepelekea changamoto ya uendeshaji wa vituo hivi vya Afya kwani fedha hizi hutumika kununua dawa na vifaa tiba, kulipa bili za umeme na maji, kulipa watumishi wa mkataba, shughuli mbalimbali zauendeshaji pamoja na stahiki mbalimbali za watumishi.

Tunaomba serikali itoe majibu juu ya changamoto hii ikizingatiwa mwaka wa fedha wa serikali umeshaisha
 
Mnashauriwa kupambana na User fee. Pesa za wafadhili zinakwenda kukata.
Wekeni mikakati yenu kupitia User fee zaidi kuliko HSBF.
Itakuwa changamoto kwasasa ila hakuna budi kujiandaa na hilo.
 
Mnashauriwa kupambana na User fee. Pesa za wafadhili zinakwenda kukata.
Wekeni mikakati yenu kupitia User fee zaidi kuliko HSBF.
Itakuwa changamoto kwasasa ila hakuna budi kujiandaa na hilo.
User fee ndio pesa ambazo mwananchi analipa hospitali.
 
Hawana Hela hawaa, Mzungu kujitoa, kumeacha boooonge la gap ambalo Serikali ndio ilikua inalitumia kama HSBF .

Zaman Serikali haikutumbukiza Pesa kwenye miradi ya Ukimw, Malaria, TB, Chanjo, n.k hivo Pesa hiyo ilitumwa HSBF.

Kwa sasa Serikali inalazimika kuwekeza Pesa zake kwenye hiyo miradi Hali inayolazim ukosefu wa HSBF.




Cha msingi, hii NCHI ni Tajiri, wakati mnalialia hivo, yupo Kijana baada ya kupewa uwaziri tu ana Magari ya kifahari zaidi ya Manne, anahonga madem Magari ....


Hapo kituoni hapo ulipo, wewe angalia cha kusepa nacho wakati huo tuungane kuipiga vita CCM
 
Hahahahaa
 
Mnashauriwa kupambana na User fee. Pesa za wafadhili zinakwenda kukata.
Wekeni mikakati yenu kupitia User fee zaidi kuliko HSBF.
Itakuwa changamoto kwasasa ila hakuna budi kujiandaa na hilo.
Wakati huohuo serikali inajisifu kutibu bure watoto under 5, wajawazito, wazee, wenye magonjwa sugu na majeruhi wa ajali..
 
Ni jamaa yangu ananiambi vituo huko mawilayani zina hali mbaya sana. Hii ndiyo hasara ya kuwa tegemezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…